Maelezo ya mwanafunzi aliepigwa na walimu Mbeya

Sasa tumesikia na tumeona pande zote, hao walimu pamoja na adhabu walizopata bado wasakwe na kufikishwa mahamani wote ili sheria ifuate mkondo wake
Kama kuna walimu wanaopigwa kama anavyodai mwanafunzi huyu basi hapa panahitajika uchunguzi wa ziada.
 
Ni vigumu kutoa hitimisho ila kama ni kweli anavyosema huyu mtoto, basi inaonekana ilikuwa ni "personal attack"

Kwanini baada ya wanafunzi wote kupewa adhabu huyu akatengwa kwa "extra punishment?

Huyu mwanafunzi inabidi awashtaki walimu wa mashambulizi ya mwilini yaani GBH- grievous bodily harm.

Sheria inasemaje na kifungo cha kosa hili?
 
I don't care dogo dogo kasema nini au ikiwa maelezo yake ni sahihi au hapana... lililo wazi ni kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha kilichofanywa na those guys the so called walimu! Sasa tuseme alimvimbia huyo mwalimu; na hao wengine ambao waliingia kundini kuanza kumtandandika nao walikosewa nini? Au huko mashuleni ndo inavyokuwa... kwamba ugomvi dhidi ya mwalimu mmoja wengine wanaingilia?! Ni mambo ya wapi haya... those guys are monsters! Watu 5 wenye age above 20 mnamchangia mtoto ambae hata 18 haionekani kama amefika?! Halafu eti itengenezwe justification kwamba mara oh, watoto wa siku hizi; mara oh... acheni mambo yenu!
 
Niimani yangu, kama ambavyo video ya kumpiga huyu kijana ilivyotumika kuwatia hatiani wale walimu, kumsimamisha kazi na kumshusha cheo aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya mbeya day, vivyo hivyo, video hii ikitumika kama sehemu ya ushahidi mahakamani, nawaona wale walimu wakirudi chuoni, mwalimu mkuu akirudi kazini.
Dogo amejichanganya kwelikweli katika maelezo yake.
Wanasheria wa mbeya, fursa ya kuwatetea watuhumiwa hiyo ishaiva.
 
Kama una macho basi yakusaidie kuona kuwa huyu mwanafunzi ni kirusi.

Hakuna kinachomkausha mate lakini analambalamba midomo.
Mtiririko wa story unajionyesha kuwa uko edited.
SOMO HUSIKA HALIFUNDISHWI NA WALIMU ZAIDI YA MMOJA anzieni hapo.
 
Niimani yangu, kama ambavyo video ya kumpiga huyu kijana ilivyotumika kuwatia hatiani wale walimu, kumsimamisha kazi na kumshusha cheo aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya mbeya day, vivyo hivyo, video hii ikitumika kama sehemu ya ushahidi mahakamani, nawaona wale walimu wakirudi chuoni, mwalimu mkuu akirudi kazini.
Dogo amejichanganya kwelikweli katika maelezo yake.
Wanasheria wa mbeya, fursa ya kuwatetea watuhumiwa hiyo ishaiva.
Huyu dogo anaonekana ni mkorofi.
 
Back
Top Bottom