Madereva wa mikoani wasitisha mgomo wao!

Madereva wa mikoani wasitisha mgomo wao!

Kuna utaratibu wa sheria si kuwaadhibu wananchi, naungana na woote wanaosema waende mahakamani wakakate rufaa. Na wananchi nao wakiyagomea mabasi itakuwaje? Hao madereva wengi saana ni jeuri hawawasikilizi abiria hata kidogo, ukishakata tiketi ni balaa mpaka mwisho. Ndani lugha mbaya, mengine ndio yanajaza hata namna ya kupita hakuna, wengine wanaweka mizigo ndani ya bus. Km Najimunisa. Mie nadhani ipo haja ya kuwashughulikia zaidi ila si wa mabasi tu bali iwe madereva woote kuanzia bajaji
 
JK alisema atakula nao na amesha anza sasa .Kuna shida hapa .Miaka 30 kwa ajali ya gari si sahihi.Dereva wa Mwakyembe hivi kesha fungwa ?
Yule wa Chacha Wangwe kafungwa miaka mingapi ?Hukumu hii ina siasa ndani yake na uchaguzi huu kuna matatizo makubwa sana .
 
Hapo wanataka kushindana na sheria ambayo ndo imeamua kuwa mwenzao ana makosa. Sheria lazima ziheshimiwe na wanatakiwa waichukulie hiyo adhabu kama fundisho kwao yasije yakawakuta pia. Labda kama jamaa hakutendewa haki.
 
suala hapa ni jinsi gani hakimu atakuwa linient lakini hukumu inatoa range ya miaka sasa huenda hakimu kaamua kutokuwa linient.
 
....Naona mabasi yameanza safari zao tena.....huenda kuna makubaliano fulani yamefanyika.sasa swali ni je; makubaliano hayo ni ya Kisheria au kiutendaji tu??
 
Adhabu kali kwa makosa ya aina hii hatujawahi kuziona huko nyuma. Ila baada ya tamko la Raisi kuhusu madereva sasa mahakama ina act fast na kwa ukali wa ajabu.
Hivi kumbe hukumu zozote za mahakama mpaka Rais atoe tamko? Ndio kusema hata kesi hivi za mafisadi ambao wameua watanzania wengi taratibu kwa miaka mingi hazitafanyiwa hivi mpaka Mhe. JK atoe tamko? (kama akipenda)
 
Mafisadi wanaua wengi kwa mwendo wa taratibu, Madereva wanaua na kujeruhi wengi kwa mwendo wa spidi kali....

Kutetea maderava wahuni na wauaji waliojaa katika barabara zetu ni sawa tu na kuwatetea mafisadi wahuni na hatari waliojaa miongoni mwetu ambao wengine tunakunywa, kucheza, kusali, kuomboleza na hata kulala nao....

omarilyas
Ni kweli wote hao hawafai kutetewa...lakini kinachojitokeza hapo ni udhaifu wa kushughulikia matatizo kwa uzingativu wa sheria na haki. Hatujasahau mamia ya watu waliofariki dunia katika ajali ya MV Bukoba ambayo hukumu yake licha ya kusababisha msiba wa kitaifa, na mahakama kubaini uzembe wa wazi...watuhumiwa wapata adhabu nyepesiiii....kulikoni ajali hii
 
Ni kweli wote hao hawafai kutetewa...lakini kinachojitokeza hapo ni udhaifu wa kushughulikia matatizo kwa uzingativu wa sheria na haki. Hatujasahau mamia ya watu waliofariki dunia katika ajali ya MV Bukoba ambayo hukumu yake licha ya kusababisha msiba wa kitaifa, na mahakama kubaini uzembe wa wazi...watuhumiwa wapata adhabu nyepesiiii....kulikoni ajali hii


Jamani nimesema hapo juu, sheria iko wazi na inatoa range ya miaka ambayo mkosaji akisha bainika kutenda kosa anaweza kuhukumiwa. Kinacho leta tofauti ni linience ya hakimu, na ktk hili sheria inamruhusu, sasa kinachoonekana ktk kesi ya huyu dereva ni kwamba labda kwa uoga hakimu kachukua maximum purnishment, na hakutaka kuwa linient.

Kutatua hili inabidi waziri wa sheria na katiba awasilishe mswada wa sheria ili adhabu isimpe mwanya hakimu wa kuwa na alternatives. Pindi mtu akiwa convicted basi hukumu iwe ni moja.
 
Naomba hapa JF kuwe na mjadala huru ili tujue nini maana ya over speeding,naamini gari imeundwa kwa kuzingatia tafiti mabalimbali muhimu ili kuhakikisha zinaundwa na kuwekewa kiwango cha mwendo kasi ambacho hakitakiwi kusababisha ajari kama mazingira tarajiwa ya gari yatakuwepo,si kweli kwamba basi likiendeshwa kwa speed ya 120km/hr litapata ajali,ajali yaweza kutokea hata kama unaendesha kwa speed 60kms/hrs,lilio la muhimu inabidi tuangalie mazingira ya ajari kwa ukumla wake tukianzia na barabara na alama husika,ubora wa magari yenyewe na uwezo wa madereva.
Uzembe ni chanzo kikubwa cha ajali,wala kuendesha kwa speed kubwa hakuna uhusiano na uzembe,ni muhimu basi ajali inapotokea tuchunguze ni aina gani ya uzembe uliosabaisha ajali badala ya kukimbilia kuhukumu speed ya dereva. Huwezi ukaendesha gari Dar-Songea kwa 80kms/hr.labda kama abiria watakuwa na mkataba wa kudumu nawe,safari ni ndefu sana inafupishwa na speed inayotumiwa na madereva ambayo ndcho kivutio kwa abiria walio wengi.
Umakini wa madereva,wamiliki na mamlaka zinazohusika na miundo mbinu utaopunguza au kuoandoa ajali na si speed ya magari,speed itapunguza maafa lakini si kuondoa ajali

Nakuunga mkono na mguu! wanapogongana watembea kwa miguu na kung'oana meno sina hakika wanakua kwenye spidi gani!

Hakuna dereva anayekusudia kuua abiria wake wala kujizuru mwenyewe. Huko njiani kuna mambo mengi ubovu wa barabara, spea feki, ujuzi wa binadamu (mizizioloji) na mambo kedekede. Muulizeni mzee wa mistari kutoka kusini nini maana ya ajali!

Kwa dereva au mwenye kutarajia kudraivu asishabikie hukumu yeyote kwa dereva
 
Hao madereva hawatumii comon sense..wanawasababishia hasara maboss wao.Wanafikiri wapo peke yao wenye uzoefu wa kuendesha magari?
Kama kuna uwezekano wenye ma-bus wawaajiri watu wengine kwa sababu hawapo peke yao,i think hii inaweza ikasaidia..Na kama wataleta fujo sheria ichukue mkondo wake.
 
Hao madereva hawatumii comon sense..wanawasababishia hasara maboss wao.Wanafikiri wapo peke yao wenye uzoefu wa kuendesha magari?
Kama kuna uwezekano wenye ma-bus wawaajiri watu wengine kwa sababu hawapo peke yao,i think hii inaweza ikasaidia..Na kama wataleta fujo sheria ichukue mkondo wake.

Tatizo jingine ni kwamba hawa madereva hawana ajira rasmi.
 
Kapondo!

Niko nje ya Dar je kuna mtu anayeweza kuniambia hayo mabasi yameanza kuondoka au madereva wanaleta solidarity yao ya kipuuzi au wenye mabasi wako nyuma yao?

Kupasuka kwa tairi ya basi la Mohamed Trans ulikuwa ni uzembe wa dereva na mvua aliyopewa ni sahihi but nataka na mwenye hayo mabasi apande kizimbani kwani nae akiwa kama mmliki alishindwa kuhakikisha gari linaendeshwa likiwa na tairi nzima na zenye upepo wa kutosha!

Katika hali ya kwaida tairi ya tubeless huwa hapati bust kama imejazwa kwa kuzingatia viwango na haikuwa kipara!!!

Hawa madereva na wamiliki ifike mahali wajali wateja wao tusikubali watuburuze. Dereva hawezi kuchinja watu 30 halafu tukaita ni bahati mbaya.

Let us call it a day dereva akiua watu wanaozidi watano ikibidi anyongwe na iatapeleka ujumbe ili kazi ya udereva iheshimiwe. Kama ni dereva hata kama anaendesha bajaji akiua anakula life au kitanzi then those crazy cannibals should not have a palace in the society na hata barabarani yes we can do it!!!
 
Mimi nadhani ukiwa katika speed ya kawaida 80Km/h tairi za mbele zikipasuka hakutakua na athari kubwa sana. Ila huyu jamaa inavyosadikika alikua kwenye speed kubwa sana. Pia hatuwezi kulinganisha kesi ya ufisadi na utoaji wa roho za watu, uizi na ubadilifu wa mali ya uma ni ufisadi ambapo vyote vinaweza kutafutwa ila roho ya mtu ikishapotea utaitafuta wapi?

Madereva wanagoma kwani wengi wanatabia ya kuendesha kwa kasi na kutozingatia sheria za barabarani, wanaogopa wasikumbwe na mkasa wa mvua ya miaka. Mini naendeshaga mwenyewe kutoka Dar hadi Moshi. Lakini huko njiani kuna ukiukwaji sana wa sheria za barabarani. Utakuta mtu ana overtake kwenye kona, pasiporuhusiwa, wanapaki ovyo hasa malori, speed kali sana, penye speed 50km/h anaendesha mia

Mimi nadhani adhabu hii itakua fundisho kwa madereva wazembe na ninaiomba mahakama zetu hapa nchini zisicheleweshe kesi za namna hii. Mtu akiua halaiki ya watu namna hii haina tofauti sana na wanaojitolea mhana uko mashariki ya kati au mauajia ya jimbari, Darful n.k

Ungekua wewe ni mfiwa mmojawapo usingemtetea dereva hata kidogo. Umesababisha ajali kwa speed kali na kutofuata sheria za usalama barabarani then sheria ichukue mkondo wake.

Ila mimi nashangaa kwa nini mmiliki wa basi lile hajatiwa hatiani kwa makosa ya watendaji wake. Kifungu ni Skendo la Richmond amabapo Luwasa aliwajibishwa kutokana na Utendaji mbovu wa watendaji wake. Pia Mwinyi alijiuzuli akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na utendaji wa askari wake.

Nawasilisha hoja

Mkuu naona hujawapata watu vizuri. Chenge aligonga bajaj kwa nyuma akaua abiria wawili toka mwezi wa tatu mpaka leo kesi haijasikilizwa. nafikiri kama chenge angekuwa kwenye speed ya 50km/h akiendeshea kwenye njia za mjini na siyo Motorway/highway asingeua pia. Ila usukani wa chenge haukuwa na itilafu, mpaka leo anahudhuria vikao vya bunge. Sasa iweje dereva tairi limempasukia katika motorway ambayo hata speed limit sidhani kama kuna alama yoyote inayoonesha ni ngapi, chini ya mwezi mmoja ale mvua 30?. Je hawa madereva waliogoma nao si itabidi waogope kuendesha?, maana hujui kama tairi hazitapasuka na adhabu ya kupasukiwa tairi ni miaka 30 je ungekuwa wewe ungekubali?.

Usimamizi wa sheria na mfumo mzima una mashaka. Huwa nasema kila siku kuwa hakuna kitu muhimu kama kuwapa watu imani na mfumo. watu wakishaona mfumo haupo kwa ajili yao ni dhahili wataupinga. DITTO(R.I.P) Alipiga mtu risasi ikageuzwa kuwa manslaughter, Chenge kagonga kibajaji kilichokuwa kimebeba nyumba ndogo yake kesi haijulikani mpaka leo inaendeleaje. Wanachofanya ni delay tactic kufanya watu wasahau. Leo Dereva wa basi tairi limempasukia haraka haraka tunampiga mvua 30. Kweli hii ni haki?
 
TBC saa 7 mchana imesema upcountry journeys zimeanza,madereva wameshauliwa watafuta muongozo wa kisheria
 
Jamani Tanzania tunaelekea wapi. Dereva miaka 30, mafisadi wanapeta...
Kulikoni?...

Kimsingi ilitakiwa hawa madereva wadai haki kistaarabu, kwa kuteua wawakilishi wao (kama vile mwenyekiti wa chama chao madereva) kuangalia namna ya kukata rufaa kumsaidia mwenzao aliyehukumiwa, kama wanaona haki haijatendeka, sio kuwachelewesha abiria wao.

Hivi ingekuwaje kama mabasi ya mikoani yangekuwa ya SIRIKALI,2ngeona adhabu za mtindo huu,au wao wana device iitwayo accident removal so that kusingekuwa na ajali,Mbona kimya kuhusu Chenge?

Mabasi ya serikali yalikuwa, na yangekuwa decent sana, tofauti na hawa waendeshaji binafsi. Kumbuka enzi za KAMATA, TRC (mabasi sio treni) na UDA.

....Yule wa Chacha Wangwe kafungwa miaka mingapi?

Mitatu tu
 
adhabu kwa ujumla haikuzingatia sheria za usalama barabarani,haiwezekani na haikubaliki, kesi imeingiliwa na mambo ya kisiasa
 
du ila jamaa wanamsimamo mkali sana, kugoma watu wote si kitu raisi hasa kwa tz,
 
Sheria imekata mno kama ndo hivyo tunataka na Chenge nae kesi iende speed afungwe miaka 20 maana nae kaua la sivyo mgomo utaitishwa tena.
 
Back
Top Bottom