Mabroo acheni kuwasakama wadogo zenu ambao hawajatoboa

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,823
Kumekua na kasumba ya mabroo ambao washatoboa kutushambulia wadogo zao ambao bado tunajitafuta bila kuangalia kwa upana utofauti wa mazingira ambayo wao walikutana nayo na sisi tumekutana nayo

Mabroo ukweli ni kwamba wengi wenu mmeingia mtaani zama za kitonga (awamu za Mkapa na Kikwete), hamjua kuanzia zama za vyuma kukaza hustle za mtaani kuanzia kutafuta ajira, kuanzisha na kudumu kwenye biashara mpya hali ilikuaje. Ndio maana mnaishia kutuona wadogo zenu wavivu, wazembe au mazombi fulani yasiokua na akili.

Mabroo mmefika hatua ya kuwadhihaki graduates na kusema hawajui chochote, chuo wameenda kusomea ujinga n.k. mkiwapokea madogo wa field au wageni kazini ni kuwasimanga tu hawajui hiki hawajui kile. Hivi unategemea dogo alietoka shule awe na ujuzi na uzoefu sawa na wewe uliopo hapo kazini kwa miaka 10+?

Mabroo ukweli ni kwamba wengi wenu you are nothing special, kilichowaokoa mlibahatika tu kuingia mtaani kipindi ambacho kulikua na uwiano mzuri wa fursa na wahitaji, tofauti na baada ya awamu ya 5 fursa zimekua chache sana huku wahitaji wakiwa wengi sana.

Mabroo mnachukulia mambo kirahisi rahisi sana. Unakuta bro anakwambia tu nenda kawe winga Kariakoo, jichanganye kwenye vijiwe bodaboda utapewa pikipiki, piga picha rusha mtandaoni kutafuta wateja. Hivi mabroo wangapi mnapiga hizo mishe? Kwanini msitushirikishe kwenye michongo yenu badala ya kutuambia hizo theories pendwa za motivational speakers

Utaamka tu asubuhi uende Kariakoo watu wakuamini uwe winga? Nani atakupa pikipiki au bajaji yake akiwa hakujui eti kisa tu umeshinda hapo kijiweni kwa wiki moja?, mnajua cost ya bando la kushinda mtandaoni siku nzima ni hela ya kula breakfast na dinner?

Mabroo jueni zama zimebadilika kazi ambazo zilikua zinapuuzwa tu zama zenu kama kuwa winga, konda wa mabasi, kuosha magari car wash n.k kwa sasa zinagombaniwa na kuzipata ni lazima uwe na mtu wa kukushika mkono (connection). Uwiano wa kutoboa ni 10:5000, yaani katika watu 5000 watakaotoboa ni 10 tu mfano mzuri angalia watu walioitwa katika interview ya TRA majuzi halafu fatilia idadi ya watu wanaotakiwa kuajiriwa.

Mabroo wekeni pembeni ego na ujuaji angalieni uhalisia wa mambo. Serikali haijaajiri wala kupandisha mishahara kwa miaka mitano mfululizo, watu wanaachishwa kazi kwa maelezo ya vyeti feki, sekta binafsi inapigwa vita, matajiri wamefanyiwa figisu(Manji, Mo. Mbowe n.k). Katika hali kama hiyo graduate alieingia mtaani hana connection unatarajia atakutana na mazingira gani katika heka heka za kujitafuta?. Hata nyie mabroo mngekua ndio sisi mngetaabika pia.

Mabroo msitudhihaki msituone wajinga na wazembe. Heshimuni hustle zetu pale mnapoweza kutuongoza au kutupa connection fanyeni hivyo pale ambapo unaona huwezi kusaidia chochote tuacheni tupambane na hali zetu, If you can't help at least don't insult.

Ingawa sometimes mnazingua ila majobless tunawapenda sana mabroo zetu.
 
Mimi nashauri nenda kasome ukiwa umejitafuta mtaani ujue ukisha soma ukiingia mtaani ila utaloambiwa unahisi unaonewa wakati hayo maneno akiambiwa mtu ambae sio msomi anachukulia kama vitu vya kumsogeza mbele ila msomi anahisi anaonewa kisa yeye msomi
 
Msoto wa jobless we acha tu, Mabroo hawataki hata kutushika mkono. Kutwa kucha kutuhadithia upuuzi wa ndugu zao walowatoa mbwinde huko na kuwapachika Kweny vitengo kisha wanaleta hasara na kuwaharibia.
Mwingine anakuadithia jinsi anavyopiga hela kwenye mishe zake ukimuomba akuunganishe anaanza visingizio utasikia hauwezi wewe na blah blah zingine kibao
 
Hao mabroo wenyewe misifa yao kibao uchoyo Moto, mtoto wa field akienda na vitu vya kula wanashobokea tu, alafu kingereza wanababaika babaika wanauliza uliza tu, ukivaa vizuri mimacho inawatokatoka.
aisee kumbe wenzetu mnatolewa mimacho
 
Kazi buti comred utatoboa tu, hizo kauli zao za dharau chukua kama fursa na maitisha ya kukuchochea kupambana kwa bidii zaidi bila kuchoka wala kukata tamaa, im sure utatoboa na atapata aibu sana once na wewe uko chuma maisha.
Mimi nawatakia mema mabroo wote na Mungu awazidishie na wala sipambani maisha ili kuwa-prove wrong ila kiukweli mabroo sometimes wazingua
 
Back
Top Bottom