Maendeleo ya kweli ya Tanzania yatafanywa na Watanzania wenyewe

Hennes kolon

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
673
1,287
Watawala wangu kama hamtalishika Hilo neno hapo juu, na kulifanyia kazi kwa dhati yenu yote, sahauni kabisa kuwa na maendeleo kwenye nchi hii.

Nawaambia hivi hata mlete malaika kutoka mbinguni kamwe hamtayapata hayo maendeleo. Sio malaika tu hata Mungu mwenyewe aje hawezi kuwaletea maendeleo zaidi atawangalia nyuso zenu, mioyo yenu, akili zenu na kadhalika, halafu atajiondokea zake Mbinguni kwake.

Tangu Uhuru Hadi Sasa mmeleta wafanyabiashara wangapi kutoka mataifa ya mbali, je mlipata Nini!? mliyapata hayo maendeleo? Nipeni jibu. Wengi wamekuja wakachuma Mali na kuondoka zao makwao. Kesho Tena nyinyi huamka na kwenda kuwatafuta wengine, nao huja huchuma na kujiondokea makwao. Hii tabia mtaacha lini?

Hao mnawapigia kinanda huko misikitini na juzi mlikuwa kwenye madhabahu mkiendelea kuwapigia kinanda hawaji kutafuta kwa manufaa ya mataifa yao na familia zao? Naapa kwa nafsi yangu, Mungu anipe maisha marefu nishuhudie hayo mnayotaka kuyafanya, mapinduzi ya bandari.

Ngoja niishie hapa!
 
Back
Top Bottom