Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa bado ni himilivu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Waziri wa fedha na Mipango Mhe.Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa wizara inaendelea kusimamia deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada,

Mhe. Mwigulu ameyasema hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya fedha na Mipango ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo amesema ili kuwa na taarifa sahihi kuhusu udhibiti wa deni la Serikali, wizara imefanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali kwa miaka 20 ijayo, kuanzia 2022/23 hadi 2041/42.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa Matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa, deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

Aidha, Mhe.Dkt. Mwigulu amesema kuwa taarifa inaonesha kuwa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.
 
SBS tuna mtaka firmino sasa,,kwa maana sisi na wabrazili bladii bladii!!
 
Mimi bado niko bandarini, siondoki n'go!.

Majizi yasiyo na huruma yanatuuza, mmetoka Loliondo mnahamia bandarini kote huko mnawapa shemeji zenu.
 
Maadam tumbo lake linajaa na sasa ametakata kwa kipupwe cha kiyoyozi kikali basi deni la Tz kwa sasa ni himilivu.. akija Rais mpya awamu ijayo atabadili maneno kulingana na beats za bwana mpya.. tulikopa sana bila mipango, mnafiki mkubwa!.
 
Mimi bado niko bandarini, siondoki n'go!.

Majizi yasiyo na huruma yanatuuza, mmetoka Loliondo mnahamia bandarini kote huko mnawapa shemeji zenu.
Huko kwenye deni hutaki? Hujui limefika trillion 97
 
Kama deni bado ni himilivu, na sisi watu wa kawaida turuhusiwe tukope mabasi ya Scania au Yutong.
 
Shida sio kukopa shida wakikopa wanakula wenyewe hawatupi hata sent ndio tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom