Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,815
- 11,992
Hii video ni eneo la Mtakuja lipo Igoma kuelekea Kakebe, ni moja ya maeneo hatari kwa usalama wa watu kwa jinsi lilivyoharibu ardhi.
Eneo hilo lipo karibu na Mto unaotenganisha Kakebe na Mtakuja.
Diwani wa eneo hilo pamoja na maafisa mazingira wa Jiji la Mwanza wanajua na hawataki kufanyia kazi.
Mwenyekiti wa eneo hilo la Mtakuja akiulizwa anasema hana muda wa kushughulikia kero za barabara zote za eneo hilo hatarishi kwa mmonyoko wa udongo na hatarishi kwa wakazi wa Mtakuja.
Aidha, eneo hilo hakuna miundombinu ya mfereji wa kupitisha maji, hali hiyo ilisababisha hata Wanafunzi wa maeneo hayo kufika Shule ya Msingi Mtakuja au Igoma C kupata wakati mgumu na kifo kimoja cha Mwanafunzi wa Darasa la Nne kuripotiwa kutokea mwezi wa nne 2022.
Hakuna juhudi za ujenzi wa daraja wala njia mbadala ya kuvuka hata muda wa mvua za masika.
Hivyo, tunaomba mheshimwa Mkuu wa Mkoa Makala afike kujionea eneo hilo hatarishi.