Mkakati mpya mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkakati mpya mgomo wa Madaktari

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Mar 8, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Serikali inaandaa mkakati wa chini kwa chini wa kuzimisha kabisa mgomo wowote wa watumishi wa umma na kwa kuanzia itakuwa kwa huu unaoendelea wa madaktari, taarifa za kiinteligensia zimetonya.

  Hii inafuatia kitendo cha Madaktari kuendelea kuishinikiza Serikali kuwaondoa madarakani wateule wa Mhe. Rais yaani Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (Dr, Haji Mponda) na Naibu wake( Lucy Nkya
  ).

  Taarifa za kuaminika zinabainisha kuwa ilipofikia sasa, Serikali imeona kuwa kitendo cha madaktari kushinikiza kuondolewa kwa Wasimamizi hao wa Wizara kunaweza kupelekea madaktari hao kuja kushinikiza kuletewa Waziri na Naibu wanayemtaka wao na sio wa chaguo la Mhe,. Rais (hii ni dharau kubwa!!) Aidha, kwa upande mwingine, Serikali inaona kuwa itadharaurika kwa kusalimu amri iwapo itatekeleza matakwa wa madaktari kwa asilimia mia moja. Serikali pia inaamini kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa imefungua migomo isiyoisha kwa watumishi wa umma hasa walio katika Sekta nyeti ikiwemo,. Afya na Elimu. Pia, Serikali imeona kuwa, upo uwezekano mkubwa kwa madaktari kuishia kugoma mara kwa mara kushinikiza madai yeyote wanaodhani yanafaa..

  "....Hii nchi kila mtumishi wa umma pasipo kujali taaluma ana umuhimu wake kwenye kazi anayofanya, leo kwa nini tuwajali zaidi madaktari...Walitaka Katibu Mkuu na mganga Mkuu waondolewe, tumewaondoa..sasa wanataka Waziri na Naibu wake... hivi tusipokuwa makini katika kushughulikia hili, ipo siku hawa madaktari wanaweza kutaka Mhe. Rais nae ajiuzuru..ikifikia hapo tutafanyaje, si itaonekana nchi imetushinda...potelea mbali??" alisikia akibainisha mmoja wa viongozi wa juu katika wa Serikali alipokuwa akieleza mkakati unaochukuliwa kusambaratisha mgomo wa madaktari..

  Haifahamiki miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa ni nini katika kumaliza mgomo huo lakini zinaweza kuhusisha kuwashughulikia viongozi wa juu wa mgomo huo, kuzuia vyombo vya habari visitoe taarifa na kuweka taratibu mpya za kiutumishi katika hospitali za umma ili kuwabana madaktari wasifanye mgomo baridi, pia kuwahamisha baadhi ya vinara wa mgomo kutoka kituo kimoja kwenda kingine....

   
Loading...