Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

PSPF Tuhuma zimekua nyingi, inasemekana kuwa mfuko unapumulia gesi sasa wadau sisi kama watumishi inakuaje? yaani chenga zimekuwa nyingi balaaa.

kazi22.jpgkazi 1.jpgkazi 3.jpgkazi 4.jpg
 
Hapa kuna mchezo mchafu wa kuchafuana...
kwenye hizi pension funds Pspf ndo wako vzr!
bila shaka itakuwa kazi ya PPF hii kuhalikisha inawaharibia wenzao
 
Usikakamae na check namba yangu na kutotuma ukathibitisha kwamba ni uchuro,,kesho ukienda ofcn angalia 2013 mmepokea madai ya mafao ya kustaafu mangapi na katika hayo mmelipa mangapi kwa wakati gani,,halikadhalika kwa madai ya mirathi. angalia mwaka huu 2014 pia. Mnasumbua sana mtu anakaa miezi 6-8 toka ajira kukoma hamjalipa mafao kwa visingizio vya kubumba bana,mirathi ndo kabsaaa miaka inapita tokea mletewe nyaraka, mnatafutiza pesa toka sehemu mbalimbali mkipata ndo mnatoa hundi

Kassim umekimbia kitoto ama kweli unafiki ni kitu kibaya sana next time jipange ukileta uzushi jaribu kuutetea kidogo. .
 
Kassim Awadh nimeamini mawazo ya wengi kwenye hii thread kwamba wewe ni mtumishia au mwanachama mwenzangu wa LAPF unaetumika kuchafua mfuko wa PSPF. Wanachama wenzangu wa LAPF tuwe makini na watu hawa wanaotaka kutulaghai tufikirie majahazi ya wenzetu yanakwenda mlama wakati kwetu ndo panazama. Umeombwa cheque namba yako na mtu wa PSPF wakupatie ufumbuzi wa malalamiko yako unapga chenga zisizo na mantiki. Unasema ulikuwa unachangia hazina moja kwa moja kabla ya July 1999. Kama unadai mafao yako PSPF uende kaombe statement ya michango yako PSPF utaiona imeanzia July 1999 kisha kapate uthibitisho wa michango yako ya kabla ya julai 1999 huko Hazina kwamba hiyo michango yako ilipelekwa PSPF. Utaona aibu ya huu uzushi unaouleta hapa JF kwa kuwa utaelewa kwamba PSPF wanakulipa mafao hata ya kipindi ambacho hawana michango yako na hapo ndio utawambia PSPF, shikamoo! Tumika kuwachafua lakini uozo wetu LAPF utadhihirika muda si mrefu!

Mkuu situmiki na yeyote, nimeanza kuchangia pspf july 1999 walipoanzishwa, siwajui lapf. Ninachosema hapa ni magumashi ya pspf kwenye kulipaa mafao iwe ya kustaafu ama mirathi. kwa sasa kasi yao iko low, mie wamenambia mapungufu nikafika kwa mwajiri wangu na hatimaye kwao, mara ya mwisho wamenambia jina langu kwenye kadi ya benki ina utata, nimerectify hiyo Feb mpaka leo bado cjalipwa,,nimestaafu 2013 mpaka nije nilipwe na thamani ya hela ishashuka c sawa na kama ningelipwa mwaka jana. kama sio kufilisika ni nini? na kundi unalolikuta pale kila mmoja ana manung'uniko ya aina hiyohiyo
 
Mkuu labda ni kasoro zilizo kwako peke yako, Mirathi ya Mama yetu imechukua hardly 2 months PSPF washatoa cheque. Jaribu kwenda ofisini kwao upate suluhisho la tatizo lako kuliko kulalama humu.
 
labda wanataka ten percent.haka kanchi ka kitu kidogo bwana mzee.jipinde......
 
Jamani hivi ni kweli Pspf inasumbua kulipa mafao? Ninachojua mimi ni foleni oficin ndio kubwa bora nssf
 
labda wanataka ten percent.haka kanchi ka kitu kidogo bwana mzee.jipinde......

Nitapambana nao mpaka kieleweke, 10% marufuku cause ile ni jasho langu,,michango yangu na ya mwajiri kwa kipindi chote cha utumishi wangu na riba,,Pspf wajipange kuhudumia wanachama na kutulipa haraka iwezekanavyo sio ilivyo sasa
 
Mkuu labda ni kasoro zilizo kwako peke yako, Mirathi ya Mama yetu imechukua hardly 2 months PSPF washatoa cheque. Jaribu kwenda ofisini kwao upate suluhisho la tatizo lako kuliko kulalama humu.
Nimelipwa hatimaye mkuu,,lkn kwa ujumla jamaa wako hovyo bana. wewe ulikuwa na bahati yako tu kama unasema kweli na ulipwaji wa miezi mbili
 
Utafiti wa kutosha unahitajika kwa waajiriwa wapya !
 
Baada ya kukanusha kwa matangazo katika vyombo vya habari kuhusu hali mbaya ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Mkurugenzi wake, Adam Mayingu, sasa amekiri kuwa na hali mbaya.

Amesema Mfuko huo una hali mbaya kifedha na huenda ukafa baada ya miaka mitatu ijayo, endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuunusuru.

Mayingu alisema hayo mjini hapa jana mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo baada ya kuona hali hiyo, iliitisha mkutano wa dharura wa viongozi wa PSPF na Wizara ya Fedha, ili kuona namna ya kuunusuru.

Serikali ilikiri kuhusika kuudhoofisha Mfuko huo, na kuahidi mbele ya Kamati hiyo, kuwa itachukua hatua za haraka wiki hii, kwa kuanza kulipa madeni inayodaiwa na PSPF ikiwa ni hatua ya mwanzo ya kuukomboa.

Akitoa maelezo kuhusu hali ya Mfuko, Mkurugenzi huyo alisema unakabiliwa na uhaba wa fedha, kutokana na madeni makubwa yaliyoko nje yanayosababisha uwezo wa kifedha kufikia asilimia 10 tu.

"PSPF kwa sasa uwezo wake kifedha, umeshuka na kufikia asilimia 10 kiwango ambacho ni cha chini, ikilinganishwa na kiwango kilichowekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA), ambapo kila Mfuko wa hifadhi hutakiwa angalau kuwa na uwezo wa kifedha wa asilimia 40," alisema Mayingu.

Alisema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa za kuuokoa, ikiwa ni pamoja na Serikali kupitia taasisi zilizo chini yake kulipa madeni yao yanayodaiwa na Mfuko huo, baada ya miaka mitatu utakuwa umekufa kwa kushindwa kujiendesha.

Mayingu alisema hadi sasa Mfuko umefanya tathmini takribani tatu, za namna ya kupandisha kiwango chake kifedha na matokeo yalionesha kuwa tatizo kubwa la PSPF ni mlundikano wa madeni inayodai nje.

"Pia Serikali ilifanya uchunguzi kwa upande wake kwa Mfuko na kubaini kuwa mwaka 1997, Serikali ilitakiwa kuuchangia kutoka michango ya watumishi wake wastaafu kiasi cha Sh bilioni 250.

"Ripoti hiyo ilitabiri kuwa kiwango hicho kingeweza kupanda na kufikia Sh bilioni 658.23 mwaka 2006, na hivyo Serikali ilitakiwa kuongeza michango," alisisitiza.

Mayingu alisema Mfuko ulianzishwa bila fedha za kuuwezesha kufikia kiwango kinachotakiwa kuuendesha, na katika tathmini ya kwanza mwaka 2003, kabla ya Mfuko kulipa mafao, ilionekana Serikali inadaiwa fedha za wastaafu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, PSPF ilibeba mzigo wa Serikali baada ya kuanzishwa ambao sasa ni deni lililofikia Sh bilioni 933.4.

Alisema deni hilo, linatokana na malipo yaliyofanywa na Mfuko kwa wastaafu waliokuwapo kabla ya kuanzishwa, ambapo PSPF kwa wakati huo ilikuwa na uwezo wa kulipa mafao hayo kwa asilimia 93.3 lakini tangu ilipe fedha hizo hadi jana Serikali haikuwa imefidia deni hilo.

Katika tathmini ya pili mwaka 2007 baada ya Mfuko kuanza kulipa mafao, ilionesha kuwa hali inazidi kuwa mbaya, kwa kuwa deni ambalo Serikali inadaiwa, lilikua na kufikia Sh trilioni 3.3 huku uwezo wa fedha wa Mfuko ukishuka hadi asilimia 40.

Katika tathmini ya tatu mwaka 2010, ilionesha hali ya mfuko kuzidi kuwa mbaya, kwani uwezo wake kifedha ulishuka hadi asilimia 10 huku deni la nje likikua hadi Sh trilioni 6.4.

"Kitendo cha Serikali kushindwa kulipa angalau robo ya madeni haya, kinarudisha nyuma juhudi za Mfuko za kuboresha huduma zake kwa wateja," alisema.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Kawawa (CCM), alisema ni wakati wa Serikali sasa kuanza kulipa madeni kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko mara moja ili kuuokoa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alionesha kusikitishwa na kitendo cha Serikali kuchelewa kulipa madeni hayo, na kuuweka Mfuko katika hali mbaya.

"Hali ingekuwa tofauti kama Mfuko ungelipwa Sh bilioni 250 tangu mwanzo kabla ya kuanzishwa," alisema.

Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, alikiri kuwa Serikali haikuutendea haki Mfuko huo na kuahidi kushirikiana na wenzake kutafuta suluhu ya tatizo hilo.
 
Michango wanayokusanya wanapeleka wapi? Au wameisha shinikizwa kutoa za uchaguzi?
 
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, alikiri kuwa Serikali haikuutendea haki Mfuko huo na kuahidi kushirikiana na wenzake kutafuta suluhu ya tatizo hilo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene???????????????????????????
 
Tatizo lingine kubwa la mfuko huu ni formula Yao ya kulipa mafao. The formula is unrealistic
 
Back
Top Bottom