Serikali inapanga kutumia Tsh. Trilioni 12.10 kulipa Deni la Taifa, Mishahara Tsh. Trilioni 11.77

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Serikali imepanga kulipa kiasi hicho kutoka katika Makusanyo ya Tsh. Trilioni 47.42. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Makusanyo hayo pia yatagharamia Miradi ya Maendeleo Tsh. Trilioni 15.32 na Shughuli nyingine za Serikali Tsh. Trilioni 8.22

Fedha za Maendeleo zitajumuisha Ruzuku mbalimbali za Kisekta ikiwemo Elimu Msingi na Sekondari Bila Ada na Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Pia, italipa Miradi ya Elimu, Afya, Umeme na Maji iliyokamilika

Aidha, Serikali imepanga kutumia kiasi kingine kwaajili ya Gharama za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Bajeti ya Tsh. Trilioni 47.42 ni ongezeko la Tsh. Trilioni 3.04 kutoka Tsh. Trilioni 44.38 ya mwaka 2023/24 ambapo Tsh. Trilioni 6.31 zimeelekezwa katika Deni la Taifa, Tsh. Trilioni 11.89 Utawala, Tsh. Trilioni 5.95 Elimu, Tsh. Trilioni 4.68 Ulinzi na Usalama, Tsh. Trilioni 3.84 Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano na Tsh. Trilioni 3.05 Nishati.

Soma zaidi hapa Waziri Mwigulu: Serikali itakopa Tsh. Trilioni 8.69 kwaajili ya Bajeti ya mwaka 2024/25
 
Mwaka huu wa fedha unaoisha June 30, 2024 ilitengwa bilions ngapi kwa ajili ya kulipa deni la Taifa?
 
kwani Selikali kwenye account yake kuna shilingi ngapi jumla ili niwasaidie mahesabu ?
 
Back
Top Bottom