Kizazi kijacho kitalelewa vipi?

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Nasikitika kusema kwamba sisi tutakuwa kizazi cha mwisho kuwa na wazazi wanaojielewa. Nasikitika kusema kwamba sisi ndio tutakuwa kizazi cha mwisho kuwa na mama bora na baba bora pia wanaojielewa.

Huenda labda mimi ni mpofu, lakini niwapashe tu kuwa nayaamini macho yangu kuliko ambavyo mnaziamini fikra zenu. Nakionea huruma sana kizazi kijacho, kimekosa wazazi wenye maadili na tabia njema.

Hapana, situkani ila nasema ukweli, kama ukweli wenyewe ni matusi basi acha niendelee kutukana. Mara zote huwa naongea ukweli hata kama nadanganya.

Kipindi wazazi wetu wanavuta hewa kumshukuru Mungu, ndio kipindi ambacho vijana wa sasa wanavuta shisha kumkufuru Mungu.

Vijana wa sasa ndio wazazi wa kizazi kijacho, poleni watoto mnaokuja mmekosa wazazi bora kama wetu. Mama zenu huku wapo Sinza, wavuvi camp na kitambaa cheupe wanauza nyumba zenu za kutokea.

Baba zenu wanaunguza sana maini, wanajichoma na moshi wengine wapo wanavaa suruali zao magotini. Daah! Mmekosa wazazi bora kabisa.

Mama zenu ndio hawa mabinti wa sasa ambao wanasagana, poleni sana watoto wa kizazi kijacho, hakika mmekosa wazazi wema.

Watoto mnaokuja, wazazi wenu sidhani kama watawalea kwenye maadili sahihi kama tuliyolelewa sisi. Wazazi wenu wajianikao uchi mtandaoni sidhani kama wana jema la kuwafundisha.

Wazazi wenu wasio na maarifa, wanasema hata kusoma vitabu ni kupoteza muda. Wazazi wenu sijui watawalea kwenye maadili ya aina gani, maana wenyewe tu wanatisha kwa wanayoyafanya sijui ninyi mtakuwaje maskini.

Baba zenu ndio hawa akina Chokuu, ambao wame left group ni upinde wamepinda kweli kweli na wanataka kupindishwa wafikishwe ambako mama zenu huwa wanafika.

Wazazi wenu ndio hawa ambao wanapenda tope wenyewe wanaita kisamvu, wanakosoa uumbaji wa Mungu wanapita walipokatazwa kupita, Astaghafirulaaah!

Sijui watoto mjao mtalelewa kwenye maadili gani, sababu hebu fikiri tu kama wazazi wenu wanabishana na Mungu nyie je maisha yenu yatakuwaje.

Wazazi wenu si ndio hawa vijana wa sasa, vijana ambao kupoteza simu inauma sana kuliko kupoteza bikra zao. Vijana hawa ambao wanapambana kumiliki simu za bei kali wakati kichwani hawana future wala positive mindset.

Poleni sana watoto wajao, baba zenu wamejikita huku kwenye michezo ya kubahatisha kama sehemu kubwa ya ajira zao. Yaani wao ili wale na kuvaa, basi ni lazima Barcelona ashinde dhidi ya Mallorca.

Kizazi kijacho kimekosa wazazi bora, maana vijana wa sasa ndio hawa kila siku wanajiua. Mara ngapi umeshuhudia kwenye taarifa za habari watoto wa rika dogo wakijinyonga kwa sababu zisizo na mashiko.

Wazazi wa kizazi kijacho, ndio hawa vijana wa sasa ambao wanateseka sana na mapenzi. Wamejawa na ulevi, uzinzi, usaliti na stori nyingi za dhambi zenye aibu na mashaka lukuki.

Wazazi wa TikTok ambao kutwa ni matusi, kujianika uchi na kumkufuru Mungu. Wengine wanaenda mbali na kuzichezea hadi dini eti wanaimba "Yesu nipe mimba ya Imani" hawana hata uoga. Ni laana isiyo na maana.

Kizazi kijacho kimekosa sehemu kubwa ya malezi ya maadili mema na uadilifu. Nathibitisha kusema hivyo !!
1709135318003.jpg
 
Mama zenu ndio hawa mabinti wa sasa ambao wanasagana, poleni sana watoto wa kizazi kijacho, hakika mmekosa wazazi wema.

Ujumbe ufike kwa yule binti msagaji ambaye alitangaza kutaka kupewa mbegu tu halafu mkataba wa ubaba kwa mwanaume aliyelala naye ukaishia hapo...

Halafu baada ya kupata huyo mwanaharamu, kizazi cha sasa kikakusanyika kuyoa pongezi...🤔🤔

Maisha yanaenda kasi sana...
 
Kama wazazi wenu walikua bora, wakawapa nyie malezi bora, sasa iweje kizazi kijacho kiharibike?

Nyie mliolelewa na wazazi bora, wote mmekua wazazi? wote mmekua watu bora?

Kukariri mistari ya kitabu cha hadithi ndo kuwa mtu bora? Basi kila aliyekariri angekuwa mtu bora....

Mtu anaefanya maovu sasa, una uhakika ataendelea hivyo milele?

Mnachagua visa(cherrypicking) ili muwanyoshee vidole wengine nyie mjisikie vizuri.
 
Nakisikitikia kizazi kijacho maisha yao yameharibiwa na babu zao kwa kuwapa malezi ya kishenzi vijana wa sasa.

Hiki tunachokiona ni matokeo ya malezi ya kipumbavu kutoka kwa hawa wazee wanaojitapa walipata malezi mazuri kutoka kwa wazazi wao.
 
Sometimes watu wanakengeuka tu. Hujaona kuna familia zinenyookq ila anatokea mtoto mmoja kakengeuka balaa?
 
Kama wazazi wenu walikua bora, wakawapa nyie malezi bora, sasa iweje kizazi kijacho kiharibike?

Nyie mliolelewa na wazazi bora, wote mmekua wazazi? wote mmekua watu bora?

Kukariri mistari ya kitabu cha hadithi ndo kuwa mtu bora? Basi kila aliyekariri angekuwa mtu bora....

Mtu anaefanya maovu sasa, una uhakika ataendelea hivyo milele?

Mnachagua visa(cherrypicking) ili muwanyoshee vidole wengine nyie mjisikie vizuri.
Percentage comparison. Wema hamkosekani na wabaya hawakosekani kila kizazi
 
Sometimes watu wanakengeuka tu. Hujaona kuna familia zinenyookq ila anatokea mtoto mmoja kakengeuka balaa?
Hakuna kukengeuka ndiyo malezi aliyopewa. Vijana wengi wanaharibika wakiwa bado chini ya uangalizi wa wazazi au walezi.

It means, wanajivunza tabia mbovu mbele ya macho ya wazazi wao, ila wazazi wanakuja kujifanya kushtuka tatizo limeshakuwa kubwa.
 
Mna shida sana nyie mliozaliwa miaka ya 90-2000's
Sisi tuliozaliwa miaka ya 70's-80 tuna unafuu mkubwa Sana wa maadili ..
Ebu fikiria watoto wa mwijaku, babalevo na akina gigy money watajifunza kipi kupitia wazazi wao?
Kweli kabisa , kizazi chenu japo uhuni ulikuwepo ila watu walikuwa wanabadilika, wanajielewa sana ,wapambanaji na watafutaji tofauti na sasa vijana wadogo wana mambo mengi ya hovyo kibaya zaidi ni kushindwa kujicontrol na kujinasua .

Wakati namaliza form 4 shuleni kwetu hali ya vijana nilioiacha ilikuwa mbaya sana mpaka ikafanya nifikiria sana kuhusu future vijana wanaokuja katika Taifa hili ,kipindi nipo A_level Kuna siku class mwalimu aliwahi kusema "Kama nyinyi ndio wasomi mmefaulu je ambao wako mitaani wako hali gani ?
 
Hakuna kukengeuka ndiyo malezi aliyopewa. Vijana wengi wanaharibika wakiwa bado chini ya uangalizi wa wazazi au walezi.

It means, wanajivunza tabia mbovu mbele ya macho ya wazazi wao, ila wazazi wanakuja kujifanya kushtuka tatizo limeshakuwa kubwa.
Umeamua kubisha tu. Nimekwambia same family wanatoka watoto wamenyooka na mwingine kapinda kabisa. Kwa maelezo yako huyu mwingine kapewa malezi tofauti na wenzie?
 
Nasikitika kusema kwamba sisi tutakuwa kizazi cha mwisho kuwa na wazazi wanaojielewa. Nasikitika kusema kwamba sisi ndio tutakuwa kizazi cha mwisho kuwa na mama bora na baba bora pia wanaojielewa.

Huenda labda mimi ni mpofu, lakini niwapashe tu kuwa nayaamini macho yangu kuliko ambavyo mnaziamini fikra zenu. Nakionea huruma sana kizazi kijacho, kimekosa wazazi wenye maadili na tabia njema.

Hapana, situkani ila nasema ukweli, kama ukweli wenyewe ni matusi basi acha niendelee kutukana. Mara zote huwa naongea ukweli hata kama nadanganya.

Kipindi wazazi wetu wanavuta hewa kumshukuru Mungu, ndio kipindi ambacho vijana wa sasa wanavuta shisha kumkufuru Mungu.

Vijana wa sasa ndio wazazi wa kizazi kijacho, poleni watoto mnaokuja mmekosa wazazi bora kama wetu. Mama zenu huku wapo Sinza, wavuvi camp na kitambaa cheupe wanauza nyumba zenu za kutokea.

Baba zenu wanaunguza sana maini, wanajichoma na moshi wengine wapo wanavaa suruali zao magotini. Daah! Mmekosa wazazi bora kabisa.

Mama zenu ndio hawa mabinti wa sasa ambao wanasagana, poleni sana watoto wa kizazi kijacho, hakika mmekosa wazazi wema.

Watoto mnaokuja, wazazi wenu sidhani kama watawalea kwenye maadili sahihi kama tuliyolelewa sisi. Wazazi wenu wajianikao uchi mtandaoni sidhani kama wana jema la kuwafundisha.

Wazazi wenu wasio na maarifa, wanasema hata kusoma vitabu ni kupoteza muda. Wazazi wenu sijui watawalea kwenye maadili ya aina gani, maana wenyewe tu wanatisha kwa wanayoyafanya sijui ninyi mtakuwaje maskini.

Baba zenu ndio hawa akina Chokuu, ambao wame left group ni upinde wamepinda kweli kweli na wanataka kupindishwa wafikishwe ambako mama zenu huwa wanafika.

Wazazi wenu ndio hawa ambao wanapenda tope wenyewe wanaita kisamvu, wanakosoa uumbaji wa Mungu wanapita walipokatazwa kupita, Astaghafirulaaah!

Sijui watoto mjao mtalelewa kwenye maadili gani, sababu hebu fikiri tu kama wazazi wenu wanabishana na Mungu nyie je maisha yenu yatakuwaje.

Wazazi wenu si ndio hawa vijana wa sasa, vijana ambao kupoteza simu inauma sana kuliko kupoteza bikra zao. Vijana hawa ambao wanapambana kumiliki simu za bei kali wakati kichwani hawana future wala positive mindset.

Poleni sana watoto wajao, baba zenu wamejikita huku kwenye michezo ya kubahatisha kama sehemu kubwa ya ajira zao. Yaani wao ili wale na kuvaa, basi ni lazima Barcelona ashinde dhidi ya Mallorca.

Kizazi kijacho kimekosa wazazi bora, maana vijana wa sasa ndio hawa kila siku wanajiua. Mara ngapi umeshuhudia kwenye taarifa za habari watoto wa rika dogo wakijinyonga kwa sababu zisizo na mashiko.

Wazazi wa kizazi kijacho, ndio hawa vijana wa sasa ambao wanateseka sana na mapenzi. Wamejawa na ulevi, uzinzi, usaliti na stori nyingi za dhambi zenye aibu na mashaka lukuki.

Wazazi wa TikTok ambao kutwa ni matusi, kujianika uchi na kumkufuru Mungu. Wengine wanaenda mbali na kuzichezea hadi dini eti wanaimba "Yesu nipe mimba ya Imani" hawana hata uoga. Ni laana isiyo na maana.

Kizazi kijacho kimekosa sehemu kubwa ya malezi ya maadili mema na uadilifu. Nathibitisha kusema hivyo !! View attachment 2930113
Walaumiwe wazazi wa 1980's, wao wamelelewa vizuri katika maadili halafu wanakuja kutuletea malezi ya hovyo kwa vijana
 
Back
Top Bottom