Wabunge wote wa upinzani watoka bungeni baada ya Spika kukataa kuahirisha bunge

wabunge wote wa upinzani yaani wa CUF, CDM, TLP ,NCCR wametoka bungeni kupinga kitendo cha spika kukataa kuahirisha bunge kwa dharura ili kuweza kutoa nafasi kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya meli inayozama Znz.

Alitoa hoja Hamad Rashid kuwa Bunge lipitishe bajeti kabla ya mawaziri kuhitimisha ili kutoa nafasi kwa wabunge kufuatilia na kuweza kusafiri. Spika akamjibu kuwa hoja hiyo ingefaa kama maafa yametokea karibu na Bunge kama Chamwino etc ili wabunge waende wakatoe damu .

Hali ni mbaya , Bunge linapitisha bajeti kwa suala gani?
 
hata wambunge wa CCM hawazidi kumi ukiondoa wanao unda sirikali. Huyo naibu waziri anatoa majibu ya hoja kama hajui kusoma!
 
Wabunge ni wawakilishi wa wananachi, sasa wanaongea nini huko Dodoma wakati wananchi wenyewe ndio hao wanazama baharini? Makinda anasimia bunge la wawakilishi wa nchi ipi? Huu mchezo wa kuendesha bunge kama kikao cha CC leo umeingia sura mpya, na wabunge wa CCM wanapitisha bajeti ya kununua sanda? Watanzania wanazama as we write, wanaongoe nini hawa watu????? arrrrrggg
 
Hata G/mboto alidharau hivyo hivyo, lakini alipowatembelea wahanga akatoa machozi, sijui viongozi wetu wanauwezo kweli wa kufikiri au la? Si angemuuliza hata katibu wa bunge basi kama hawezi kufanya maamuzi.
 
Huyu mama anaelekea pabaya kabisa? kafanya kama bunge ni NGO yake na familia yake, kazi yake ni kulazimisha hoja zake na dhaifu zikubalike. Nadhani sasa CUF wanaweza wakaanza kuona kuwa CCM sio rafiki ila ni mnyama.
 
hata wambunge wa CCM hawazidi kumi ukiondoa wanao unda sirikali. Huyo naibu waziri anatoa majibu ya hoja kama hajui kusoma!

hivi lini mtakuwa? Kwa masuala kama haya acheni kuchangia kiushabiki wakuu, tuhabarisheni juu ya hiyo meli madhara yaliyotokea na kinachojiri bungeni.
 
Hali hii haikubaliki kamwe kwani kama angekufa mbunge mmoja tuu Bunge lote lingeahirishwa ila wanakufa wananchi zaidi ya 200 bunge linaendelea kupitisha bajeti kwa ajili ya nani? Spika hapa kapotoka na hii ni dalili ya wazi kuwa CCM haipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi bali wao.
 
mama mbona anashindwa kupima upepo ?

Huyu mama ni janga la kimataifa, anaendesha bunge kama shirika lake la misaada..sijui kama tutafika kwa mwendo huu, na wabunge wanamchekea sana huyu mama, na hawa wabunge wa vyama vingine watambue kuwa CHADEMA na wabunge wake wanapokuwa wanapigania haki pale bungeni uwa hawafanyi utani yule mama ni tatizo.
 
Back
Top Bottom