VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Madaktari waliorudi kazini hivi karibuni wanaandaa mgomo mwingine mkubwa.Mgomo huo uliopachikwa jina la 'Mgomo wa Ukombozi na Hadhi' uunapanga kuishinikiza Serikali kuacha maramoja kutumia fedha za walalahoi-watanzania kwa kuwasafirisha nje ya nchi viongozi kwa ajili ya matibabu hata ya magonjwa yanayotibika nchini.Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,kitendo hicho ni dharau kwa tasnia nzima ya utabibu nchini Tanzania.Wengine wameongeza kuwa kutokana na viongozi karibu wote kupata matibabu nje ya nchi,hata mgomo wa awali ulipuuzwa kwakuwa viongozi hawaathiriki kwa lolote.Madaktari wanahitaji mabadiliko.Matumizi yasiyo ya lazima pamoja na dharau ziepukwe.Serikali na isikie,isipuuze...
Nitafuatilia suala hili na kubandika uzi hapa soon..Mkikutana msisahau kuwaongelea akina Blandina Nyoni ambao tunaambiwa bado wako ofisini wakiendelea kusaini dokomenti!
Mbona ni madaktari hao hao ndio huwa wana-recommend watu wa kupelekwa nje kwa matibabu zaidi?
Waache usanii bana!
ukweli mtupu.Mbona ni madaktari hao hao ndio huwa wana-recommend watu wa kupelekwa nje kwa matibabu zaidi?
Waache usanii bana!
Nitafuatilia suala hili na kubandika uzi hapa soon..
...[madaktari waliorudi kazini hivi karibuni wanaandaa mgomo mwingine mkubwa.mgomo huo uliopachikwa jina la 'mgomo wa ukombozi na hadhi' uunapanga kuishinikiza serikali kuacha maramoja kutumia fedha za walalahoi-watanzania kwa kuwasafirisha nje ya nchi viongozi kwa ajili ya matibabu hata ya magonjwa yanayotibika nchini.kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,kitendo hicho ni dharau kwa tasnia nzima ya utabibu nchini tanzania.wengine wameongeza kuwa kutokana na viongozi karibu wote kupata matibabu nje ya nchi,hata mgomo wa awali ulipuuzwa kwakuwa viongozi hawaathiriki kwa lolote.madaktari wanahitaji mabadiliko.matumizi yasiyo ya lazima pamoja na dharau ziepukwe.serikali na isikie,isipuuze]
acha uzushi, hakuna kitu kama hicho, kama uko makini utaona kwamba mojawapo ya madai ya mgomo uliopita ilikuwa ni kuishinikiza serikali kuacha kupeleka wakubwa kutibiwa india bila kufuata taratibu zilizowekwa yaani ugonjwa ushindikane kutibiwa nchini, hili lithibitishwe na madaktari bingwa wasiopungua watatu!
Acha upotoshaji vuta-nikuvute
Ikiwa kweli nikutafute?
Unitafute ili iweje?? Nna wasiwasi we umetumwa humu kwa ajenda zako za siri...Get lost!