Hivi inakuwaje unakutana na demu ambaye sio mtu wako wala hakuwahi kuwa mtu wako ila mnafahamiana fresh tu... Lakini unakuta baada ya muda mrefu wa kutokuwasiliana siku ukijichenga tu ukampigia au ukamtumia sms badala ya jibu unalotarajia utasikia "nikopeshe laki na nusu nina shida nayo ntakurudishia!"... Au siku hiyo unaitwa "dear nina shida na elfu hamsini ya salon"... Sasa unabaki unashangaa mazoea hayo yameanzia wapi!!? Na kwanini mpaka ukimtafuta tu ndio anatangaza shida zake?? Mbona ukiwa kimya hakutafuti?? Girls u need to change... Shida zenu zisiwadhalilishe!! Mdau unasemaje kuhusu hili!!?
Haki ya nani Madame B!! Mapishi harufu duh..
Kwa hyo kunitanua unitanue, afu mshiko usinipe.
nilikutana na mmoja badoo one week baada ya kuonana aliniomba pesa ya matibabu elfu themanini na akanitumia picha yake ya utupu through whats app nilikomaje
kwani raha wewe hupati? kwa nini wewe usimpe mshiko huyo anayekuingizia dushelele? acha hizo mkuu
kufuatana kama kumbikumbi haifai. halafu gharama, wewe utabaki nyumbani kwa muda tu
Hapa anazungumzia ndo kwanza mmeanza mawasiliano hata week haijaisha ndo mizinga inaanza,si bora ukute hata umesha duu nae ,hata kufahamiana vizuri bado ashaanza mizinga
Mhnnn... Kweli kila uzi na komenti zake... Nimekukubali Madame BKati ya kinu na mchi nani anaumia pale kitu kinapotwangwa?
Za kuambiwa changanya na zako.
Njoo afu usinipe mshiko...uone.
Demu kumjua siku ya pili tu anataka umnunulie simu mpya, halafu hapohapo hata kabla hujanunua simu kashaanza kukuchomekea habari za kumtengeneza nywele.
Hata kama ulikuwa na moyo wa kutoa kama Mama Theresa uzalendo utakushinda.