Chama lazima kionyeshe kina miongozo isiyoyumbishwa. Kinaendeshwa kwa katiba mathubuti. Kina viongozi wenye kufuata maadili. Ukomavu na utawala wa sheria, haki na usawa unaanzia nyumbani. Madiwani wa Arusha wameonyesha ukaidi, dharau, utovu wa nidhami, shiriki na mbwa mwitu. Hawawezi kuaminiwa wala kuthaminiwa tena ndani ya chama. Vyovyote vile haingii akilini kufikia muafuka wa kufanya kazi na CCM chama tunachoamini ni cha kifisadi bila kuhakikiwa na vikao halali vya chama.
Pili siamini kwamba Dr Slaa alikaa chumbani mwenyewe na kufikia maamuzi ya kuwawajibisha wale madiwani. Dr ni katibu Mkuu, baada ya vikao halali vya chama wameona Madiwani walikengehuka, tamko limetolewa waachie pipi waliyopewa na CCM. Madiwani wamegoma na kuanza kutoa lugha za maudhi, dhalilishi, vitisho nk, jeuri hii wanaitoa wapi???????????????????
Siasa za makundi zinadhoofisha sana vyama vya siasa. Nakumbuka Joe liberman wa Democrati part nchini USA alipoamua kuungana kihoja na GOP alitemwa na Chama chake bila kujali kwamba wangepoteza jimbo. Ile ilionyesha sera na falsafa za chama ndizo nguzo imara za chama. Spika wa bunge la USA Boehner alisema tofauti zake na Obama ni pamoja na wao kila mmoja kuchagua chama cha siasa tofauti kwani vina mitazamo tofauti.
Madiwani wa Arusha kama wamekataa maelekezo ya viongozi, na vikao vya juu vya chama wanatakiwa kuwajibishwa. CDM lazima ijue kuwa haipambani na Madiwani wa Arusha tu ila inapamabana na mbinu chafu za CCM kujaribu kusambaratisha chama. Ni wakati wa kutuma ujumbe mahususi si kwa madiwani tu ila na kwa mawakala wao wanaoona kuleta migogoro ndani ya chama kunawasaidia wao.
Madiwani wachukuliwe hatua dhabiti za kinadhamu. Ikibidi wafukuzwe hata chama. Leo CDM wakilegalega kuchukua hatua kali watakuwa wanatoa tafsiri nyingi sana. Nataka kuona chama cha siasa kisichoogopa kuwajibisha watu kwa haki. Kesho kikiwa ikulu kitakuwa na wengi wa kuwaenzi na kuwawajibisha. Haki itendeke, madiwani waamue kuitumikia CDM au kutumikia CCM.
CDM waonyeshe uimara wao kuilinda katiba, na maamuzi ya vikao halali vya chama. Hili litakuwa fundisho kwa miaka mingi ijayo dhidi ya walowezi.
Ni mimi
Chief Mkwawa wa Kalenga