Madaktari wa China waendelea kuwa sehemu muhimu ya mkakati wa Afya wa Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
81e042fedee04f4f945aeaf9d7682ff7.jpeg


4840374fd4e9467eb6495ce82e73b1c7.jpeg


Mwezi Oktoba mwaka huu timu ya madaktari bingwa 11 kutoka China iliwasili mkoani Kigoma, ambako ilitoa huduma za matibabu kwa wenyeji wa huko kwa muda wa siku tano, ikiwa ni pamoja na huduma za ushauri wa kimatibabu na upasuaji. Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian aliyehudhuria hafla ya kukaribishwa kwa madaktari hao mkoani Kigoma amesema madaktari hao wanaendeleza utamaduni ambao umekuwepo tangu mwaka 1968, China ilipoanza kutuma madaktari wake nchini Tanzania. Tangu wakati huo hadi sasa, madaktari hao wameweza kutibu jumla ya wagonjwa milioni 20, wa bara na visiwani.

Ushirikiano kwenye sekta ya matibabu kati ya China na Tanzania, ni jambo linalofahamika kwa watanzania wengi wa maeneo ambayo madaktari wa China wanatoa huduma, maeneo ambayo madaktari hao wanaweka kambi za muda kutoa huduma, au wale waliowahi kubahatika kutibiwa na madaktari wa meli wa madaktari wa jeshi la China (China Peace Ark) ambayo hutembelewa maeneo mbalimbali ya Afrika.

Mara nyingi ushirikiano kwenye sekta ya matibabu kati ya China na Tanzania, au China na Afrika kwa ujumla, huwa unaangalia mambo makubwa zaidi, kama vile msaada inaotoa China katika kujenga hospitali, msaada wa vifaa tiba, au msaada inaotoa China katika kutoa mafunzo kwa madaktari wa nchi za Afrika. Lakini mchango unaotolewa na vikundi vya matibabu vinavyoweka kambi katika maeneo ya mbali na yenye watu wenye hali duni huwa haitajwi sana, ni mchango huo ambao kwa kiasi fulani unaoonesha moyo wa udaktari wa madaktari wa China wa kuweza kufanya kazi katika mazingira magumu kuwahudumia watu maskini. Ni moyo huohuo pia unaonyesha hali ya urafiki kati ya China na Tanzania, au China na nchi nyingine za Afrika zinazopokea vikundi vya madaktari kutoka China.

Pamoja na kuwa sekta ya afya katika nchi nyingi za Afrika imekuwa inapiga hatua mwaka hadi mwaka, kweli unabaki kuwa maeneo mengi sana ya nchi za Afrika hayana huduma za kisasa za afya. Tukichukulia mfano wa Tanzania, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO, uwiano kati ya daktari na mgonjwa ni 1:20,000, hii ni tofauti na kiwango kinachopendekezwa na shirika hilo cha 1:300. Na pia ni mbali sana na lengo la Tanzania la japo 1:8000. Kwa hiyo ni jambo la kawaida kusikia watu wakisumbuliwa au hata kupoteza maisha yao kutokana na magonjwa yanayoweza kutibika.

Umaalum wa kipekee wa vikundi vya madaktari wa China vinavyokwenda katika maeneo hayo ni kuwa kwanza vinakuwa na madaktari bingwa kwa maeneo mbalimbali, pili vinakuwa na zana za kisasa ambazo mara nyingi zinakuwa hazipatikani katika maeneo wanayokwenda ambako hata kama wenyeji wanaweza kumudu gharama za kutumia zana hizo hawawezi kupata huduma yake, na tatu ambalo pia ni muhimu zaidi ni kuwa wanaopewa huduma hawalipi chochote.

Madaktari huwa wanasema kama mtu ana ugonjwa fulani, jambo la busara ni kuhakikisha ugonjwa huo unatibiwa mapema, lakini kama ugonjwa haugunduliwi mapema kunakuwa hakuna uwezekano wa kutibu mapema. Kupitia huduma zinazotolewa na madaktari kama hawa, watu mbalimbali wameweza kugundua matatizo yao na kuweza kupata matibabu, wengine ambayo huenda wangeishia kuwa vipofu wameweza kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho, wamepata matibabu na kuepusha hatari.
 
Wapo kazini hao waache waendelee kutoa msaada mataifa makubwa yametuzidi maarifa aisee umaskini kitu kibaya tajiri anakuambia anataka kukusaidia kupaka nyumba yako rangi Ila kwa kutumia fundi wake.
 
Back
Top Bottom