Mamlaka: Madereva wa Mabasi ya Mikoani 'Wanaobeti' Kufika haraka waendako Kukiona cha Mtema Kuni

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Kwa hili GENTAMYCINE nasema mmechelewa sana hata hivyo nawapongezeni kwa Kuliona na kuamua kulivalia Njuga hivi sasa kwani kuna Watu wamepoteza Maisha na wengine kupata Ulemavu wa Kudumu kutokana na Upuuzi wa baadhi ya hawa Madereva wa Mabasi ya Mikoani.

Yako Mabasi mengi yenye huu Upuuzi ila kwa kuanzia nawaombeni muanze na haya Mabasi ya Waandamizi wa CCM na Serikali ambapo Mmoja ni 'Bidashi' Mstaafu Jumba la Maamuzi Dodoma na mwingine hivi sasa ndiyo anaamua Watanzania tushike Pesa au tuzikose kisha tuanze Kununiana Krismasi hii na mwaka mpya ujao.

Nina Dereva Mmoja wa Kampuni fulani ya Basi ( nalihifadhi kwa sasa ) ila Mabasi ya Kampuni hiyo yameshaua ( yameshachinja ) mno Watu aliniambia kuwa Yeye 'interview' pekee aliyofanyiwa ni Kuulizwa tu Uzoefu wake na aliposema kuwa Safari ya Umbali wa Masaa 10 Yeye anatumia Masaa 6 hadi 7 pale pale 'Secretary' akaambiwa ampe Funguo na aanze Kazi rasmi huku Bosi akiwa ni mwenye Furaha kwa hiyo CV 'hatarishi' ya Dereva huyo.

Kuna Siku Rafiki yangu Mmoja alipanda Basi ambalo Dereva alikuwa Yeye na anachokumbuka tu ni kwamba huko njiani walifyeka ( waliua ) Ng'ombe 4, Mbuzi 3 na kuna Dereva Bodaboda Mmoja walimkosakosa njiani kwa Kujipendekeza Kwake barabarani huku Abiria wote ndani ya hilo Basi wakijilazimisha 'Kusinzia' ili wasiwe wanaona yanayoendelea nje huku wale waliokukosa Usingizi huo muda mwingi wakiutumia Kumtaja Mwenyezi Mungu / Allah kwa Sura zao za Huruma.

Wachukulieni tu Hatua Kali sana hawa!!!

Taarifa kuhusiana na Tamko hili la Mamlaka inapatikana katika Mtandao wa EastAfricaTelevision.
 
Mmoja anayebet ni dereva Mwarabu mwembamba wa Caprikoni ya Arusha Mbeya. Si kwa kukimbiza vile kwenye kona na milima ya Babati.
 
Back
Top Bottom