Madiwani wa CHADEMA kata ya Kitangiri na Igoma wanyang'anywa kadi za uanachama

Sheshejr

JF-Expert Member
Jan 14, 2012
434
82
Hiyo imetokana na mvutano uliokuwepo katika vikao vya halimashauri ya jiji la Mwanza ambapo diwani huyo (wa Igoma na mwenzake wa Kitangiri) pamoja na madiwani wengine kutoka CCM waliungana kujaribu kumng'oa Meya wa jiji (kutoka CHADEMA) kwa madai kuwa anaonyesha udhaifu mkubwa wa kuliongoza jiji.

Inahisiwa ni kutokana na majeraha aliyopata diwani huyo kijana na msomi pekee wa ngazi ya degree kati ya madiwani wote wa halmashauri ya jiji la Mwanza ya kuukosa umeya mwaka 2010.

Taarifa kamili zitatolewa na viongozi wa CHADEMA kitaifa.
 
Cdm hakimfai tunamkaribisha ccm.Sidhan kama ni solution cdm kuendelea kufukuza wanachama,inaonesha ni watu wanaokurupuka,kwan hawana kamati ya maadili ya chama ambapo mwanachama anapokosea anawekwa kitimoto.Hawa jamaa tukiwapa nchi tutaingia machafukon coz chama hakijaiva kukamata dola, kama tu mtu mmoja ndan ya chama tena diwan anaweza kuyumbisha kiasi hicho,hiki ni chama cha watu wa kasikazin tuwaachie wenyewe.
 
Siasa, siasa, siasa, mhhhhhhhhhhhhhhhh. Eti unatakiwa ufumbe mdomo hata kama yanayofanywa na chama chako hukubaliani nayo, ngoja tuone huu mchezo.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Kamati kuu ya CHADEMA mkoa wa mwanza imewanyang'anya kadi za uanachama madiwani wa kata ya kitangiri HENRY MATATA na ADAM CHAGULANI wa kata ya igoma. Taarifa zaidi zinafuta
 
Hapo ndo akili yako ya kufikili ilipoishia! Mnaweweseka hata penye hamna
Cdm hakimfai tunamkaribisha ccm.Sidhan kama ni solution cdm kuendelea kufukuza wanachama,inaonesha ni watu wanaokurupuka,kwan hawana kamati ya maadili ya chama ambapo mwanachama anapokosea anawekwa kitimoto.Hawa jamaa tukiwapa nchi tutaingia machafukon coz chama hakijaiva kukamata dola, kama tu mtu mmoja ndan ya chama tena diwan anaweza kuyumbisha kiasi hicho,hiki ni chama cha watu wa kasikazin tuwaachie wenyewe.
 
Tutafika tu katika kuiweka tanzania mikononi mwa wazalendo. Mungu ibariki tanzania mungu ibariki chadema na dk slaa......semeni amina
 
Kama kweli hizo tuhuma dhidi yake huyo diwani ni za kweli basi chama ni lazima kimwajibishe kwani hatuwezi kuruhusu wachumia tumbo sample kama ya shibuda kuunda alliance na magamba kwa ajili ya utashi binafsi wa kisiasa.
CHADEMA HIYO NDIO DAWA PEKEE KWA ANAYELETA UFARAO NDANI YA CHAMA CHETU KWANI CDM INA WATU WENGI NA HATUWEZI KUWA WATUMWA KWA WAPUUZI WACHACHE KAMA HAWA.
 
Cdm hakimfai tunamkaribisha ccm.Sidhan kama ni solution cdm kuendelea kufukuza wanachama,inaonesha ni watu wanaokurupuka,kwan hawana kamati ya maadili ya chama ambapo mwanachama anapokosea anawekwa kitimoto.Hawa jamaa tukiwapa nchi tutaingia machafukon coz chama hakijaiva kukamata dola, kama tu mtu mmoja ndan ya chama tena diwan anaweza kuyumbisha kiasi hicho,hiki ni chama cha watu wa kasikazin tuwaachie wenyewe.

Nakubaliana na wewe kuwa CCM ndiko kunakomfaa huyu diwani. Kinachouwa CCM ni kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi magumu. Na la kushangaza sasa hivi CCM wanatamba kuwa ndicho chama kinachoruhusu demokrasia! Yaani unaacha kuwachukulia watu wanaokwenda kinyume na maadili ya chama hatua kwa visingizio vya demokrasia! Au unaacha kufukuza watu wazembe (soma report ya CAG) kwa sababu ya demokrasia? Wanachofanya CHADEMA ndicho kinatakiwa kwa hapa tulipofikia Tanzania. Mijadala hakuna.
 
Sababu ni kuwa walikua wanamhujumu meya kwa kutumiwa na magamba ili kukwammisha maendeleo aonekane kashinwa,na mmoja kati yao ni hasira za kukosa umeya sasa akaamua kufanya mambo kisaliti
Source.?? usisahau kutuwekea na sababu za hatua hiyo..
 
Back
Top Bottom