Mimi nadhani ukiwa katika speed ya kawaida 80Km/h tairi za mbele zikipasuka hakutakua na athari kubwa sana. Ila huyu jamaa inavyosadikika alikua kwenye speed kubwa sana. Pia hatuwezi kulinganisha kesi ya ufisadi na utoaji wa roho za watu, uizi na ubadilifu wa mali ya uma ni ufisadi ambapo vyote vinaweza kutafutwa ila roho ya mtu ikishapotea utaitafuta wapi?
Madereva wanagoma kwani wengi wanatabia ya kuendesha kwa kasi na kutozingatia sheria za barabarani, wanaogopa wasikumbwe na mkasa wa mvua ya miaka. Mini naendeshaga mwenyewe kutoka Dar hadi Moshi. Lakini huko njiani kuna ukiukwaji sana wa sheria za barabarani. Utakuta mtu ana overtake kwenye kona, pasiporuhusiwa, wanapaki ovyo hasa malori, speed kali sana, penye speed 50km/h anaendesha mia
Mimi nadhani adhabu hii itakua fundisho kwa madereva wazembe na ninaiomba mahakama zetu hapa nchini zisicheleweshe kesi za namna hii. Mtu akiua halaiki ya watu namna hii haina tofauti sana na wanaojitolea mhana uko mashariki ya kati au mauajia ya jimbari, Darful n.k
Ungekua wewe ni mfiwa mmojawapo usingemtetea dereva hata kidogo. Umesababisha ajali kwa speed kali na kutofuata sheria za usalama barabarani then sheria ichukue mkondo wake.
Ila mimi nashangaa kwa nini mmiliki wa basi lile hajatiwa hatiani kwa makosa ya watendaji wake. Kifungu ni Skendo la Richmond amabapo Luwasa aliwajibishwa kutokana na Utendaji mbovu wa watendaji wake. Pia Mwinyi alijiuzuli akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na utendaji wa askari wake.
Nawasilisha hoja