Hivi hili la halmashauri mji Tunduma kuharibu masoko lina nia gani?

ngetela

Member
Oct 12, 2021
56
32
Mfululizo wa kubomoa kuharibu masoko stendi na sehemu zingine za kazi umekuwa kwa kasi sana hapa tunduma. Hatukatai kuboresha mji lakini kwann huu ufanyaji kazi umekuwa kwa haraka kuharibu kila soko .Walianza na stendi wakahamishia kilometer 7 kutoka ilipokuwa ya awali yaani katikati ya mji wakidai wanajenga soko la mamilioni mpaka sasa ni utopolo tu . Wakaja soko la majengo miezi mitatu sasa wameishia kuchimba msingi tu soko linahitaji lijengwe Kwa miezi nane kwa ahadi zao. Na sasa wameingia soko la kimataifa la mazao na kuwambia wamiliki wa vibanda waachie vibanda haieleweki kwamba wanataka kifanyia nini. Wanatunduma wazalendo tunauliza nani anapanga huu ujinga ni madiwani au ni mgurugenzi na serikali kuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom