Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Madeni ya Serikali yaiweka PSPF njia panda

Mkuu Naunga mkono hoja yako maana hawa jamaa kazi yao kupotosha ukweli, hivyo watakao kubali kudanganyika watakuwa wamepotea maana zama hizi za ushindani watu wa mifuko wamekutwa hawaishi kuzuliana mambo ambayo hata hayapo.
Mimi nimshauri Mtoa mada atoe taarifa kwa viongozi wa pspf ili suala lake liweze kushughulikiwa maana kuna baadhi ya watu ni wepesi kulalamika pasipo kujua kuwa wao wamechangia kisasi gani. Chukua hatua Fika katika ofisi zao omba kuonana na viongozi wa juu si kulalamika kwenye social media it won't help.
Swali la kujiuliza ni WHY PSPF na si zinginezo?
 
jamani,ni kweli kabisa,mama yangu amestaafu mwezi wa 12 mwaka jana,kiukweli tunahangaika sana,ametembea na kuhangaishwa sana,mara hiki hakipo mara kile,amevitafuta vyote na kuvipata,ameambiwa aende kesho,sasa kama habari ni hii kesho mtausikia moto wake,ataomba ruhusa ya kwenda ikulu lazima,namjua mama amepoteza imani na pspf,kiukweli amenishauri mimi na wadogo zangu kutojaribu kujiunga na mfuko huo.............kama habari ndo hii MUNGU AINGILIE KATI MAMA ALIPWE.
 
Kwanini PSPF sababu ni moja tu kuna mifuko haina hoja katika ushindani hivyo wanatumia kila namna kuuchafua mfuko wa PSPFmojawapo ni habari za kizushi hi vyema tukashindana kwa hoja..aliyeanzisha thread hii hajatuma kile nilichoomba toka majuzi..na yeye no mzushi??sijajua bado namsubiria..
 
jamani,ni kweli kabisa,mama yangu amestaafu mwezi wa 12 mwaka jana,kiukweli tunahangaika sana,ametembea na kuhangaishwa sana,mara hiki hakipo mara kile,amevitafuta vyote na kuvipata,ameambiwa aende kesho,sasa kama habari ni hii kesho mtausikia moto wake,ataomba ruhusa ya kwenda ikulu lazima,namjua mama amepoteza imani na pspf,kiukweli amenishauri mimi na wadogo zangu kutojaribu kujiunga na mfuko huo.............kama habari ndo hii MUNGU AINGILIE KATI MAMA ALIPWE.

Kesho ni mei mosi mkuu nitumie cheque namba ya mzazi wako kwa pm usiwe kama Kassim awadh hajatuma mpaka sasa
 
Kesho ni mei mosi mkuu nitumie cheque namba ya mzazi wako kwa pm usiwe kama Kassim awadh hajatuma mpaka sasa

Mwakajila, Nadhani wewe ni staff wa pspf kama ni sahihi nijibu. Kuhusu huyu Mtoa mada anayejiita kassim awadh huyu atakuwa ni pandikizi na mapandikizi ni wengi humu ambao wanatumwa kuichafua pspf. Mimi ni mwanachama pspf, ninae mdogo wangu ambaye yuko chuo fulani hapa nchini kuna mfuko mmoja wanaojiita LAPF walienda chuoni kwao wakaichafua sana pspf kwa habari kama hizi za uzushi na strategy mojawapo ambayo waliwafata baadhi ya wanachuo na kuwapa somo kuwa wawe wanawachafua pspf basing kwa maarifa ya magazeti ya mwaka jana may yaliyopotosha maarifa ya CAG Kwa ahadi ya kuwalipa ujira wapo waliokubali na wengine wakakataa; wengine waliahidiwa ajira kwa wale walioko final year.
Kwa hiyo huu ni mpango kabambe wa LAPF kuwachafua kupitia social media. Hivyo yatakuja mengi tu....
Pspf kwa kweli mimi nawapenda bure huduma zenu ni nzuri sana na mafao yenu kwa kweli ni mazuri mnajitahidi sana. Mungu awalinde dhidi ya wenye hila.
 
Hivi SSRA si walisema kutakuwa na formula moja ya kulipa mafao kwenye mifuko yote?
 
Belo, ukishajua ni nan aliyetangulia kuwepo kati ya SSRA na mifuko ya hifadhi ya jamii, utaelewa kama hyo formula moja itakuja kweli au la.
 
Belo, ukishajua ni nan aliyetangulia kuwepo kati ya SSRA na mifuko ya hifadhi ya jamii, utaelewa kama hyo formula moja itakuja kweli au la.

Huwa najiuliza hii SSRA ilianzishwa kufanya nini?
Inaonekana hawana ubavu kabisa kwa hii mifuko ya jamii
 
Kati ya vitu ambavyo naiomba SSRA inifanyie mimi kama mwanachama wa LAPF ni kuwalazimisha waweke wazi ripoti zao za fedha za mwaka. Yani huwez kuziona kokote , sio ktk website ya ssra wala ktk website yao. Tumeshalalamika sana hawatak kusikia na wako hata humu Jamiiforums. Kazi yao kutembea na vipande vya magazeti utadhan tuko kwenye ngoma za vigodoro!
 
Vichwa vya panzi utawajua, hivi unaposema sema kuwa Mfuko/Taasisi fulani imekufa kwa sababu inadai. Hivi kwa akili ya kawaida anayefilisika ni yule anayedai au mdaiwa. Kwa uelewa wangu serikali yetu inadaiwa sana. Ndo maana deni la taifa ni zaidi ya trillion 20 na la pspf ikiwa ni sehemu ya deni., ila serikali inajiendesha haijatangaza kufilisika. Sasa nyie mnaotembea na kupiga ukunga wa kifo nawashangaa sana. Serikali ilishaanza kulipa deni hilo Sasa nyie mnataka tu kuwazungumzia pspf wakati wenzenu wanachapa kazi. Tumeshajua hizi ni zama za ushindani hivyo mnawachafua wenzenu ili mpate wanachama kwa kuwalaghai.
Taasisi nyingi zina idai serikali, hata mifuko mingine ya hifadhi ya jamii pia ni mojawapo. Acheni kupotosha kwa malengo ya kuwachafua wenzenu, mnatakiwa mmbuni mbinu mbadala za kiushindani kwa kuwa weledi zaidi. Acheni propaganda zisizokuwa na kichwa wa miguu.

Ukiwa unamdai mtu yeyeyote kihasibu inatakiwa iitwe debtors na hukaa kwenye asset kama unadaiwa lazima useme creditors yaani watu wanao kudai na huwa upande wa liability sasa mkuu figure hiyo ukisoma si unaona moja kwa moja ni accrual liability. Na haiko upande wa asset za mfuko isipokuwa liability.
 
Kati ya vitu ambavyo naiomba SSRA inifanyie mimi kama mwanachama wa LAPF ni kuwalazimisha waweke wazi ripoti zao za fedha za mwaka. Yani huwez kuziona kokote , sio ktk website ya ssra wala ktk website yao. Tumeshalalamika sana hawatak kusikia na wako hata humu Jamiiforums. Kazi yao kutembea na vipande vya magazeti utadhan tuko kwenye ngoma za vigodoro!

Nenda kwa website yao lapf ssra sio lapf.mimi sheria tu inanikaba ningeamia huu mfuko .
 
Mwakajila, Nadhani wewe ni staff wa pspf kama ni sahihi nijibu. Kuhusu huyu Mtoa mada anayejiita kassim awadh huyu atakuwa ni pandikizi na mapandikizi ni wengi humu ambao wanatumwa kuichafua pspf. Mimi ni mwanachama pspf, ninae mdogo wangu ambaye yuko chuo fulani hapa nchini kuna mfuko mmoja wanaojiita LAPF walienda chuoni kwao wakaichafua sana pspf kwa habari kama hizi za uzushi na strategy mojawapo ambayo waliwafata baadhi ya wanachuo na kuwapa somo kuwa wawe wanawachafua pspf basing kwa maarifa ya magazeti ya mwaka jana may yaliyopotosha maarifa ya CAG Kwa ahadi ya kuwalipa ujira wapo waliokubali na wengine wakakataa; wengine waliahidiwa ajira kwa wale walioko final year.
Kwa hiyo huu ni mpango kabambe wa LAPF kuwachafua kupitia social media. Hivyo yatakuja mengi tu....
Pspf kwa kweli mimi nawapenda bure huduma zenu ni nzuri sana na mafao yenu kwa kweli ni mazuri mnajitahidi sana. Mungu awalinde dhidi ya wenye hila.

Hakuna shaka uyasemayo mkuu karibu sana
 
Unapokuwa na jukumu la kulipa je ni asset au liability?wahasibu tusaidieni
 
Umetumwa na ukawa wewe, pspf wapo safi sana na wanalipwa vizuri kuliko mifuko mingine
 
Wakat hata wa 2011 mkuu bado.sie kama familia tunajipanga kuwaburuza mahakamani wamekuwa wakitusumbua tangu mwaka 2011
 
Sisi Watanganyika tuna tabu moja kubwa. Haki zetu za msingi na mifumo huwa hatuzidai lakini ni wepesi kulalamikia process. Mtu analalamika eti foleni mwingine analalamika eti mama yake kazunguka hadi kawashauri kutojiunga na mfuko flani. Huyo mama anakaa kwenye benchi hospitali akienda na kadi yake ya NHIF kusubiri watu wa cash wahudumiwe kwanza hajalalamika, kule ambako hakuchangia chochote kwa zaidi ya miaka 25 ya utumishi wake kabla ya 1999 na analipwa pensheni tena ya kikokotowo cha juu kulko mifuko yote TZ inayojumuisha hata kpindi ambacho hakuchangia hata senti anapakosea fadhila.
 
Kesho ni mei mosi mkuu nitumie cheque namba ya mzazi wako kwa pm usiwe kama Kassim awadh hajatuma mpaka sasa

Usikakamae na check namba yangu na kutotuma ukathibitisha kwamba ni uchuro,,kesho ukienda ofcn angalia 2013 mmepokea madai ya mafao ya kustaafu mangapi na katika hayo mmelipa mangapi kwa wakati gani,,halikadhalika kwa madai ya mirathi. angalia mwaka huu 2014 pia. Mnasumbua sana mtu anakaa miezi 6-8 toka ajira kukoma hamjalipa mafao kwa visingizio vya kubumba bana,mirathi ndo kabsaaa miaka inapita tokea mletewe nyaraka, mnatafutiza pesa toka sehemu mbalimbali mkipata ndo mnatoa hundi
 
Sisi Watanganyika tuna tabu moja kubwa. Haki zetu za msingi na mifumo huwa hatuzidai lakini ni wepesi kulalamikia process. Mtu analalamika eti foleni mwingine analalamika eti mama yake kazunguka hadi kawashauri kutojiunga na mfuko flani. Huyo mama anakaa kwenye benchi hospitali akienda na kadi yake ya NHIF kusubiri watu wa cash wahudumiwe kwanza hajalalamika, kule ambako hakuchangia chochote kwa zaidi ya miaka 25 ya utumishi wake kabla ya 1999 na analipwa pensheni tena ya kikokotowo cha juu kulko mifuko yote TZ inayojumuisha hata kpindi ambacho hakuchangia hata senti anapakosea fadhila.

Hapo kwenye red,,kabla ya 1999 PSPF walipoanzishwa watumishi wote tulikuwa tunachangia hazina moja kwa moja. Hata leo pspf wakikokotoa na kukulipa mafao yako kwa kuhesabu miaka/miezi yako ya utumishi including ya kabla ya wao kuanzishwa,,kiasi kile wana 'claim" hazina na wanapewa.Acha kupotosha, nyie jipangeni kuthibitisha hamjafilisika lipeni wastaafu na warithi mafao yao kwa wakati thats all. Sio hivi mnavotuhangaisha
 
Kassim Awadh nimeamini mawazo ya wengi kwenye hii thread kwamba wewe ni mtumishia au mwanachama mwenzangu wa LAPF unaetumika kuchafua mfuko wa PSPF. Wanachama wenzangu wa LAPF tuwe makini na watu hawa wanaotaka kutulaghai tufikirie majahazi ya wenzetu yanakwenda mlama wakati kwetu ndo panazama. Umeombwa cheque namba yako na mtu wa PSPF wakupatie ufumbuzi wa malalamiko yako unapga chenga zisizo na mantiki. Unasema ulikuwa unachangia hazina moja kwa moja kabla ya July 1999. Kama unadai mafao yako PSPF uende kaombe statement ya michango yako PSPF utaiona imeanzia July 1999 kisha kapate uthibitisho wa michango yako ya kabla ya julai 1999 huko Hazina kwamba hiyo michango yako ilipelekwa PSPF. Utaona aibu ya huu uzushi unaouleta hapa JF kwa kuwa utaelewa kwamba PSPF wanakulipa mafao hata ya kipindi ambacho hawana michango yako na hapo ndio utawambia PSPF, shikamoo! Tumika kuwachafua lakini uozo wetu LAPF utadhihirika muda si mrefu!
 
Back
Top Bottom