Madaktari waanza kuikimbia nchi..

Madaktari waanza kuikimbia nchi..

JAMANI WAAACHENI WAENDEEEE, HUENDA HII DHAHAMA YA KUTISHANA YA KITOTO KABISA ITAISHA
Mimi nakubali kabisa hawa madaktari walikuwa hawanisaidii ntabaki natibiwa hata na Manesi au MaMedical ambao walipita huko JKT wanaujua Uzalendo, hao wanaojidanganya eti ataenda Botswana wakati Leseni yake imefutwa ni uongo Mtupu hawatapokelewa,
  • Kwanza ni lazima Ubalozi wetu uwachuje,
  • Pili Nchi za wenzetu huwezi kumgusa Raia wao na kumuandikia sindano wakati huna Leseni toka nchi uliosomea au cheti cha Chuo husika
  • Hao Madaktari tuwaombee safari njema kuna kazi nyingi tu huko hata km si za Udaktari wakafanye
  • Ni kweli walikuwa sio wazalendo maana walitaka kujipima na wabunge, hivi na Wahasibu Mainjinia wanajeshi, Polisi wanasheria nao wafanye hivyo?
  • Acheni waende wametumwa hao tutawasiliana nao humuhumu JF wakitutukana lakini msg send na picha imefika THE END tusubiri mgomo wa wengine, Wakulima
Na ukisikia wamepata kazi utajinyonga?????dua la kuku halimpati mwewe, wao acha wabaki na hizo leseni unafikiri wewe ndio unajua kuliko wao????kalaga baho.
 
Wameboresha posho ya kuchunguza maiti kua 100,000/= wakati posho ya kufanya kazi masaa 24 ni 20,000/= SASA KAMA UNA AKILI UNATAKIWA UTAFAKARI

Ina maana serikali yetu inajali maiti kuliko walio hai.. inabidi madaktari watuue zaidi ili wapate posho nono ya kuchunguza maiti..

Tafakari na uchukue hatua
 
Ugomvi sasa ni sisi (wananchi) na serikali yetu; madaktari hawa ni kweli wanatakiwa kila mahali tusijidanganye, tukomae kuiambia serikali yetu kwamba kuwa na madaktari wanaolipwa na kufanya kazi sawasawa ni haki yetu na priority ya taifa hili. Mkijua priority zinazowekwa.....kusafiri nje ya nchi, kujenga Kigamboni city, kununua furniture, kutenga mamilioni ya chai ofisini.....wananchi wenzangu tugombane na serikali siyo madaktari haitatusaidia...tutawakosa madaktari na majamaa (wanasiasa/watawala) wataendelea kwenda India na ujeruman kutibiwa
 
Kufuatia mgomo wa madaktari wa hivi majuzi pamoja na uamuzi wa kuwafutia leseni baadhi ya madaktari waliogoma, wimbi la madaktari wameamua kukimbia nchi na kwenda kufanya kazi nje ya nchi...Habari zenye uhakika kutoka katika baadhi ya balozi za nchi wanachama wa SADC hapa mjini dar es salaam zinasema kumekua na wimbi la madaktari kukimbilia nchi za Namibia, Zimbabwe, South Africa, Botswana, Lesotho na Swaziland. ambako maslahi ni mazuri tofauti na huku kwetu bongo..

Mpaka sasa idadi rasmi ya madaktari waliokimbia ni 50 lakini inavyoelekea idadi ni kubwa zaidi ya hii kwani wapo wengi mno wanaoondoka kimya kimya bila taarifa.

"exodus of medical specialists has peaked over the past week in response to what the professionals see as the arrogance and vindictiveness of senior state officials." says The Tanzania Medical Association

" we pleaded with the doctors not to leave due to the invaluable services they offered. But the doctors said it was the only alternative given the government was in no hurry to resolve the situation" said Namala Mkopi, president of the Medical Association of Tanzania

Katika hatua nyingine serikali imeamua kutenga sh billion 200 kama gharama ya kuleta madaktari wa dharura huku gharama ya kumsomesha daktari mmoja kwa miaka mitano inakadiriwa kufikia millioni 100

SOURCE: gazeti la The EastAfrican

MY TAKE:
kuingiza siasa kwenye mambo ya taaluma na kutunishiana misuli kunakofanywa na WAKUBWA kutaiathiri sana hii nchi
serikali imemwaga mboga wao wamemwaga ugali...



Bora tujue hatuna madaktari kuliko kuwa na madaktari maslahi kama hawa, ni bora waondoke na watauchie nchi yetu.
 
Mkuu wakumbushe tu kuwa 2015 wasiache kuja kupiga kura na familia zao. Waakikishe wana nauli za kuja kuondoa serikali ya magamba maana wapopiga kura itakuwa balaa kwao na kwetu pia
 
Too much politics has maimed the nation and thereby stopped its development in more than one form.
 
Muhimbili Ina daktari wa upasuaji wa watoto mmoja tu.
Kutokana na manyanyaso ya SERIKALI kwenye mgomo huu wiki iliyopita katangaza kuacha kazi Muhimbili.
Inachukua si chini ya miaka 12 kama utabahatika kusoma moja Kwa moja bila kusimama baada ya kumaliza form six kuwa paediatric surgeon.
Watoto wenye matatizo mbalimbali waliokuwa kwenye list ya kufanyiwa upasuaji hawatapata hiyo huduma labda hao wanasiasa waje wawafanyie hao wagonjwa operesheni. Bahati mbaya hata wakienda kutafuta nje paediatric surgeon ni wachache sana.

Kwahiyo unachotaka kusema hapo kwa red ni nini? jaribu kuheshimu na taaluma za wengine mkuu! don't see yourself exceptional bana!
 
madai yalikuwa 8,hayo mengine wameongeza kina mwinyi na wenzao. Hivi wewe, kupunguza viongozi kwenda nje ilid fedha ziboreshwe haikusaidii? Nyumba ya daktari ikiwa karibu na hosp ili asichelewe haikusaidii? Daktari akiwezeshwa vizuri ili akuhudumie with full conc haikusaidii? After all kila mtu atapigania haki yake.

Kwahiyo usipopewa haya au yasipofanyika dawa yake ni kugoma? shida yenu hamna uzalendo na watanzania wenzenu
 
Mkuu, hivi unadhani tuna watu wenye akili humo serikalini??

tiba si sawa na ufundi mwingine wowote.... daktari hawezi kutibu bila kuwasiliana directly na mgojwa na ndio maana kila nchi inalinda madaktari wake, na kama inapokea wageni basi lzima wasome, wafanye mitihani na wafaulu. In the US alone dr anaweza kufaulu clinicals na akafeli TOEFL hata kwa miaka mitatu na kuendelea... Lengo ni kuweza kuwasiliana vyema na wateja/wagonjwa

hata wanaotibu wanyama, huwasiliana na wanyama hao kabla ya kutibu vizuri, ni utaalam maalum

Leo ukileta Dr. toka iran utawasiliana vipi?? ukiweka mkalimani, ile privacy ya mgonjwa inakua wapi??? what about "lost in translation"?

OUR GOVERNMENT IS FAILING HERSELF, HAKUNA VIAPO MTU KUWA KARANI, LAKINI KUNA VIAPO MTU KUWA DAKTARI!!! SASA UNAPOWACHUKULIA WALIOAPA POA, BASI NA WANAKUONA DADA POA TU, AND THAT IS WHERE OUR GOVERNMENT IS RIGHT NOW

THE WRITINGS ARE ON THE WALL.... AND GUESS WHAT, IT ISNT PRETTY
Umenena vema sana,ni kwa vile wale wasioelewa hili,naamini wana nta masikioni.
 
sion kama kuna ubaya kama madai ya vifaa yamejitokeza mara moja,,,,,,,hakuna asotaka maisha mazuri bhana,,,,waache wapigane nao waishi kama wanavoishi wezi halali(wanasiasa)

Kwahiyo wewe unasapoti ndg zetu wafe kisa madaktari wanataka maslahi mazuri, tena yasio realistic!!!
 
THEY CAN JUST AS WELL ,DO US A FAVOUR BY DROPING DEAD,FOR ALL I CARE.....Waache waende zao huko,wakabebe zege.........TO HELL WITH THEM........Hapa heshima ya mtu,itatokana na huduma yake kwa jamii.


Tutajisomea wenyewe notisi hizi na zile,afu Tutajitibu wenyewe .........kama atakosekana daktari mmoja mzalendo atakayebakia kututibu tutakapokuwa gonjwa ! ...........
 
[Kiongozi, sio maslahi tu. Sijui kwanini wanasiasa wanataka kushikilia hapo kwenye maslahi? Hawataki kabisa kusema madai mengine!]

Jibu la swali lako hapo kwa red ni hili hapa
Madai 12 ya madaktari wetu ni haya yafuatayo:
1. Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3. Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5. Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6. Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7. Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8. Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9. Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10. Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11. Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12. Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.

NB: Kwa madai haya maana yake ni kwamba daktari anayeanza kazi anatakiwa alipwe shilingi 7,700,000/=.
 
unahitaji kutafuta maana ya daktari kwanza.
Mkuu unalo jibu sema maana nimesoma hoja ya mtoa mada ili nipate kuelewa tunazungumzia watu gani.
Katika hatua nyingine serikali imeamua kutenga sh billion 200 kama gharama ya kuleta madaktari wa dharura huku gharama ya kumsomesha daktari mmoja kwa miaka mitano inakadiriwa kufikia millioni 100

 
Mkuu, hivi unadhani tuna watu wenye akili humo serikalini??

tiba si sawa na ufundi mwingine wowote.... daktari hawezi kutibu bila kuwasiliana directly na mgojwa na ndio maana kila nchi inalinda madaktari wake, na kama inapokea wageni basi lzima wasome, wafanye mitihani na wafaulu. In the US alone dr anaweza kufaulu clinicals na akafeli TOEFL hata kwa miaka mitatu na kuendelea... Lengo ni kuweza kuwasiliana vyema na wateja/wagonjwa

hata wanaotibu wanyama, huwasiliana na wanyama hao kabla ya kutibu vizuri, ni utaalam maalum

Leo ukileta Dr. toka iran utawasiliana vipi?? ukiweka mkalimani, ile privacy ya mgonjwa inakua wapi??? what about "lost in translation"?

OUR GOVERNMENT IS FAILING HERSELF, HAKUNA VIAPO MTU KUWA KARANI, LAKINI KUNA VIAPO MTU KUWA DAKTARI!!! SASA UNAPOWACHUKULIA WALIOAPA POA, BASI NA WANAKUONA DADA POA TU, AND THAT IS WHERE OUR GOVERNMENT IS RIGHT NOW

THE WRITINGS ARE ON THE WALL.... AND GUESS WHAT, IT ISNT PRETTY
Umesema ukweli mtupu lakini sasa hawa wanaondoka sii nao watakutana na matatizo hayo hayo huko wanakokwenda kama ya Wairan kuja hapa?. Kwa nini tumwapongeze hawa wanaoondoka kwa kufuata malipo bora zaidi lakini tunawakashifu wale wanaokuja kwa Uzalendo wao kuponya watu ktk mazingira magumu zaidi!..

Jamani serikali yetu imeshindwa kutuletea maisha bora na hali hii ipo kwa kila mfanyakazi nchini toka huyo Karani unayemsema hakufanya kiapo lakini ana umuhimu wake sana tu kwa sababu huwezi kumwona Daktari utibiwe bila kupitia kwa karani, akiondoka huyu Karani sidhani kama daktari ataweza kazi zote..Tunahitajiana sote hakuna mbora zaidi, na swala la mishahara bora nchini ni janga la watumishi wote wa serikali...
 
Umbea wa magazeti. Mlitaka wafanye nini kama nyie hamwahitaji?
 
Mwenyezi mungu amesikia kilio cha wanyonge, madaktari wakatili hao ametuepushia. Waende huko wakajiuze.

Hii njema wacha wakatafute na wachache watakao baki watuhudumie. Tunateseka na kuumia kwa maradhi walalahoi kwani idadi kubwa ya ma dk hawatoi huduma yoyote bora tujue hawapo.
 
Back
Top Bottom