Madiwani wa CHADEMA kata ya Kitangiri na Igoma wanyang'anywa kadi za uanachama

Kama ni kwa sababu ya usaliti wanastahili, naupongeza uamzi wa CDM! Uadilifu na Uwajibikaji vilindwe kwenye chama!!
Ng'oa magugu shamba liwe safi. tusilee ujinga kama magamba. ni gharama sana. Samaki mkunje angali mbichi!
 
Kanuni ya kujenga ni nzuri ijapo ni ngumu sana ila kwa kuwa ni nzuri basi na tuifate,yaani ni lazima uvunje ndo ujenge upya ....we break up so as to make up.
 
Haki ya mama,huyu jamaa wa Igoma kaanza upuuzi wake huo siku nyingi na sio siri,anataka kumpindua Mh.Wenje Wa Nyamagana,na sasa anatumiwa na magamba ya mwanza.We dogo,elimu yako mzuri,unajua kujiadress,Matata ni tofauti sana na wewe,utapotea kabisa ktk siasa.
 
Nadhani huyu ni boflo.
Fikiria kama CHDEMA kitaanza kulea wasaliti kama hawa, hakitafika mbali, Kumbuka pamoja na Degree yake lakini bado haiwasaidii wananchi wa Igoma. maana kwa taarifa hata wananchi walishamchoka maana anausaliti wa wazi. Kuna kipindi meya alikwenda Igoma kikazi, akafanya mkutano pale Igoma, haka mnakokaita msomi kakaja katikati ya mkutano kakadai kwanini meya huyo kaingia sehemu yake bila taarifa? Wananchi walitaka kukachapa hapohapo. Kanashindwa kujua kuwa pamoja na yote meya huyo pia ni mbunge wa eneo hilo, kwa hiyo bado ni bosi wake. Pambafu sana haka.

shangaa huyu gamba vipi?
 
Cdm hakimfai tunamkaribisha ccm.Sidhan kama ni solution cdm kuendelea kufukuza wanachama,inaonesha ni watu wanaokurupuka,kwan hawana kamati ya maadili ya chama ambapo mwanachama anapokosea anawekwa kitimoto.Hawa jamaa tukiwapa nchi tutaingia machafukon coz chama hakijaiva kukamata dola, kama tu mtu mmoja ndan ya chama tena diwan anaweza kuyumbisha kiasi hicho,hiki ni chama cha watu wa kasikazin tuwaachie wenyewe.

Chadema huwa wanafanya kweli mtu akikosa na akadhihirika amekosa hata baada ya utetezi wake anafukuzwa kwa mujimu wa taratibu na sheria za chama , hakuna kutishana nyau kama ccm wanavoimba wimbo wa gamba miaka mitatu sasa lakini hakuna hata mjumbe wa nyumba kumi aliyetimuliwa! Dhana ya uwajibikaji ndani ya CDM inapewa kipaumbele bila kujali cheo cha mtu! Shoka limewekwa tayari kumuelekea Shibuda stay tuned!!CDM mean what they say!
 
chadema wataalam wa kuvuana uanachama

offcourse CDM hawawezi kubeba mzigo wa viongozi wabovu kuna hazina kubwa ya viongozi ukikosea taratibu na sheria off you go anakuja mwingine ipo kama japan ndani ya miaka 3 kuna mawaziri wakuu karibu sita,. lengo ni kusimamia dhana ya uwajibikaji!!ccm watu wanafanya makosa ya wazi kabisa lakini unasikia mtu anasema sijiuzulu ng'o na aliyemteua yupo anakaa kimya dhana hiyo haipo CDM!!
 
Sielewi ni namna gani gani mtu anayetumia vizuri uwezo wake wa kufikiri anaweza ku-conspire na ccm?! Kwangu mimi ni afadhali ku-conspire na mbuzi kuliko ccm. Jamani, anayejua anisaidie kuelewa.
 
chadema kweli chama dume.
naona mnamandaa shibuda kisaikolojia,nyie mnafaa kuongoza hili taifa letu kazeni buti 2015 si mbali.
 
movement for chagga kwisha habari yake watawafukuza wote, nimegundua kila anayetaka uongozi anataka kujinufaisha yeye binafsi siyo wananchi.
 
Cdm hakimfai tunamkaribisha ccm.Sidhan kama ni solution cdm kuendelea kufukuza wanachama,inaonesha ni watu wanaokurupuka,kwan hawana kamati ya maadili ya chama ambapo mwanachama anapokosea anawekwa kitimoto.Hawa jamaa tukiwapa nchi tutaingia machafukon coz chama hakijaiva kukamata dola, kama tu mtu mmoja ndan ya chama tena diwan anaweza kuyumbisha kiasi hicho,hiki ni chama cha watu wa kasikazin tuwaachie wenyewe.

You Sound like mbaguzi vile...
 
movement for chagga kwisha habari yake watawafukuza wote, nimegundua kila anayetaka uongozi anataka kujinufaisha yeye binafsi siyo wananchi.

Chadema hawana shukurani leo Matata ana thamani tena wakati ndio kaijenga Chadema Mwanza, huyu dogo mwingine wa Igoma nae kafukuzwa?
 
Huwa Nachukia watu wanapoleta personal interest kwenye mambo ya public. Hakika wavuliwe Uanachama hawafai.
 
Back
Top Bottom