Kuhusu mgomo wa madaktari: John Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu mgomo wa madaktari: John Mnyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Jan 27, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  [h=2]Friday, January 27, 2012[/h][h=3]KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI[/h]

  Mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa umedhihirisha kwamba tuna serikali dhaifu yenye ombwe la uongozi. Haiwezekani wananchi wakawa wanakufa kwa kukosa matibabu stahiki na wengine wakipata madhara kutokana na kuchelewa kupata matibabu sababu ya mgomo wa madaktari halafu viongozi wenye dhamana hawachukui hatua sahihi.


  Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.

  Kwa upande wetu CHADEMA tulitoa kauli tarehe 25 Januari 2012 ya kutaka serikali ichukue hatua na tuliona tuipe serikali nafasi ifanye kazi yake hata hivyo serikali haionyeshi kuupa uzito unaostahili mgogoro huu wenye kuathiri hali za wagonjwa na maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

  Tuliacha kwenda katika eneo la mgomo kukutana na madaktari katika siku za awali kuepusha suala hili kutafsiriwa kuwa ni la kisiasa. Hata hivyo, kuchelewa kwa serikali kukutana na madaktari kunahitaji hatua za pamoja. Dhamira yangu kama mwananchi, mbunge katika mkoa wa Dar es salaam na kiongozi wa chama cha siasa naumizwa na hali inayoendelea. Ni vigumu kuweza kuendelea na majukumu ya kibunge na ya kichama katika masuala mengine wakati serikali iko legelege katika suala ambalo linahusu uhai wa wananchi wenzangu uko mashakani.

  Hivyo nawajibika siku ya leo kuelekeza nguvu katika kuungana mkono na madaktari katika madai yao ili kuishinikiza serikali kuweza kutuma ujumbe mkubwa kukutana na madaktari leo au kesho. Na iwapo serikali haitakutana nao katika muda huo, itabidi uongozi wa kambi ya upinzani bungeni ukiwa ni serikali kivuli na uongozi mkuu wa CHADEMA ukiwa ni chama mbadala kuweza kukutana nao.

  Natambua kwamba uzembe na ufisadi katika serikali kwenye sekta ya afya unaligharimu taifa na maisha ya wananchi. Hivyo, CHADEMA inaitaka serikali kukamilisha kwa haraka majadiliano na madaktari na kutimiza madai yao ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

  Nawapa pole wananchi ambao wameathirika na migomo inayoendelea na kuzingatia kwamba mgomo huo umesababishwa na udhaifu katika serikali.

  Natoa mwito kwa umma wa watanzania kuwaunga mkono madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika hospitali na zahanati za umma kama sehemu ya kuboresha huduma katika maeneo husika.

  Madai ya madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini yasiposhughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu watumishi husika wanaweza wasiwe kwenye mgomo wa wazi kama ilivyo kwa baadhi ya hospitali na zahanati nchini lakini wataendelea na migomo baridi kwa kutoa huduma mbovu au kuacha kazi kwenye maeneo ya umma na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi wakati kukiwa na uhaba wa watumishi nchini.

  Aidha, pamoja na migomo inayoendelea, naendelea kutoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.

  Nimezungumza na viongozi wetu wakuu kuhusu suala hili na natoa mwito kwa wadau wote kuunganisha nguvu katika kuisimamia serikali kushughulikia madai ya madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya kwa haraka ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

  Wananchi wenzangu wa Jimbo la Ubungo na umma kwa ujumla uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.

  Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.

  Ni imani yangu kwamba serikali ikiwa na dhamira inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko. Hii ni pamoja kuwezesha malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.

  Kwa sababu hii, leo sitashiriki kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kinachoendelea ili kupata wasaa wa kufuatilia kwa karibu suala hili na kuwasiliana na viongozi wenzangu kwa ajili ya hatua zaidi za pamoja.

  Wenu katika utumishi wa umma,  John Mnyika (Mb)
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mchango mzuri Mnyika lakini nilitegema waziri kivuli wa Afya aitoe hii statement. CHADEMA jitahidini kwenye safu ya 'shadow cabinet' Waziri wa serikali iliyo madakarani akifanya/asipofanya jambo ni vema tena kwa haraka sana Waziri kivuli akasema CHADEMA wangefanya nini tofauti? Sasa Waziri kivuli yuko wapi?
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Nashanga!!! Waziri kivuli wa Afya ni nani vile?
   
 4. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mwanzo mzuri, ila wasiwasi wangu ni kwamba chadema wakienda hapo serikari watasema mgomo huo ni wa kisiasa, wakati najua kabisa yawezekana mpaka sasa hawajui waanzie wapi kumaliza hilo tatizo maana walidhani madaktari watabeep kama walivyozoea kwa walimu.
   
 5. m

  mwikumwiku Senior Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu umetowa changamoto nzuri sana! Wasi wasi wangu humu ndani watakuita wewe ni gamba! Hata hivyo ukweli utabaki pale pale! Pamoja na dhamira "nzuri" ya CHADEMA kujaribu kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa warafi wachache, bado chama hiki kinaupungufu watu wenye uzoefu wa kuendesha serikali!

  Wakati huu wa mgomo wa madaktari ambapo waziri wa afya na timu yake wameudhihirishia umma kwamba hawana uwezo wakuongoza wizara tulitegemea kuona waziri kivuli akitueleza yeye na seikali yake ya chadema wangefanya nini kutatua mgogoro huu! Badala yake tamko linatolewa na kiongozi wa chama!!
   
 6. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni Dr Mbassa, mbunge wa CDM jimbo la Biharamulo lakini nahisi hana uelewa wa kutosha
   
 7. mpiganaji jm

  mpiganaji jm Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  That y cdm inatakiwakuongoza nchi hii cz hawa ccm wamechemka, madaktari wanagoma baba riz anasurvey nchi za mbali
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Songa mbele kijana pamoja naviongozi wenzako mhakikishe hawa serikali wanatimiza wjibu wao...
   
 9. D

  DOMA JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ****** yupo angani ama kweli cdm chapeni kazi tutafika tu.
   
 10. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Alie post ni Osokoni lakini mwisho jina la John Mnyika,hapo sielewi kidogo.
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sasa kutoenda kwenye kikao ndio umesaidia nn ? au ndio kujijenga kisiasa?
   
 12. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Wengi wa wananchi wa Pwani si VILAZA kama wewe........................ Pole!!!!
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Sauti kutoka nyikani? ikiletwa kwenu na John nyika.... pole pole baba ni rahisi kupiga chenga za midadi ukiwa nje ya uwanja.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  Sawa nimesoma na nimejaribu kukuelewa,
  lakini serikali yetu haiko serious na mambo ambayo
  yanaweza kuleta majanga ya kitaifa kama hili la mgomo wa madaktari,
  mimi pia naungana na madaktari, acha wagome mpaka kieleweke.

  Mnyika nakupa big up sana kwa kututengenezea barabara za
  kule uswazi kwetu - mbezi mwisho.

  Kwa kweli umefanya kazi inayosomeka.
  Sasa kuna wale waliojenga fence zao zinafanya greda
  lishindwe kuchonga barabara, nakuomba mkuu uwe sambamba nao
  kwa maana hili likitoka litakuwa limetoka.

  Big up mkuu.
   
 15. d

  davidie JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani cdm pamoja na uwezo wao wa kuyaona hayo mapungufu lakini wakitoa njia mmbadala ya kutatua tatizo utaambiwa wamechochea mgomo. Na hii ni dalili ya woga wa magamba
   
 16. d

  davidie JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIO KILA ALIAE KWENYE MSIBA ANAUCHUNGU NA MAREHEMU:lol:
   
 17. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  updates: kikaoni mawaziri mponda,ghasia,nkya pia nyoni na mtasiwa wapo kikaoni. Mwenyekiti anawasomea madai ya madaktari. Pinda amekwepa.!
   
 18. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu, namwangalia waziri hapa, hajielewi elewi..... Ujumbe ni kwa waziri mkuu,
   
 19. D

  Deo JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yes, huo ni uchaguzi sahihi wa vipau mbele. Huna haja ya kushiriki vikao wakati wananchi na hasa wagonjwa wakihangaika bila kujua hatima yao. Keep it up young man
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kila kitu Rais jamani hivi nchi hii hatuwezi kuwawajibisha hata wale ambao Rais akiwa safarini na wao wanalala. Je Tutafika
   
Loading...