Dola milioni 27 kuondoa foleni ya malori Tunduma

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
34
30
Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amesema zaidi ya Dola za Marekani milioni 27 zimetengwa kuondoa foleni katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe.

Aidha amewahakikishia wadau wanaotumia kituo cha forodha Tunduma kuvusha mizigo kupitia Nakonde upande wa Zambia kuwa kufuatia maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia Haikande Hichilema kuwataka watendaji kuhakikisha changamoto zote zinazowakuta wasafirishaji mizigo kutatuliwa kwa haraka ambapo utekelezaji umeanza.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo jana mjini Tunduma, mkoani Songwe wakati wa kikao cha kujadili mpango wa kuondoa msongamano mpakani hapo na kurahisisha biashara.

Kikao hicho kiliwaleta pamoja taasisi za serikali kuu zinazohusika na mpaka huo, Jeshi la Polisi, Wizara ya Ujenzi na uongozi wa mkoa wa Songwe.

Amesema wasafirishaji kwenda nchi za Zambia, DRC, Zimbabwe na nchi nyingine tayari Trade Mark East Afrika na Benki ya Dunia (WB) wamekubali kugharamia mpango kabambe wa maboresho mradi wa mwaka mmoja utakaogharimu dola za Marekani milioni 27.

Prof.Kahyarara amesema mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja na serikali itahakikisha unakamilika ili kuondoa kero hiyo inayoikosesha nchi mapato.

"Mradi utakapokamilika utawezesha kituo hicho kuwa na mifumo inayosomana kwa kuwa na 'scanner' za kisasa zinazotumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA hatua itakayoongeza ufanisi na ushindani kwa Bandari ya Dar es Salaam," amesema.

Mwisho amesisitiza hatua hiyo ni kati ya mageuzi makubwa yanayotekelezwa na Rais Samia kwa lengo la kuimarisha bandari na kukuza biashara na kukuza uchumi.
 
Bima kwa watoto je
Cupace20230923075117117.jpg
 
Back
Top Bottom