Hali halisi tunayoiona leo ni matokeo ya viongozi wa aina hii ambao hawana uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi kulingana na hali halisi ya wakati huo. Utamaduni uliojengeka miaka mingi umewafanya wasijiamini kutumia akili zao wenyewe kutoa maamuzi halali kutokana tu na hofu ya mamlaka zilizo juu yake. Matatizo haya ya kutojiamini yanaambatana nao hata pale wanapofika kwenye nafasi za juu kabisa kama urais, uspika na ujaji mkuu na matokeo yake jamii inaanza kuyumba, misingi ya maadili inamomonyoka na hata machafuko huweza kutokea! Hata kama hakuna mamlaka nyingine juu yao katika nchi zao, hofu inahamia nje ya nchi kwa mataifa makubwa au mashirika ya kimataifa!
Mara nyingi watu wenye mawazo huru, wanaojiamini hutofautiana na viongozi wa aina hii na wanawaona kama wapinzani au watu hao kujiunga na upinzani rasmi kisiasa. Hata hivyo utamaduni huu upo ukingoni kwani kizazi kilichoathirika zaidi ni kile cha waliozaliwa kabla ya miaka ya 1970! Inawezekana kabisa kwamba hali hiyo ina mizizi yake kwenye ukoloni.