Maelezo ya mwanafunzi aliepigwa na walimu Mbeya

Maelezo ya mwanafunzi aliepigwa na walimu Mbeya

Walimu walifanya kosa ila hilo haliondoi ukweli kuwa huyo Dogo ni nunda Wa kutupwa... Kwa waliosoma somo la criminology watakuwa wanajua pa kimuweka huyu Dogo...

Hilo kama lisipojirekebisha na kuvimba kichwa na kauli za wanasiasa wanaolinda matumbo yao miaka si mingi tutaletewa habari zake hapa .....

Jaman hata sisi tulisoma na kufanya vikazi vya hapa na pale... Wanafunzi ambao zaidi ya 80% ambao hutoa sababu ya kuumwa huwa ni waongo wakubwa hivyo hivyo maofisini.... Morphologically na ukimuangalia anavyoongea + darasa lake yaani form two Mimi nampa sifa za kuwa mdogo wake scorpion yule mtoboa macho..

Mnaomtetea endeleeni tu hawa ndio wakikuweka anga zao tunabaki kusema mtuhumiwa akikamatwa anyongwe au apigwe risasi kwenye uwepo Wa watu
Acha kupotosha. Unachofanya hapa ni labelling unalazimisha huyo dogo aonekane deviant kutetea uhalifu aliofanyiwa na walimu wake.

Logic kwa waTz ngumu sana.....hapa tunashughulika na aina ya adhabu aliyopewa huyo dogo. Nakwambia walimu mnao tetea uhalifu huu mnajichosha bure tu kwasababu jamii imeshaona haipatani na AKILI kutumia utetizi "wanafunzi siku hizi manunda" ili mhalalishe vipingo vya kudhalilisha.

Mwisho unapaswa uelewe.....adhabu zinazozingatia heshima kwa wanafunzi zitaendelea na walimu wanaotenda jinai watashughulikiwa mara moja bila kuchelewa. Ole wako ugundulike...
 
Pamoja na yoote tutegemee kuona mambumbu wengi sana mitaani baada ya miaka kadhaa kwa hali hii
 
Ni vigumu kutoa hitimisho ila kama ni kweli anavyosema huyu mtoto, basi inaonekana ilikuwa ni "personal attack"

Kwanini baada ya wanafunzi wote kupewa adhabu huyu akatengwa kwa "extra punishment?

Huyu mwanafunzi inabidi awashtaki walimu wa mashambulizi ya mwilini yaani GBH- grievous bodily harm.

Sheria inasemaje na kifungo cha kosa hili?
Kwanini unadhani alitengwa
 
Jamani kama wewe ni madam , mwanafunz akikusumbua mwambie
I AIN'T YOUR MAMA

Na kwa mwalimu wa kiume ukisumbuliwa na limwanafunz mwambie
I AIN'T YOUR DAD
 
Ujue watu wana muweka yule dogo kama mtu asiye na kosa kwenye tukio hilo, na mi naona hiyo hatumtendei haki yeye mwenyewe dogo, sasa kwenye tukio kama hilo ata jifunza nini zaid ya kujiona mshindi tuu!!?
Ni ukweli usiopingika yawezekana dogo ni nunda wa kutupwa...je walichokifanya walimu ndio utaratibu?
Nakumbuka enzi zetu tulikuwa na manunda nini kilifanyika ni 'stick' tu hakuna mwalimu alierusha ngumi wala kibao utakula bakora mvua hadi utasimulia.
So kwa sasa tunatibu nidhamu ya walimu 'mabrazamen' ili watengeneze mazingira ya kuheshimika ili watusaidie kuwanyoosha wanafunzi kwa busara sio ngumi na mateke
[HASHTAG]#Mwalimu[/HASHTAG] anavaa kata K pia kakunja shati mwanafunzi nae the same unatarajia nini?
 
wekeni na maelezo ya mwalimu mbona upande mmoja
Ndugu hakuna wa kuhitaji maelezo ya mwalimu kwa sababu keshahukumiwa bila kujitetea hivyo hata akiongea haita saidia mwalimu si mtu wa kusikilizwa na jamii iwe kwa jema au baya polen sana walimu mema yenu mengi huwa hayaonekani kabisa hata yakiwa wazi lakin mabaya yetu hata yaliyo jificha yatatafutwa huko yaliko na kila mtu atakuwa muongeaji na msemaji.
 
Wanadhani wanajenga kumbe wanabomoa !
 
I don't care dogo dogo kasema nini au ikiwa maelezo yake ni sahihi au hapana... lililo wazi ni kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha kilichofanywa na those guys the so called walimu! Sasa tuseme alimvimbia huyo mwalimu; na hao wengine ambao waliingia kundini kuanza kumtandandika nao walikosewa nini? Au huko mashuleni ndo inavyokuwa... kwamba ugomvi dhidi ya mwalimu mmoja wengine wanaingilia?! Ni mambo ya wapi haya... those guys are monsters! Watu 5 wenye age above 20 mnamchangia mtoto ambae hata 18 haionekani kama amefika?! Halafu eti itengenezwe justification kwamba mara oh, watoto wa siku hizi; mara oh... acheni mambo yenu!
Kulikuwa na thread humu ya maelezo ya tukio, briefly: Dogo alikataa adhabu ya kawaida iliyotolewa kwa wote walioshindwa kufanya zoezi walilopewa, mwalim akataka kumlazimisha, Mwl akapigwa ngumi, walimu wakampeleka chumba cha walimu wakashindwa kumuadhibu coz alirusha makonde kisha akakimbia, mwalimu aliyekuwa nje akamdaka akamrudisha ofc, ndipo wakaamua kumaliza hasira zao
 
Usipate taabu, audio clip hii hapa wanafunzi wakielezea kilichotokea!!!

Na kama unataka maelezo ya texts ni kwamba, kwanza dogo hakuwepo siku ya test na kwa mujibu wa mwanafunzi mmoja ni kwamba alikuwa anaumwa! Siku ya siku, huyo Mwalimu akaja darasani na kuwataka ambao hawajafanya test watoke mbele... dogo nae akatoka! Kitu cha kwanza ambacho mwalimu alifanya ni kuwapa adhabu ya kupiga magoti... dogo akajitetea kwamba anaumwa! Baada ya hapo, teacher akaenda ofisini ambako alirudi na wenzake ili wamsaidie kuwaadhibu ambao hawajafanya hiyo tests... adhabu ilikuwa ni bakora! Dogo akahoji kwanini aadhibiwe kutofanya test wakati yeye hakuwepo siku ya test kv alikuwa anaumwa!

Teacher kuona dogo anahoji; akaona dogo anamletea kujua... akamtandika kofi!!

Kwanza kabla ya yote, huyo mwalimu angekuwa na busara angeenda kwanza kwa mwalimu wa darasa ku-verify ikiwa alikuwa ana taarifa za kuumwa kwa huyo mwanafunzi lakini kinyume chake, akachukua sheria mkononi!

Baada ya kashkashi ya dogo kutokuwa tayari kuadhibiwa kwavile aliamini hana kosa, ndipo walimu wengine wakaingilia wakaanza kumshushia dogo kisago... wakaona haitoshi, wakambeba hadi ofisini... huko ambacho kiliendelea wanafunzi hawakijui! Baada ya muda, walimu wakarudi tena na dogo darasani na kuendelea kushusha kipigo...!!!
 
Hao walimu nao sio kabisa mtu kashindwa kufuata vigezo muite mzazi wake, kama ingelikuwa mwanangu daaah ningeeleweka na vibaya....
 
Ni vigumu kutoa hitimisho ila kama ni kweli anavyosema huyu mtoto, basi inaonekana ilikuwa ni "personal attack"

Kwanini baada ya wanafunzi wote kupewa adhabu huyu akatengwa kwa "extra punishment?

Huyu mwanafunzi inabidi awashtaki walimu wa mashambulizi ya mwilini yaani GBH- grievous bodily harm.

Sheria inasemaje na kifungo cha kosa hili?
Miezi sita jela, au na faini isiyofika laki moja
 
kwa upande mmoja au mwingine dogo anaelekea Ana makosa.
nimejaribu kuwasikiliza wanafunzi wenzake jana kwenye redio wanavyo sema nikweli kwa tukio hilo lilifanyika baada ya mwanafunzi huyu kugomea adhabu ya push up iliyo tolewa na mwalimu huyo baada ya adhabu ya push up mwalimu akambia wanafunzi wapige magoti mwanafunzi akagoma kwa kusema anaumwa na goti

walienda mbele zaidi kuwa mwanafunzi huyu alishawahi kumgomea mwalimu huyo pale alipo mwambia avue sweta na mwanafunzi akagoma kwa madai kuwa mwanafunzi huyo anaumwa na kifua.

KWA NIONAVYO huyu mwanafunzi Ana kama ujeuri au kiburi kwa ninavyo elewa mimi mwalimu huwa anaumia pindi anapo towa adhabu na mwanafunzi akagoma inakuwa ni dharau.
na kwa sababu wengi tumekuwa wanafunzi inavyo julikana wanafunzi huwa wana wadharau sana walimu wanao kuwa field.
KWA UPANDE mwingine nao walimu hawakupaswa kumwazibu mwanafunzi kwa kiasi kile.
haku kukuwa na adhabu nyingine?
mwalimu alishindwa kumpeleka mwanafunzi kwenye ofisi ya nidhamu kama mwanafunzi alimuona anakosa?
Vipi mwalimu wa taaluma hayupo?
kabla ishu haija fika kwa mwalimu mkuu huwa unakuwa na ngazi mpaka ishu kama hiyo imfikie!

Hapo hata hao walimu watoe maelezo ya kujitetea bado wataonekana wana makosa ya kumshambulia pia haiwezi kumfanya mwanafunzi anakosa kwa kuwa swala lililopo kubwa ni juu ya kile kipigo
 
Ni ukweli usiopingika yawezekana dogo ni nunda wa kutupwa...je walichokifanya walimu ndio utaratibu?
Nakumbuka enzi zetu tulikuwa na manunda nini kilifanyika ni 'stick' tu hakuna mwalimu alierusha ngumi wala kibao utakula bakora mvua hadi utasimulia.
So kwa sasa tunatibu nidhamu ya walimu 'mabrazamen' ili watengeneze mazingira ya kuheshimika ili watusaidie kuwanyoosha wanafunzi kwa busara sio ngumi na mateke
[HASHTAG]#Mwalimu[/HASHTAG] anavaa kata K pia kakunja shati mwanafunzi nae the same unatarajia nini?
Yaani hakuna aliye furahia kile kitendi cha yule dogo kupigwa vile, ila sifurahii pia dogo kiachwa tuu kama walimkuta amesimama mahali flani halafu wakaanza tuu kumpiga, sioni haja ya kusema dogo kaonewa tuu, je naye hakumkosea mwalimu wake!!?,nataka nijue hilo ili nipime stori na dogobkuna sehem yake lazima ali takiwa ajifunze ika kwa hivi mmemuingezea ujeuri tuu hapo shule
 
Back
Top Bottom