Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binafsi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binafsi)

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by X-PASTER, Dec 5, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binasfi)

  Leo nitajaribu kuelezea maradhi makubwa yanayo tusumbua wanadamu wengi kwenye nafsi zetu. Binadamu tunaye adui mkubwa kabisa ambaye tunaishi naye, tunatembea naye na tunalala naye na kushauriana naye kila kukicha. Adui huyu si mwingine ila nafsi zetu wenyewe, hii ni nafsi iliyojaa uadui uwovu na majivuno yakiambatana na kiburi na kutafuta kukomoana, pasipo sababu za maana. Hakuna tabia mbaya katika tabia za binadamu na yenye kuchukiwa kama tabia hii**.

  Tabia hizi kama zikimea kwenye nafsi zetu basi uondoa mfungamano wa kirafiki na kindugu na hata majadiliano yetu hukosa busara na hikma kiasi cha kupelekea kwenye utengano na uhasama.

  Mwenye hizi tabia usababisha kufungulia madirisha na milango ya kuchukiwa na watu. Japokuwa kila mtu anatarajia apendwe na aheshimiwe na wengine, ndivyo hivyo hivyo, mtu huyo anategemewa awapende na ahifadhi heshima za wengine pia. Na ajiepushe kabisa na kila jambo linalokwenda kinyume na maingiliano mazuri au yanaosababisha kuharibika kwa maelewano na wengine.

  Naweza kuuhita ugonjwa huu kwa jina la maradhi ya kimaadili yanayompata mtu, maradhi haya ya chuki na uadui ni miongoni mwa maafa makubwa ya ufanisi na utulivu wa nafsi, yanaotokana na tabia mbaya ya hasira ya kushindwa katika medani ya kutafuta maisha au kushindwa kwako katika kile unachokitafuta katika kuboresha maisha yako, kiasi ya kuvuruga mtiririko wa fikra chanya na kupelekea kuvuruga uthabiti wa kiroho wa mtu. Huenda ni kutokana na sababu Fulani fulani za kukosea hapa na pale au kujaribu hiki na kile. Kushindwa uku umfanya muhusika kupata hamaki na kujichukia na kupelekea kuwachukia wale waliofanikiwa kimaisha, kiasi ya kwamba kwa wale wasio na uvumilivu uamua kuwasingizia mambo haya na yale wale wanao waona kuwa ni maadui zao. Kiasi ya kusahau kuwa kufanikiwa au kuto fanikia ni mipango yako tu kutokuwa mizuri au kwa kutaka kutumia njia ambazo si za kimaadili, kama vile wizi au utapeli.

  Hamaki hizi ni ile chuki iliyojengeka muda mrefu kiasi cha kusababisha moto uliofunikwa chini ya majivu ambao unaweza kutoa cheche za chuki na uadui zitakazounguza na kuteketeza mazao ya ufanisi na utulivu wa nafsi yako.

  Bila shaka kutozijali hisia za watu huleta matokeo mabaya ya kudharauliwa na wengine na kuonekana ni mtu duni usiyefaa katika jamii za watu wastaarabu na wasomi.

  Kama vile ambavyo kusamehe kunaonyesha utukufu na umakini wa nafsi ya mtu pia kunaleta usalama na umoja na utulivu wa nafsi, vivyo hivyo, uadui na uhasama kunapelekea kuwa na, chuki ambayo uzaa chanzo cha mfarakano na ugomvi. Ingawa uhasama hufanywa ili kutuliza misukosuko ya ndani ya nafsi, lakini madhara anayopata mtu kwa kulipiza ubaya kwa ubaya huwa ni makubwa zaidi kuliko madhara anayopata kwa njia nyingine, kwani maudhi licha ya kuwa ni shida kuvumilia, mwisho wake uondoka, lakini uhasama unapoota mizizi huchoma moyo wa mtu kama miba ya sumu na humkera daima. Isitoshe, uadui hauwezi kuondoa ubaya. Bali hulipanua na kulichimba zaidi donda. Kwa kawaida, uhasama humfanya hasimu ajitetee zaidi na alipize kisasi zaidi, akitegemea kupata utulivu wa nafsi, kumbe ndio anajirimbikizia machungu ambayo umletea maradhi ya saratani ya akili na kupelekea kuwa na maamuzi yasiofaa na yaliojaa visasi na chuki.

  Wakati mwingine matokeo ya uadui huwa machungu mno kwa kadiri kwamba huwa hayumkiniki kurekebisha uharibifu unaotokana nao. Huenda mtu katika umri wake wote akaungua moyoni mwake na akaitesa roho yake kutokana na kosa kubwa alilofanya la kuweka chuki. Kutotumia akili na kutofikiria matokeo mabaya ya kufanya ugomvi, akifikiria kwamba anamkomoa mtu kumbe anajikomoa mwenyewe. Maana kila binadamu ana kamusi ya maisha yake na kuna baadhi ya watu, hawana maneno kama vile 'samehe au upendo' kabisa, bali kuna maneno kama vile 'uadui, ugomvi, nitamkomoa, atajuta katika maisha, ataipatapata fresh' na mishabaha na minyambuliko yake ndiyo iliyojaa humo. Kinyongo na hasira kali hutumia nguvu zote katika kulipiza kisasi na kujenga chuki kati ya watu. Tabia ya kupandwa na hasira haraka huandalia uwanja wa chuki. Mtu mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kuhamaki havumilii kusikia akikosolewa au akichambuliwa hata kidogo. Kinyume chake, watu wenye nyoyo safi na madhubuti huchukulia kukosolewa na kuchambuliwa kwao kuwa ni fursa nzuri ya kujirekebisha.

  Watu wengi wanashindwa kuelewa kwamba kushikwa na hasira sana ni dalili ya kutopevuka kiakili, kwani huenda mtu anayekosoa huwa hana nia ya kumtukana au kumdharau mwenzake mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kukasirika. Hata kama kitendo hicho kitaonekana ni cha kutukana na kudharau, lakini huenda hakukusudia hivyo. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuudhika na kulalamika.

  Uchambuzi uliokusudiwa kuudhi na kudharau, kama una ukweli na unaonyesha kosa lenyewe, basi huwa ni zinduo na funzo kwa mwenye akili badala ya kuwa chukio. Lakini uchambuzi usiokuwa na msingi na ukweli usitiwe maanani, kwani unatokana na husuda na ubaya. Kitendo cha kuchambua bila ya msingi wowote ni kitendo cha kitoto, kichuki na kiwivu chenye lengo la kujitukuza kwa kuwadharau wengine. Hata hivyo, tusikereke na watu kama hao, bali tuwafunike kwa shuka ya amani na upendo.

  Moyo wa kuweka kisasi na kukomoana ni dalili ya unyonge wa nafsi. Na ni ishara ya maudhi na maonevu aliyoyapata mtu udogoni mwake aidha shuleni, mtaani kwake alipokuwa akiishi au aliyo yaona katika familia au wazazi wake. Mambo haya huweka athari mbaya na kinyongo katika moyo wake kwa kadiri kwamba nafsi yake husumbuliwa na aina moja ya chuki iliyotia fora. Kwa ufupi, kukomoana na kulipiza kisasi ni njia mojawapo wanayoitumia wenye kujihisi duni ili kufidia kushindwa kwao. Hutumia visingizio mbalimbali kuwakera wengine na utenda uhalifu wa hatari kulipiza kisasi kwa yale yaliomsibu alipokuwa mdogo, akitafuta kujifariji ukubwani kwa masahibu ya utotoni. Watu wa aina hii mara nyingi wanakuwa wamelelewa katika koo duni na wakapata vyeo au kusafiri nchi za mbali na kujiona kuwa wao ni bora, hivyo kupelekea kuwa wajeuri. Kwa njia hii hutaka kufidia uduni waliolelewa nao katika koo hizo. Na ujiona ni watu bora kuliko wengine, na hutaka kutumia uhasidi na ubinafsi wao kujitangazia ubora wao. Wengi wetu tunaweza kuwatambua watu wa aina hii miongoni mwetu.

  Njia mojawapo ya kuishi kwa amani ni kuwa na utulivu wa moyo na kusahau mabaya ya watu uku ukuzingatia shabaha ya maisha kwa kujaribu au kujitahidi kuishi kwa roho safi na huyapuuza mabaya na upinzani wa kiadui anaokutana nao mtu.

  Kila binadamu ana hiari ya kudhibiti taathira ya ubaya katika roho yake, vile vile anao uwezo wa kubadilisha jambo baya kuwa zuri au fikra mbaya kwa fikra nzuri na kujibu ubaya kwa uzuri. Kwa hivyo, tunaweza kupunguza nguvu za taathira mbalimbali juu ya fikra zetu kwa kutegemea nguvu za matakwa yetu, na kwa njia hiyo tukapata nguvu za kutosha kuweza kuvunja hisia ya chuki ambayo huzisumbua roho zetu. Hakuna mtu atakayeweza kutusaidia tutakapo shindwa kutekeleza wajibu wetu zaidi ya mtu binafsi mwenyewe.

  Kukomoana na kuzushiana mambo yasio mazuri, kama vile vifo au uhalifu ni mambo ambayo si katika ubinadamu, watu wa namna hii ujificha katika ngozi tofauti tofauti. Baadhi ya watu huvaa ngozi za urafiki au uswahiba au kujionesha kuwa ni mpenda dini na haswa hizi zama za utumiaji wa mitandao, watu uweza kukuomba urafiki na kuwaongeza kwenye orodha ya watu utakaokuwa ukiwasiliana nao au wengine ujitia kwenye siasa na kujifanya kuwa wao ni wapinzani, kumbe ni wanafiki na kuchukuwa siri za wengine kisha kuwachongea na kwa njia hii wanaweza kuwakomoa au kuwaangamiza wengine kisiasa au kiuchumi na katika jamii kuonekana kama ni wasaliti.

  Niliwahi kusoma sehemu zamani kuwa:

  “Chuki na uadui ni matokeo ya upumbavu hasa panapokosekana sababu maalumu. Tunaweza kuyatatua mambo mengi kwa urafiki, lakini ubinafsi hautuachii. Hutokea mara nyingine tukavunja urafiki kwa sababu ya adha ndogo kabisa, wakati tunaelewa kwamba kosa lao ni kuwa na imani tofauti na yetu au wakati mwingie wanaunga mkono fikra tofauti na sisi. Kwa kweli, tunashindwa vipi kuvumiliana katika mustakabari wa maisha yetu na hali sote tuna haki ya kuamini na kufuata fikra tunazo amini kuwa zitatukomboa kimaisha...!?”

  Watu hawa wapo tayari kupoteza muda na wakati wao na nguvu zao katika kujitengenezea maadui, uku wakijikomba kwa watu (matajiri, watawala au wanasiasa) wanao amini kuwa wanaweza kuwasaidia katika kutatua maisha yao waliyo yaharibu kwa uhalifu wao. Hali hii uendelea mpaka pale hasidi huyu atakapo fanikiwa, ingawa ni mara chache sana kufanikiwa, lakini hata atakapo fanikiwa hakumpi utulivu wowote wa nafsi na matokeo yake umpelekea kutafuta adui mwingine na mwingine mpaka kumpelekea kupata maradhi mabaya ya nafsi na kuanguka kwa aibu.

  Wengi wetu tunashindwa kuelewa kuwa mapenzi ya kijamii ni sababu muhimu kabisa ya mtu kupata maendeleo na mafanikio mazuri katika maisha yake. Mtu mwenye mapenzi na watu akaishi kwa wema na upendo kiasi ndio zikawa sifa zake, basi mtu huyu anayeweza kutawala hata nyoyo za watu na kupanda ngazi ya maendeleo kwa kunufaika kwa msaada na ushirikiano wa jamii na kupata ufunguo wa mafanikio. Mtu mzuri kwa tabia na amali ni kama taa inayong'aa yenye kuongoza fikra na maendeleo ya jamii. Usafi wake wa moyo una taathira kubwa katika muundo wa maadili ya watu.

  Kwa kuwa kijicho kina sura mbaya, hivyo hujitangaza chenyewe kuwa ni adui wa tabia na sifa nzuri na kizuizi kati ya watu. Kijicho hakimpi mtu fursa ya kupendwa na watu anao ingiliana nao. Hivyo, mwenye kijicho hukosa fursa za ushirikiano na neema ya mapenzi. Hasidi huonyesha waziwazi ubaya wake unaotokana na vitendo vya tabia yake mbaya, na kwa sababu hiyo hulaaniwa na huchukiwa sana na watu. Na kupelekea kupata huzuni ambazo huingia moyoni mwake kutokana na uhasidi wake, kiasi huikandamiza roho yake katika moto mkali na kuteketeza maisha yake.

  Siku zote moyo wa mwenye wivu, husda na roho mbaya, daima uona uchungu na uwa hauna raha wakati wowote. Kwa sababu anaishi kinyume na imani yake, kwa sababu ya kuikataa neema za Mwenyezi Mungu hambazo hazina kikomo, hivyo uishi kwa mashaka na wasiwasi kwa sababu hiyo zile kutu za huzuni huwa haziwezi kutoka kabisa katika moyo wake mpaka anaingia kaburini.

  Hali hii ya uhasidi ikishamiri katika jamii, basi upelekea migogoro na ugomvi wa kila aina. Mazingira kama hayo yanayochafuliwa na ugonjwa wa chuki na roho mbaya ya uhasidi huwa ni kizuizi mbele ya maendeleo si ya mtu mmoja mmoja tu, bali jamii kwa ujumla, hivyo kuvuruga nidhamu ambayo ni kiini cha maendeleo ya watu na kusababisha maanagamizi ya jamii hiyo akiwemo hasidi mwenyewe.

  Kila mtu au binadamu ana haki ya kuheshimiwa katika jamii kwa kadiri ya heshima na hadhi yake. Mtu anayejifunga katika kuta nne za majivuno na nafsi yake ikatawaliwa na chuki, hatajali kamwe kuwaaribia wengine isipokuwa atazingatia matakwa yake tu. Kwa hivyo, atajaribu kwa nguvu zote kuwaudhi na kuwakera wengine na kujifanya mashuhuri na msifiwa, na kuilazimisha jamii imuone yeye ni bora.

  Dhana mbaya ni athari isiyozuilika katika nafsi ya hasidi. Miali ya moto ya mwenye dhana mbaya ya kujiona daima huwaka na huwadhania wote kuwa ni wenye kumchukia na kumtakia mabaya.

  Kudharauliwa kwake na kupata mapigo ya daima kutokana na maringo yake hakumsahaulishi kamwe ubaya wake. Bali uendelea kutafuta mbinu hizi na zile kiasi ya kwamba kichwa chake husumbuliwa na fikra zake bila ya mwenyewe kutaka. Na kila akipata fursa hutaka kuifanyia chuki jamii, na uwa hawezi kuona raha madhali machafuko na machemko ya ndani mwake hayajatulia.
  Kirusi cha majivuno na maringo hutokeza katika dhamiri ya mtu baada ya kuugua maradhi ya kinafsi ya kujihisi duni. Maradhi hayo hugeuka kuwa kirusi duni ambacho kwa sababu ya kuwa kiharibifu na chauma, huenda kikawa ni chanzo cha hatari nyingi na uhalifu wa kila aina. Kirusi hiki duni humfanya mwenye kujinata afanye ukatili na udhalimu.

  Mtu mwenye thamani na hadhi ya kweli hatakuwa na haja ya kujivuna au kujionyesha mbele ya watu wakati wowote ule, kwa sababu anaelewa vyema kwamba kujiona si msingi wa ubora, na roho mbaya haimfai mtu yeyote wala haimfikishi mtu yeyote kwenye kilele cha utukufu na ufakhari.

  Basi nadiriki kusema kwamba, kumdharau mtu mpumbavu na kujiepusha na marumbano yasio na tija ni fimbo tosha kabisa, kwa sababu ukiingia wenye marumbano na mtu mpumbavu atakushusha hadi ufikie upeo wake wa kufikiri kijinga na kipumbavu, na kisha atataka kukugaragaza kwa upumbavu wake, na kwa sababu hana hoja, mwishoni utashindwa kuendelea naye... Lakini ukiingia kwenye marumbano ya hoja dhidi ya wasomi, ukiwashinda au wakikushinda basi utafaidika kwa elimu yao, kwa sababu wana upeo unao lingana na wewe, na hapo lazima utaondoka na faida japo mbili au tatu.

  Siri moja kubwa sana ya kumuumiza mtu mpumbavu kisaikolojia ni kumdharau na kumfanya kama hayupo, yeye mwenyewe ndio atakuwa akiangaika, maana hajui umeuchukuliaje upumbavu wake.

  Kila mtu ana mwendo wake maalumu unaotokana na hali yake ya kimaadili na kinafsi. Msamaha ni mojawapo kati ya sura angavu kabisa ya utukufu na udhibiti wa nafsi, na ni aina moja ya ushujaa na uungwana. Mwenye kuwa na sifa hiyo kwa kadiri ya kutosha na mbali ya kuwa na nguvu na uwezo wa kulipiza lakini akasamehe, hufaidika kwa kuwa na uhakika na usafi wa moyo ambao hauwezi kulinganishwa na kitu chochote kingine. Kusamehe kunaitukuza na kuiimarisha roho ya mtu, na ni kipawa ambacho kwacho hububujika upole na wema. Kusamehe humtoa mtu kwenye kifungo cha ubinafsi. Ingawa ni shida sana kusahau madhara na mabaya ya wengine na moyo huumia sana mwanzoni, lakini kwa kadiri mtu atakavyovumilia katika njia hiyo ndivyo atakavyoweza kupunguza sana masumbufu yake ya rohoni na mwisho wake akawa ni mtu msamehevu na aliye bora kabisa katika jamii.

  Hapana shaka kwamba kusamehe kunaweka athari nzuri katika moyo wa adui kwa kadiri kwamba uweza kuleta mabadiliko katika fikra na mwendo wake. Chuki nyingi zimeondoshwa kwa kusamehe, na uadui mkali na wa kizamani umeondoshwa na mahali pake kukaa usafi wa moyo na upendo. Adui mchokozi hulainika na husalimu amri mbele ya mtu aliyejizatiti kwa silaha hii kali na kwa fikra za kiungwana.

  Jambo la kuzingatia:
  “
  Kimojawapo kati ya vipawa vikubwa kabisa vya binadamu ambavyo wanyama wengine hawakufaidika navyo ni hisia ya kusamehe makosa ya wengine. Mtu anayekuudhi huwa kwa wakati huohuo hukupa fursa nzuri ya kumsamehe na kuona utamu wake. Tumefunzwa kuwasamehe maadui zetu lakini hatukuambiwa tusiwasamehe marafiki zetu. Hivyo, ni wazi kwamba ni lazima tusahau mabaya tuliyotendewa na wengine. Unapomlipizia kisasi adui wako huwa ni sawa naye, lakini unapomsamehe wewe huwa ni bora kuliko yeye, kwani yeye huwa ni mwovu, nawe huwa ni msamehevu. Huenda tusifanikiwe tunapotaka kulipiza kisasi, lakini kusamehe ni njia bora kabisa ya kulipiza kisasi. Kwa kusamehe tunaweza kuwashinda maadui zetu bila ya kupigana na kuwafanya wainamishe vichwa vyao mbele ya utukufu wetu. Kwa hivyo, kuacha chuki na kukwepa uadui ni shambulio kubwa kabisa lenye kuwashinda mahasimu wetu. Tunapotendewa maovu, tuwatendee mema, kwani kulipa mema kwa mabaya uliyofanyiwa ni siasa ambayo kwayo hupatikana amani duniani
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  X Paster! Shukrani kwa mada yenye umuhimu mkubwa!
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Chuki ni kama sumaku ...swali huwa inavuta na kushikilia nini?
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  shukurani Mkuu,nitaenda kuipitia vizuri kwenye cafe kesho M/mungu akipenda. Nalog off
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  "Mstahamilivu hula mbivu"
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Ni maneno yaliyojaa hekima na busara kwa mwenye kutafakari.

  Ahsante kwa kutupa darsa iliyonyooka.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  hakika hoja imejaa hekima na utukufu maanake kama binadamu tungeweza kutafsiri nafsi zetu kwa moto basi wengi tungeisha waka moto na kuwa jivu kutokana na chuki, Uhasidi na Uadui lakini ndio katika mitihani alotupa Mwenyezi mungu kuweza kuzikarifisha nafsi zetu dhidi ya hayo mambo makubwa...

  Mara nyingi mimi husema kutokua na imani ndiko haswa sababu kubwa ya Chuki, Uhasidi na Uadui maana dunia hii tofauti baina ya binadamu na mnyama inazidi kuppungua maana wengi tumeshindwa kutumia tunu tulotunukiwa yaani - AKILI ktk kuzikosha nyoyo zetu..

  Inshaallah, Kwa rehma zake Mwenyezi Mungu tutafika..Darsa kama hili tunalihitaji sana.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,492
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Mkuu X-Paster, ujumbe umetulia na labda utasaidia sana katika kuleta mabadiliko hapa jamvini.

  Usiku mwema Mkuu na salaam kwa familia yako.
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mkuu asante kwa Elimu nzuri, nitarudi kumalizia kuisoma..
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Asante Saana X-Paster kwa Ujumbe wa Msingi na pia Naomba niongezee haya...


  Kila mwanadamu ana kila tabia... iwe ni Chuki, Wivu, Uchoyo, Ubinafsi, Upendo n.k.... Kitutofautishacho kati ya mmoja na mwingine ni ile utofauti wa tabia ipi hasa imeshika hatamu kati ya tabia hizi nyingi ndani ya mwanadamu husika... Kiasi kwamba hio tabia yaweza tumika kumulelezea/muelewa am kumfafanua mtu kwamba yu/sio Mpole, Mkali, Mkarimu, Wa Chuki, Dharau na tabia nyingene kede kede.... Mara nyiiingi hizi tabia ni matokeo ya kuzaliwa nazo ingawa pia huchangiwa na malezi, makazi, mazingiira na the whole life circulated circumstances of a person. Hizi tabia huchangia saana msumkumo wa mtu/mhusika kufanya mambo mbali mbali - iwe mazuri ama mabaya (ingawa hutegemea saana toka jamii husika). IKUMBUKWE kua hakuna mwanadamu huchagua tabia ipi itawale ndani yake.... Yaani iwe na nguvu kiasi kwamba akawa Kero kwa wenzie/kwa wachache ama kwa Jamii kwa Ujumla! KIKUBWA na KIZURI ni kua Kila mwanadamu with Determination and Focus ana nafasi na nguvu ya Kujirekebisha tabia hio ilomtawala hasa kama ni Kero na mbaya kwa wengine. Hizi tabia zaweza rekebishwa kwa kupita hatua tatu (3) za muhimu.


  1]. Kupata ujumbe na kuufanyia kazi kwa kutambua kua ujumbe wakuhusu.

  2]. Kutambua kua wewe ni mmoja wa Walengwa wa huo ujumbe muhimu.

  3]. Kukubali kua kweli yatakia urekebike ile kupelekea kuweza badilika na kua mwanadamu bora zaidi katika jamii yako popote pale.  NI MUHIMU KUA:-

  Kama Mwenyezi Mungu kakujaalia Utafakari, Ujuvi, Busara na Simile; ni MUHIMU saana kuvitumia hivo vipaji ka ufasaha na mara zoote hasa inapohusu mwanadamu mwingine kukukwaza. Ni rahisi kama una vipaji hivo kuhimili kama mhusika nia Mhanga wa tabia yoyote hata CHUKI (Iwe mhusika kagubikwa na Chuki AMA Kapambana na alogubikwa na Chuki); NDIO.... Sio kazi rahisi; na Ndio maana ni moja ya mitihani ambayo kama waweza shinda hasa mara kwa mara - yampelekea muhusika kuelekea katika safari ya UTU UZIMA ULOJAA BUSARA. Faida ambayo haiwi kwa mhusika tu! Bali kwake, walomzunguka na jamii kwa Ujumla.


  NI MUHIMU KUZINGATIA:-

  Kama mwanadamu yeyote kagundua/kajua kua ni Chanzo cha Chuki dhidi ya Mwanadamu Mwenzie.... Asikimbilie kumchukia na kumlaumu Mhusika..... Ni vizuri Mhusika (alochukiwa) Amsome/Muelewe/Mtafakari huyo Mwenye Chuki dhidi yake ili walau kuelewa nini hasa tatizo... Nini hasa Chanzo... Nini hasa Chamsibu huyo alojaa Chuki juu yake na si kwa Wengine bali kwa wewe. Matokeo siku ya Mwisho yaweza kushangaza... Waweza kuta sa ingine wewe ndo wa Kulaumiwa yule Mwenzio KACHUKIA... Ni ngumu Kumeza lakini saa ingine Ukweli ndo huo.

  La Msingi la kutambua ni kua Chuki HAILIPWI kwa Chuki.... Hio hufanya mwnye Chuki na Alolengwa na hio Chuki wooote wawe sawa. (Between them their is NO Better Person when that HATE is Reciprocated). Mmoja ya wanafalsafa (Mahatma Ghandhi) walojawa na Busara za hali ya Juu katika Nyanja mbali mbali za maisha alishawahi sema/andika.... (tafsiri "Popote pale unapokua Umeandamwa na Adui - Silaha pekee ya kummaliza ni Mapenzi juu yake" Ina maaana nzito saaana hii Quote na Naipenda saana.


  X-Paster Ujumbe Ulotoa hapa ni mzito na wa hali ya Juu saana. Na nashukuru na kufurahi kua ni mmoja wa walobahatika kuupitia. Na natumai kua ni weengi wataupitia na kuufanyia Kazi. Asante.

  Pamoja Saana

  AshaDii.
   
 11. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Always remember others may hate you but those who hate you don't win unless you hate them. And then you destroy yourself
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... Chuki halipwi kwa chuki ... fantastic fact Indeed!

  ... Ni kweli kuwa chuki hailipwi kwa Chuki kwani chuki ni sumaku ... Inavuta nini? ... Hadi isifae kutumika kulipizia kisasi?

  ... Kwa kuwa Chuki ni sumaku haifai Kutumika kwa matumizi ya mwanadamu ndio maana ... Tutumieni mapenzi ya Juu kabisa vinginevyo ... itakuwa Mhh!! , Naheshimu sana msemo huo wa Mahatma Ghandhi, I wish nigeweza kuufanyia kazi 100%!!

  Sijaweza kuutekeleza kama inavyotakiwa.. Tatizo?.. Nitayapata wapi mapenzi (LOVE) ya kutosha kushindia chuki!
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... Hivi ingekuwa ni kweli kuwa ...Chochote unachokichukia kwa MOYO na Dhati .... Kinakurukia na kung'ang'ania Moyoni na kukufuata popote unapokwenda.. ni nani angenfaya kosa la kijinga kama hilo na Kutumia moyo wake kubebea matatizo!!?

  ... Hakika usinge mchukia mtu anaye kuchukia au kukuchikiza kwani ni kweli utakuwa umembeba Moyoni! Hata ukiwa mbali naye ki mwili lakini moyoni kwa kuwa umembeba ...Atakuwa anakusumbua kikamilifu kama vile yuko hapo ulipo ... anaweza akawa anajirudia rudia kwenye fikra zako hata kuwa unaona taswira yake inayoghazi na ilyobeba kero ..nk!

  ... Kiukweli atakusumbua sana ..ingawa ... kimwili hayuko hapo ..lakini MOYONI yupo!! Na ukweli ni kuwa Utaipata fresh ... !! utakosa hata usingizi, utapata msongo wa mawazo kumhusu nk ... KOSA ...?
   
 14. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Niogezee japo kidogo kuwa, darasa kama hili tunalihijati sana hapo Jf na zaidi kwa viongozi wetu wa kiserakali hasa pale mjengoni kila Bunge jipya linapo zinduliwa!! Nafikiri Mtizamo wa Kitaifa na Kizalendo ungukuwa JUU!!
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  tupo pamoja ni vizuri kujitambua.
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni kweli maneno yako, si unajuwa kuwa hasidi hana sababu?
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nashukuru mkuu wangu kwa kunisoma, tupo pamoja na tutakuwa pamoja Insha'Allah

  Kaka, Tuwone ndugu yangu...! Mkuu, ni wachache sana wenye kutaka kuzibadiri nyoyo zao kuelekea kwenye mazuri, na yote hayo ni katika kutaka kuonyesha kuwa wao ndio wao, upper class, kumbe wanajiangamiza.

  Mkuu, matumaini yangu utakuwa umerejea tena na umepata japo moja, mbili, tatu... Mchango wako unahitajika mkuu.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Haya uliyoyaweka hapa ni muhimu sana kwa mwenye kuzingatia... Tupo pamoja dadaa AshaDii.
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  @ X-paster NIce article
  Kwenye hili jamvi kuna aritcles zako nzuri huwa zinanifanya nimkumbe yule jamaa wa Jitambue( nimemsahau jina) Nilikuwa sikosi gazeti lake na kipindi chake TVT.

  Ukiwezekana tunga kitabu maana hivi sasa watu watu tunajua maisha ya artificial. Hata watoto walioko mashuleni wanafundishwaa hesabu, na eglish na physics mpaka wanajua kutumia facebook lakini kuna kitu kinakosekana . Na kinachokosena ni elimu kama hizi.

  Ndio maana sikubalini na mkandara aliyesema inayosababisha chuki ni watu kutokuwa na IMANI. No kwa sababu kwa experince yangu na humu JF watu wenye imani za dini ) Sisi ndio hasa wenye chuki. KInachosababisha ni watu kukosa elimu na msingi wa maisha halisi. Tena wengine hizo imani etu tulizonazo ndio tunazitumia vibaya kuwa msingi wa zege wa chuki. kwa wengine wasio na imani kama zetu.

  Kuna watu wakiomuona Kikwte kavaaa kanzu pale ikulu wanakosa raha kabisa. Hivyo Hivyo kuna wengine.. ....ngoja niihsie hapa

  X-paster UShauri
  Social-studies ni somo linalokoseana kwenye jamii na shule . Ungekuwa na muda mkuu ungefanya mambo uwasiliane na wandeshaji wa elimu uone watakusaiia vipi hizi makala zako au vijarida viwepo kwenye shule Al- levele hata vyuo.

  Makala au vijarida kama hivi zinaweza kuokoa maisha ya watoto wawili kwa mwaka wanaokunywa sumu na kujiua mashuleni na vyuoni sabbau ya chuki au kuchukiwa.
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Aliyekuwa Mmiliki wa Gazeti la JITAMBUE ni Munga Tehanan RIP!
   
Loading...