Madiwani Tunduma wabebeshwa lawama za kuua biashara

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,319
24,220
08 April 2023
Tunduma, Tanzania

BARAZA LA MADIWANI TUNDUMA LAWAMANI KWA KUUA UCHUMI


Baraza la Madiwani linaloongozwa na CCM la mji wa Tunduma walaumiwa kuua mzunguko wa biashara na uchumi wa wananchi ktk mji wa Tunduma na matokeo yake sasa wafanyabiashara wanakwepa kununua mizigo ktk mji huo wa mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Hilo linatokana na amri ya baraza la madiwani kukazimisha vyombo vya usafiri kuishia kituo cha Mpemba na hivyo abiria na wafanyabiashara wenye mizigo kulazimika kuingia gharama zingine za ziada kutika mjini Tunduma au kutoka mjini Tunduma kwenda kituo hicho cha Mpemba ambacho kipo nje ya mji kusiko na maduka wa makazi mengi ya watu.

Viongozi wa CHADEMA imebidi waingilie kati kuishauri baraza la madiwani likilisheheni wanachama wa CCM kutokana na uchaguzi wa 2020 kuwa waruhusu abiria na wafanyabiashara wanaotumia vyombo vya umma vya usafiri kama mabasi, coaster viruhusiwe kuingia mjini Tunduma baada ya vyombo hivyo kupita kituo cha Mpemba kulipa ushuru wa stendi maana wamiliki wa vyombo vya usafiri wapo tayari kuwapeleka na kuwachukua wateja wao toka mjini Tunduma na kupitia kituo cha Mpemba bila kuwatoza nauli ya ziada vyombo hivyo vya usafiri vikitokea Sumbawanga, Mbeya, Dsm n.k
1680955160259.png

Picha kwa hisani ya https://tundumatc.go.tz/new/mkurugenzi-wa-tunduma-asherehekea-siku-ya-baba-wa-taifa-standi-ya-mabasi

Abiria na wafanyabiashara hulazimika kukodisha bajaj, hiace, pikipiki kutoka na kwenda kituo kipya cha mabasi cha Stendi ya Mpemba hivyo kuingia gharama kubwa kumalizia safari au kuaza safari zao hivyo sasa wanaukwepa mji wa Tunduma na kupelekea kuua mzunguko wa biashara ktk halmashauri ya mji wa Tunduma.
 
Tunduma, Tanzania

Mwakajoka naye atoa ushauri kuhusu stendi ya Mpemba Tunduma kuwa karaha kwa wananchi, wageni na wafanyabiashara wa ndani na kimataifa toka Zambia, DR Congo, Republic of South Africa, Zimbabwe n.k

 
Maamuzi ya kijinga kwelikweli hakuwa sababu ya gari za abiria kuishia Mpemba.
Enyi madiwani la 7B kuweni wabunifu kupata vyanzo mbadala vya mapato.
 
Back
Top Bottom