MADAM SPEAKER: Rai... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MADAM SPEAKER: Rai...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Apr 24, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Spika.jpg

  karibu sana nimefuatilia shughuli zako za bunge hili la saba ambalo limetwikika mabegani mwako sawasawa. Ni kazi nzito, Ngumu yenye changamoto nyingi..

  Kumbuka kwamba Bunge Hili la Tanzania kwa miaka mingi sana liliongozwa kiimla chini ya Mzee wetu Adam Sapi Mkwawa, Imagine Tokea 1962 hadi 1994 alikikalia kiti cha Bunge, tulishajua ndiye Speaker wa Milele wa Bunge,hatukuwa tunaelewa na Chochote maskini ya mungu toka kwenye kajengo ka pale Karimjee.. Mie sijui walikuwa wanafanyiana nini humo ndani, ingawa pale katikati yaani 1973-1975 Chief Erasto Mangenya alikikalia kiti cha ubunge kwa-tumiaka tuwili kabla ya Mzee Mkwawa kuendelea tena.

  Ingawa kwa heshima Bunge lako lililovumbuliwa mnamo 1953 na spika wa kwanza Mzee Karimjee alikalia uspika kwenye vuguvugu la vyama vingi TANU, UTP na ANC akatuvusha kwenye Uhuru Tukajipatia Mwalimu Nyerere Julius ambaye alisaini sheria zetu badala ya kuzivusha baharini hadi kwa malkia.

  Madam Speaker, Ukumbuke pia kwamba Vuguvugu la vyama vya kisiasa vilifufuka tena 1992, na kufuatiwa na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari ambapo ndipo kwa mara ya kwanza matongotongo yanatutoka kwa kuona ITV ilipoanza 1994 baada ya kukaa kwenye kiza cha kupata habari-picha makumi ya miaka, ingawa Kenya "redio hii ya sinema" wenzetu tokea 1960 wanaangalia TV. Hali hii ikafuatiwa na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 ambapo Mhe Pius Msekwa aliendelea kuutwaa uspika alioupokea kwa Mkwawa tokea 28,April 1994. Yeye alidumu nao kwa miaka Kumi na moja hadi 2005, ambapo alitamani nae kuendeleanao tuu ila mzee Sita akamwekea Kigingi. Yeye Sita akakishika kijiti cha uspika kwa miaka mitano tu hadi 2010. Alitamani sana kuendelea na uspika ila mama wewe Ukasema No.. na wanawake embu Tujaribu .. wakatiule kamsemon""wanawake wanaweza wakiwezeshwa" kakitawala, ingawa sasa kameshachakachuka sana "wanaweza hata wasipowezeshwa".

  Sasa kwanini nakutupia hoja hii,Kumbuka wakina baba hawa wamefanya kazi nzuri ya uspika, hasa mzee sita na bunge la kasi na viwango na Msekwa. Sasa niko makini nakufuatilia kila bunge ila nina mashaka na mwenzetuwewe.. unaturudisha kwa bunge la Mzee Sapi Mkwawa ..

  Kwanza Ulipoingia kwenye kiti hicho ulianza na mbwembwe kwa ile kaulimbiu yako kwamba, "Bunge linaongozwa na kanuni, na Ni kanuni hizo za bunge ndizo utakazo zitumia kwa kwenda mbele hatuangalii sura ya mtu " tutukasema mwanamke hapa kaamua, tukatarajia sheria kweli zitachukua mkondo wake,baadae ukajaziliza mavitabu mengi ya sheria na kanuni zake. mara katiba, mara kanuni za Bunge..mezani kwako, ukayasoma mpaka ukawa unayachanganya changanya, ukawakuta mjengoni vijana ambao wanazijua kanuni za bunge as if wao ndio waliozitunga. Ukataka ushauri kwa wazoefu wakakwambia usiwe serious sana bungeni, do it as a kitchen job, akalegeza msimamo hadi ukawa unapwaya, wewe kwa asili hujui matani sasa ukimtania mtu atadhani unamtukana, huna kipaji hicho..

  Ukabadili stail ukaona uliongoze Bunge Kibabe kwa kamsemo "hivi hawa wananiona mie mwanamke ndio wanichezee sio, ngoja niwaonyeshee", ukaingia kibabe lakini ukagonga ukuta wa vikanuni .. mpaka wabunge wanakutaka ujitolee mwongozo, ukatorokea nyumbani, wiki kadhaa unaliangalia bunge ukiwa hom..

  Tabia ya Kumwachia Ndugai Bunge, imekuwa haiwafurahishi "mabosi"ambao wanasema wewe spika ndiye uliyemezeshwa siri za serikali sasa kwanini muda mwingi gari liendeshwe na dereva asiyejua siri za safari. Sasa maneno hayo yamekufanya ukikalie kiti upende usipende , na sasa huna msimamo kamili, kadiri siku zinavyoendelea bungeni changamoto kali zinaibuka zenye vuguvugu kali za kisiasa. Na kadiri unavyolihandle Vuguvugu hilo hali inazidi kuwa dhoofu sana kiutendaji na kwa kasi unapoteza mvuto kwa jamii..

  Inshu sio CHADEMA kama unavyolalamika all ways. Mbona Mhe Sita, Mhe Msekwa waliongoza Bunge kama hilihili.. Inshu ni wewe..

  Labda Nikushauri yafuatayo

  1. Bunge sio Yote katika maisha yako, Kukubali kushindwa ni Ushindi. Achia Uongozi wa spika, atauchukua mwingine tena tujitahidi awe mwanamke na ataendelea tu. Kubali kwamba Huwezi kuwa kiongozi wa kila kitu. Uongozi ni kipaji, kama huna huna tu.

  2. Au Achana na sura za watu Bungeni, Chapa kazi yako, Tenda haki, Fuata kanuni na taratibu za bunge, Usipendelee Upande wa wabunge wala usipendelee upande wa serikali. Mwenye haki mpe haki.. Usiogope kwamba baadhi ya maamuzi ya Bunge yataathiri Chama Chako, achana na mambo ya chama, weka wananchi mbele kwanza, kazi mbele , chama baadae. Chama kikibeba wajibu wake hakitakufa, kikikaidi kufa kitakufa tu.

  3. Wanawake wengi wanakuangalia kama ishara ya uadilifu na uthabiti wa uongozi. Utavyotenda Bungeni sasa utahamasisha bunge la 2015 kujaa au kupungua kwa idadi ya wanawake. ukiendelea kuongoza Bunge kwa staili hizi za Kimanati utaua Sifa ya mwanamke kwenye Uongozi huku ukiwasaliti, kuwatosa na kuwaabisha wanawake. mvuto wa uongozi kutoka kwa wanawake Tanzania utauangamiza mbele ya jamii, hata wanawake kujihisi si kitukukamata nafasi kubwa za uongozi. itachukua miongo mingi baadae ili jamii iweze kubariki tena dhima ya kuongozwa na Mwanamke kwenye sekta nyeti na kubwa. Nina imani bado una Muda mzuri wa kusahihisha makosa, Tunakutaka uwe jasiri, shupavu na usiyeyumbishwa.

  4. Uwe unakunywa maji mengi pamoja na cocacola,..

  Asante Madam Speaker.

  ...
  YA LEO

  update nyingine 2013
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  salute.....
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuanzia sasa natangaza rasmi kuna baadhi ya watu nitakuwa nasoma thread zao mojawapo ni wewe Salma25. Unanibariki sana. Mfano nakumbuka rai yako wakati wa uchaguzi wa Igunga, Arumeru na leo hii. Big up mdada.
   
 4. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mama kigeugeu sn,anahitaji maombezi huenda anapepo wa kuchukia taifa,chama siyo kitu tena mama anatakiwa awe mtu wa taifa na si wa sisiem kwa nafasi aliyonayo.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Salma25 umeandika vizuri. Nakupa big up! Lakini binafsi nina shaka moja, je mbuzi atacheza chuni ya nyizi za gitaa lako? Kuna uchawi ambao ukiisha logwa hakuna tena dawa wala mganga wa kukutibu. Ukinywa maji ya bendera ya sisiem kamwe hutakaa uweze kutofautisha kati ya haki na dhulma na kwa kuwa kuna watu wasioweza kuhitimisha jambo kwa kumpaka mnafiki mafuta kwa mgongo wa chupa, mnahitimisha kwa kusema dawa ya mnafiki na msaliti ni kuvunjika shingo.
  .
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyu Mama kha ..ametudhalilisha kina mama ameshindwa kazi ..hakana maamuzi .....:(
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Yani anachonikera zaid ni pale mbunge anapomaliza kuongea na yeye anadakia na vijimaneno vya kebehi, natamani siku moja akiropoka ashtukie katandikwa ngumi ya taya kihere+here kitaisha
   
 8. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Imetulia!

  I admire your Intelligence!
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  It is a wonderful piece.... Salute to you Madam!

  Madame Speaker is a "Disgrace" to CCM, to herself, to Women na wananchi in Particular.... Toka mwanzo alitaka afanye ile kazi kwa kuonesha/kujionesha kua anaweza na NOTHING can go wrong. Akasahau na hakutambua kua haya mambo as much as yategemea ushauri katika jopo lake la pembeni la washauri Muhimu zaidi ni relying on one's Intelligence, Insticts and honor. Angetenda haki kwa kufuata what is right and what na what is wrong.... badala yake matendo yake ni kua she always wants to prove kua anaweza/yeye ndie yeye/yupo strong (ambayo haelewi maana yake for Ubabe sio kua strong).

  Kwa upande mwingine naona tusimlaumu saana.... Ukweli ni kwamba HAWEZI, HAFAI, wala hana the intelligence required for the job. Huwezi kukimbiza upepo... kama HUWEZI - HUWEZI tu! Na kwa kweli as sad as it is to say... katika wanawake ambao wanawakilisha mahala mbali mbali katika nafasi nyeti hapa nchini... Katuangusha na katutia aibu. Sio kwa wanawake tu bali na Wananchi kwa Ujumla... she is useless kwa kweli.... Sad.
   
 10. s

  sanjo JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Is this Speaker having proper job description and smart objectives? are these objectives SMART [specific, Measurable, Achievable, Relevant and Time bound] enough? Where is she answerable to?
   
 11. e

  ebrah JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi Hugh mama ana mime na watoto kweli? Mwanaume kutokuwa na uchunngu na nchi si ajabu sana, kwani hatafamilia huwa wanatelemeza na kwenda kufight! But sijaona mwanamke Mwenge watoto akawakana watoto wake kwani anakumbuka uchungu alioupata, sa nikimwangalia makinda Mapatano wasiwasi!
   
 12. R

  Rev. Damasus Mkenda Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanawake wanasema "wakiwezeshwa wanaweza" but when things go wrong dont go with them madam Anne. God help you. Amen!!!
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tusimlaumu sana, hiyo post aliipata kwa njia ya "Viti Maalum", viti maalum vingi havipatikani kwa merit bali kwa upendeleo. CC ya CCM walisema this time wanataka Spika Mwanamke, maana wanawake wakiwezeshwa ... wanaweza!

  Sikumbuki kwenye hiyo post alipambanishwa na nani, wakati mwingine huwa naona hata yule Mwalimu wa Shule ya Msingi Jenister Mhagama ana uwezo mkubwa kuliko hata Mama Makinda pamoja na usomi wake na kuwa kwenye politics kwa zaidi ya miaka 35 sasa.

  Haya ndio madhala ya "Viti Maalum", huyu Mama atakuwa loyal kwa CCM kuliko hata kwa Wabunge waliompa kura, maana CC ndio iliamua kuwakata wanaume competent ili wampe mwanamke hiyo nafasi. Kwa hiyo bila msaada wa CC leo hii huyu Mama asingekuwa Spika. Kwa sasa analipa fadhila kwa waliomuweka hapo ambao ni CC kwa kushirikiana na mafisadi waliom-tip tangu mapema kwamba gombea then tutajua namna ya ku-fix mambo kwenye vikao vya uteuzi. Ogopa politics za CCM, na ndio maana tunaishia kupata magarasa kila kona!
   
 14. m

  mtembez Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :smile:
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, I secind you,
  Jenister ni mashine nyingine kabisa.
  Ni mfano halisi wa walimu - sio hawa wa siku hizi lakini!!!:rolleyez:
   
 17. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  tuna vichwa humu. I salute you madam.
  imetulia hiyo mada yako
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  sanjo CV ya madame Speaker is Impressive on paper..... However that alone is not enough, for any Leader to be Great at what they do they also have to have inborn natural insticts and Intelligence to be able to Lubrically run the area they are committed and those within reach. She was Sitta's right hand for God sake! That alone ilikua tosha for her to perfom better... She has no excuse whatsoever of being such a blunder.
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180

  Haya mambo ya kuwezesha wanawake yana Mipaka yake.... Hio ni wazi na hata JK, Viongozi et al wanaelewa hilo. Basi tu sababu tu wameshazoea "power abuse". Huwezi mpa mwanadamu yeyote nafasi kama "Speaker wa Bunge" kwa vigezo vya upendeleo na Kuwezeshwa... It is Crazy.

  One thing I can vouch ni kua hata wao CCM wameona kua ni Mistake kubwa walifanya kumuweka Madame Makinda katika hio nafasi. Ukikumbuka wakati wa mchakato wa U-speaker, ilikua ni wazi kabisa kua Makinda alichaguliwa sio sababu ya kuwezeshwa bali kwa sababu tu ya Kuepusha Sitta kupata hio nafasi tena (just because the guy alikua haangalii Chama ama sura ya mtu when it came to matters of the Parliament, among other reasons/propagandaz).

  Wakawa wameangalia tu hilo suala on the surface wakisahau kabisa kufanya utafakari wa timing (kua saizi Siasa zilikua zinawiva kwa kasi ya juu na Upinzani una nguvu kubwa hivo ilitakiwa a Strong reliable Parliament Speaker); wakisahau kabisa kuangalia Circumstances (ni wazi kabisa hio ni nafasi ambayo ni lazima madame awe challenged for kwanza ni CCM, wazi kapendelewa na tupo katika jamii ambayo a Woman has to work twice as hard to be appreciated). Kitendo ambacho hakija cost wananchii tu... Bali hata wao wenyewe CCM (Mfano halisi ni her remarks on JK na mambo ya posho wakati wa migomo wa madaktari dhidi ya Serkali iliyo kua contrary na tamko la JK that morning.... hana hata chembe ya busara - a catasrophy kwa nafasi aliyopo).
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Binadamu tupo wa aina nyingi. Hujaona mwanamke analea mimba miezi 9 halafu anatupa mtoto chooni, kwenye mfuko wa rambo; anazaa, analea, ikifika wiki, miezi, miaka anatupa mtoto?

  Huyu Mama anaweza kuwa wa aina hiyo au kubwa zaidi, anaweza hata kuwa mchawi. Mchawi hutoa kikoa (mtu) wake kwanza. Huyu Mama amewatoa kikoa wanawake wenzake na Watanzania kwa jumla.
   
Loading...