Mtoa mada anatuletea mchango wa akili ndogo uchangiwe na akili kubwa.
Nimeangalia mfuko mmoja mmoja
http://www.pspf-tz.org/?od=report
Local Authorities Pension Fund (LAPF)
Government Employees Provident Fund
Annual Reports - PPF Pensions Fund
Downloads | Annual Reports | Reports
pamoja na web ya SSRA ambako nimesoma current annual report ya SSRA,
https://www.ssra.go.tz/?page_id=553
Ukiangalia huko kote utaona kuwa ni PSPF pekee yenye kuweka annual reports zake wazi na utaona taarifa hadi ya 2013/14 tofauti na mifuko mingine yote isiyo weka taarifa zake wazi. Hii ni ishara ya accountability.
Pili, soma katika website ya SSRA utakuta na annual reports za mifuko nako ni PSPF inaonekana waazi taarifa zake za mwaka. Ukurasa wa 22 na 23 wa annual reports za SSRA utaiona PSPF ambayo mtoa mada anaiita imejaa foleni kwa hiyo inafilisika. Huko utailinganisha PSPF na mifuko mingine kama LAPF na GEPF utaona uhalisia wa mambo. Ukichukua net assets za LAPF na GEPF kwa pamoja hazifiki hata nusu ya PSPF ktk mwaka, chukua contributions za LAPF, PPF na GEPF kwa pamoja zoote hizi hazilingani na za PSPF ktk mwaka; Chukua total investments na membership size ya LAPF na GEPF kwa pamoja haziwafikii hata nusu ya hao jamaa wa PSPF. Hapa ofisini kwangu tuliandikishwa LAPF kwa kulazimishwa lakini kwa hakika nisingeingia huku kama ningeliyajua haya. Mara nyingi mifuko ya LAPF na NSSF imekuwa ikilalalmikiwa kwa kuandikisha wanachama kwa kuwalazimisha kupitia kwa waajiri wao.
LAPF kwa mfano imekuwa miaka 45 iliyopita lakini cha kushangaza ina wanachama chini ya 160,000 hadi leo wakati hao jamaa wa PSPF wana wanachama zaidi ya 320,000 ktk miaka 15 tu tokea 1999. Taarifa ya SSRA hii hapa mtoa mada. Soma ukurasa wa 22 na 23 ingawa najua kusoma kwako itakuwa mtihani.
https://www.ssra.go.tz/?page_id=553