Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,605
Bajeti ya Mwigulu imeshaonesha kwamba haitakuwa na matokeo mazuri kwenye uchumi. Hisia za kodi kuwa kubwa tena kwenye bidhaa muhimu ni dhahiri.
Kwenye uchumi, kuna kitu tunakiita 'Equillibrium Price' - yaani ile bei ambayo mnunuzi na muuzaji wataafikiana. Sasa kuna baadhi ya bidhaa ambazo kulingana na kupanda kwa bei, imesababisha 'price equillibrium' imepotea kabisa.
Maana yake ni kwamba bei mpya baada ya kodi na tozo, imesababisha wanunuzi kutokuhisi uhalali wa kununua kwa bei mpya. Mfano mdogo tu, mimi nilikuwa namiliki line mbili za simu, ila tangu tarehe moja, ni kama line moja nimeitelekeza na sijafanya muamala wowote wa kutuma wala kutoa pesa kwa wakala, kwasababu, akili yangu inaniambia hii bei ya sasa ni kubwa mno kulinganisha na huduma ninayopata.
Matokeo yake ni nini sasa?
Muitikio ukiwa mdogo kwa walaji, itakuwa ngumu sana kwa Mwigulu kuweza kukusanya kiasi ambacho amakitegemea. Kumbuka serikali ime target zaidi ya Tzs 1.5 Trillioni itoke kwenye miamala ya simu na tozo.
Sasa kwa upepo ulivo, sidhani kama hata nusu ya hii itapatikana. So maana yake, bajeti ya Mwigulu mpaka sasa ina shimo la karibu zaidi ya Tzs 1 Trillioni ambayo ili liweze kujazwa, itabidi serikali ikope, maana kumbuka kuna miradi ya SGR na Bwawa la umeme bado inahitaji pesa.
Ni kama kusema, tayari nakisi ya bejeti yetu tayari ipo kubwa zaidi ya walivoitabiri, kwasababu kuna kodi na tozo hazitaweza kukusanywa kama hii ya miamala ya simu.
Ama kwa kweli Mwigulu amefeli sana, tena sana.. Anasema eti hizi tozo zitatumika kuunda mfuko wa kizalendo, ila ni uwongo kwa sababu huwezi kuwa na mfuko wa kizalendo wakati bajeti yako siku zote ipo kwenye nakisi.
Ni kama kusema eti mtu uweke akiba ya mtoto kwenda shule wakati unadaiwa kodi ya nyumba.. Ni kitu hakiwezekani ni kuwadanganya tu watu, maana ameshabugi.
Kama inawezekana kurudia bajeti, nashauri Mwigulu afanye hivo mapema, la sivo.. naona deni la taifa likiendelea kupaa just kwa mtu kushindwa kufanya kazi yake vema.