Tamko la Chama cha Madaktari Tanzania kuhusu mgomo wa intern Doctors

Dec 5, 2011
78
93
Namala Mkopi ▶ Medical Association of Tanzania
04/01/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KUHUSU SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI WANAOFANYA KAZI CHINI YA USIMAMIZI (INTERN DOCTORS).

CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA KIMESIKITISHWA SANA NA MGOGORO NA MIGOMO INAYOENDELEA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI NCHINI KWA MADAKTARI WANAOFANYA KAZI CHINI YA USIMAMIZI YAANI “INTERNS”.
TATIZO KUBWA NI KWAMBA SERIKALI HAIJAWALIPA MALIPO YAO KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA HADI MITATU HALI AMBAYO IMEWAFANYA WASHINDWE KUENDELEA NA KAZI YAO YA KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA WASIOKUWA NA HATIA

IKUMBUKWE KWAMBA MADAKTARI HAWA WALIO CHINI YA UANGALIZI NDIYO UTI WA MGONGO WA UTOAJI HUDUMA KATIKA HOSPITALI WANAZOFANYA KAZI HASA IKICHUKULIWA KUWA WAO NDIO WA KWANZA KUMWONA MGONJWA NA KUMPA MATIBABU KABLA YA KUONWA NA MADAKTARI BINGWA WALIO WACHACHE.

HIVYO KUTOKUWEPO KWAO KAZINI KUNAFANYA UTOAJI WAHUDUMA KWA WANANCHI KUDORORA KATIKA HOSPITALI HUSIKA.

BAADA YA KUFANYA UTAFITI WA KINA, CHAMA KIMEBAINI KUWA HOSPITALI TANO ZA RUFAA NCHINI TAYARI MADAKTARI HAWA WAMESHINDWA KUFANYA KAZI ZIKIWEMO

1. HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
2. HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO
3. HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA
4. HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA
5. HOSPITALI YA MANISPAA YA TEMEKE

KATIKA VITUO AMBAVYO MADAKTARI WAMEENDELEA KUFANYA KAZI, IMEBAINIKA KUWA NI KUTOKANA NA VITUO, HOSPITALI AU HALMASHAURI HUSIKA KUAMUA KUWAKOPESHA WATAALAM HAO ILI KUWAWEZESHA WATAALAM HAO KUWEZA KUENDELEA NA MAISHA YAO YA KILA SIKU HUKU WAKITOA HUDUMA WAKATI UFUATILIAJI UKIENDELEA KWENYE SERIKALI KUU.

AIDHA CHAMA KIMEBAINI KUWA HALI HII INAENEA KATIKA HOSPITALI NYINGINE ZENYE MADAKTARI HAWA NA PIA INALETA MZIGO MKUBWA KWA WALE MADAKTARI MABINGWA NA WAANDAMIZI NA HII INAWEZA KULETA MGOGORO KATIKA FANI YOTE YA UDAKTARI NCHI NZIMA.

PIA CHAMA KINAKITAFSIRI KITENDO CHA KUTOWALIPA MADAKTARI MALIPO YAO NA KUWAFANYA WAISHI KWA SHIDA KWA MUDA HUO WOTE KUWA NI KITENDO CHA DHARAU KWA FANI YA UDAKTARI NA HUDUMA WANAZOTOA KWA WANANCHI. PIA NI UDHALILISHAJI WA HALI YA JUU KUWAACHA MADAKTARI WAISHI KWA KUOMBA OMBA HUKU WAKITOA HUDUMA KWA WANANCHI. PIA INATAFSIRIWA KUWA NI JINSI GANI SERIKALI ISIVYOJALI HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI INAOWAONGOZA.

KUTOKANA NA HAYO:

1. CHAMA KINALAANI KITENDO CHA SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUTOWALIPA MADAKTARI MALIPO YAO HALALI HADI KUFIKIA MGOMO UNAOPELEKEA WANANCHI KUKOSA HUDUMA STAHILI ZA MATIBABU

2. CHAMA KINAITAKA JAMII NA SERIKALI IELEWE WAZI KUWA MADAKTARI KUWEPO KAZINI BILA MALIPO KWA MUDA MREFU NI UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAM, KINYUME NA KIAPO CHA UDAKTARI NA INAPELEKEA UTOAJI WA HUDUMA HAFIFU NA VITENDO VYA UVUNJIFU WA SHERIA KAMA KUKARIBISHA MAZINGIRA YA RUSHWA.{SEHEMU YA KIAPO INAYOZUNGUMZIWA INASEMA HIVI “ ... WAKATI NIKIKISHIKA KIAPO HIKI NA IJALIWE KWANGU KUFURAHIA MAISHA NA KAZI YANGU, JAMII INIKUMBUKE NA KUNIHESHIMU NIKIWA HAI AU NIMEKUFA ...”

3. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUWALIPA MADAKTARI WOTE MALIPO YAO MARA MOJA NDANI YA KIPINDI CHA MASAA 48 ILI WAWEZE KUENDELEA KUFANYA KAZI YA KUWAHUDUMIA WATANZANIA

4. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUHESHIMU KAZI YA UDAKTARI NA HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI NA IEPUKE KUWA CHANZO CHA MIGOGORO YA MARA KWA MARA KATIKA SEKTA YA AFYA.

5. CHAMA KINAITAKA SERIKALI YAANI VIONGOZI WA WIZARA NA TAASISI KUACHA KUTUMIA LUGHA ZA VITISHO WAKATI TETE KAMA HUU HASA BAADA YA KUSHINDWA KUWALIPA MADAKTARI STAHILI ZAO

6. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUWA NA MIPANGO ENDELEVU NA YA MUDA MREFU KATIKA KULIPA STAHILI ZA WAFANYAKAZI ILI KUEPUKA KUFANYA KAZI KWA ZIMAMOTO KAMA INAVYOFANYA SASA

7. CHAMA KINAIALIKA WIZARA YA AFYA KUSHIRIKIANA NACHO KATIKA UTENDAJI WAKE ILI KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA KAMA HII INAYOPELEKEA MATESO KWA WANANCHI WASIO NA HATIA.

KWA KUMALIZIA, CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA(MAT) KINAPINGA UNYANYASAJI UNAOFANYWA NA WIZARA YA AFYA KWA WATAALAM WAKE, PIA CHAMA KINAONA WATAALAM HAWA HAWANA HATIA YA UVUNJIFU WA KIAPO CHAO KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WATANZANIA KUTOKANA NA SERIKALI KUTOKUTIMIZA WAJIBU WAKE KAMA INAVO ELEKEZA KWENYE KIAPO NA MAKUBALIANO YA KAZI.
CHAMA PIA KINASIKITISHWA NA MATOKEO YANAYOTOKANA NA MGOGORO HUU KWA WANANCHI WASIO NA HATIA NA TAIFA KWA JUMLA.
PIA CHAMA KINAZIPONGEZA HOSPITALI, NA HALMASHAURI ZOTE ZILIZOAMUA KUWAKOPESHA MADAKTARI MALIPO YAO ILI KUEPUSHA MIGOGORO ISIYOKUWA YA LAZIMA.

CHAMA KINAPENDA KUWEKA WAZI KWAMBA IWAPO WIZARA ITASHINDWA KUSHUGHULIKIA MALIPO HAYA NDANI YA SAA 48 BASI ITATULAZIMU KUITISHA MKUTANO WA DHARURA KWA MADAKTARI NCHINI ILI KUTAFAKARI MSTAKABALI WA JAMBO HILI NYETI NA YOTE YANAYOHUSU FANI YA UDAKTARI KATIKA TAIFA LETU.

IMETOLEWA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA

DR. NAMALA MKOPI
RAIS - MAT
 
WATAALAM!

Kazeni kamba na msikubali kuiachia. Mkilegeza tu, kwa ****** mtachekea chooni. Serikali inajali mambo ya anasa na kutojali mambo ya msingi kwa watanzania.

Angalia leo hii jioni karuka kwa ndege kwenda Korogwe Tanga kuzika kwa kutumia kodi za watanzania badala ya kutuma hata muwakilishi. Gharama hizo za kutumia ndege na huo msafara wa magari angalau ngarama zake zingeweza kupunguza angalau hata makali ya madeni ya aaaaaamaDaktari wawili watatu hivi.

Tanzania basi tena.
 
huo mgomo hauwahusu viongozi kwa sababu wao wanaenda kutibiwa india .kwa hiyo nyie wananchi mkiamua kufa kufeni who cares.
 
wazee haki haiji kwa mdebwedo kazeni kamba hawa waheshimiwa wao wanajiongezea tu posho rakini wezao hata ile kujikimu hawataki kuwapa mimi kama mzalendo nawaomba sana komaeni bila hivyo mtauwa wagojwa unaweza kufanya vitu vya ajabu kwa wagojwa chadema oheeeee :eyebrows:
 
Namala Mkopi ▶ Medical Association of Tanzania
04/01/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KUHUSU SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI WANAOFANYA KAZI CHINI YA USIMAMIZI (INTERN DOCTORS).

CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA KIMESIKITISHWA SANA NA MGOGORO NA MIGOMO INAYOENDELEA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI NCHINI KWA MADAKTARI WANAOFANYA KAZI CHINI YA USIMAMIZI YAANI “INTERNS”.
TATIZO KUBWA NI KWAMBA SERIKALI HAIJAWALIPA MALIPO YAO KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA HADI MITATU HALI AMBAYO IMEWAFANYA WASHINDWE KUENDELEA NA KAZI YAO YA KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA WASIOKUWA NA HATIA

IKUMBUKWE KWAMBA MADAKTARI HAWA WALIO CHINI YA UANGALIZI NDIYO UTI WA MGONGO WA UTOAJI HUDUMA KATIKA HOSPITALI WANAZOFANYA KAZI HASA IKICHUKULIWA KUWA WAO NDIO WA KWANZA KUMWONA MGONJWA NA KUMPA MATIBABU KABLA YA KUONWA NA MADAKTARI BINGWA WALIO WACHACHE.

HIVYO KUTOKUWEPO KWAO KAZINI KUNAFANYA UTOAJI WAHUDUMA KWA WANANCHI KUDORORA KATIKA HOSPITALI HUSIKA.

BAADA YA KUFANYA UTAFITI WA KINA, CHAMA KIMEBAINI KUWA HOSPITALI TANO ZA RUFAA NCHINI TAYARI MADAKTARI HAWA WAMESHINDWA KUFANYA KAZI ZIKIWEMO

1. HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
2. HOSPITALI YA MKOA WA TANGA BOMBO
3. HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA
4. HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA
5. HOSPITALI YA MANISPAA YA TEMEKE

KATIKA VITUO AMBAVYO MADAKTARI WAMEENDELEA KUFANYA KAZI, IMEBAINIKA KUWA NI KUTOKANA NA VITUO, HOSPITALI AU HALMASHAURI HUSIKA KUAMUA KUWAKOPESHA WATAALAM HAO ILI KUWAWEZESHA WATAALAM HAO KUWEZA KUENDELEA NA MAISHA YAO YA KILA SIKU HUKU WAKITOA HUDUMA WAKATI UFUATILIAJI UKIENDELEA KWENYE SERIKALI KUU.

AIDHA CHAMA KIMEBAINI KUWA HALI HII INAENEA KATIKA HOSPITALI NYINGINE ZENYE MADAKTARI HAWA NA PIA INALETA MZIGO MKUBWA KWA WALE MADAKTARI MABINGWA NA WAANDAMIZI NA HII INAWEZA KULETA MGOGORO KATIKA FANI YOTE YA UDAKTARI NCHI NZIMA.

PIA CHAMA KINAKITAFSIRI KITENDO CHA KUTOWALIPA MADAKTARI MALIPO YAO NA KUWAFANYA WAISHI KWA SHIDA KWA MUDA HUO WOTE KUWA NI KITENDO CHA DHARAU KWA FANI YA UDAKTARI NA HUDUMA WANAZOTOA KWA WANANCHI. PIA NI UDHALILISHAJI WA HALI YA JUU KUWAACHA MADAKTARI WAISHI KWA KUOMBA OMBA HUKU WAKITOA HUDUMA KWA WANANCHI. PIA INATAFSIRIWA KUWA NI JINSI GANI SERIKALI ISIVYOJALI HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI INAOWAONGOZA.

KUTOKANA NA HAYO:

1. CHAMA KINALAANI KITENDO CHA SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUTOWALIPA MADAKTARI MALIPO YAO HALALI HADI KUFIKIA MGOMO UNAOPELEKEA WANANCHI KUKOSA HUDUMA STAHILI ZA MATIBABU

2. CHAMA KINAITAKA JAMII NA SERIKALI IELEWE WAZI KUWA MADAKTARI KUWEPO KAZINI BILA MALIPO KWA MUDA MREFU NI UVUNJIFU WA HAKI ZA BINAADAM, KINYUME NA KIAPO CHA UDAKTARI NA INAPELEKEA UTOAJI WA HUDUMA HAFIFU NA VITENDO VYA UVUNJIFU WA SHERIA KAMA KUKARIBISHA MAZINGIRA YA RUSHWA.{SEHEMU YA KIAPO INAYOZUNGUMZIWA INASEMA HIVI “ ... WAKATI NIKIKISHIKA KIAPO HIKI NA IJALIWE KWANGU KUFURAHIA MAISHA NA KAZI YANGU, JAMII INIKUMBUKE NA KUNIHESHIMU NIKIWA HAI AU NIMEKUFA ...”

3. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUWALIPA MADAKTARI WOTE MALIPO YAO MARA MOJA NDANI YA KIPINDI CHA MASAA 48 ILI WAWEZE KUENDELEA KUFANYA KAZI YA KUWAHUDUMIA WATANZANIA

4. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUHESHIMU KAZI YA UDAKTARI NA HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI NA IEPUKE KUWA CHANZO CHA MIGOGORO YA MARA KWA MARA KATIKA SEKTA YA AFYA.

5. CHAMA KINAITAKA SERIKALI YAANI VIONGOZI WA WIZARA NA TAASISI KUACHA KUTUMIA LUGHA ZA VITISHO WAKATI TETE KAMA HUU HASA BAADA YA KUSHINDWA KUWALIPA MADAKTARI STAHILI ZAO

6. CHAMA KINAITAKA SERIKALI KUWA NA MIPANGO ENDELEVU NA YA MUDA MREFU KATIKA KULIPA STAHILI ZA WAFANYAKAZI ILI KUEPUKA KUFANYA KAZI KWA ZIMAMOTO KAMA INAVYOFANYA SASA

7. CHAMA KINAIALIKA WIZARA YA AFYA KUSHIRIKIANA NACHO KATIKA UTENDAJI WAKE ILI KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA KAMA HII INAYOPELEKEA MATESO KWA WANANCHI WASIO NA HATIA.

KWA KUMALIZIA, CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA(MAT) KINAPINGA UNYANYASAJI UNAOFANYWA NA WIZARA YA AFYA KWA WATAALAM WAKE, PIA CHAMA KINAONA WATAALAM HAWA HAWANA HATIA YA UVUNJIFU WA KIAPO CHAO KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WATANZANIA KUTOKANA NA SERIKALI KUTOKUTIMIZA WAJIBU WAKE KAMA INAVO ELEKEZA KWENYE KIAPO NA MAKUBALIANO YA KAZI.
CHAMA PIA KINASIKITISHWA NA MATOKEO YANAYOTOKANA NA MGOGORO HUU KWA WANANCHI WASIO NA HATIA NA TAIFA KWA JUMLA.
PIA CHAMA KINAZIPONGEZA HOSPITALI, NA HALMASHAURI ZOTE ZILIZOAMUA KUWAKOPESHA MADAKTARI MALIPO YAO ILI KUEPUSHA MIGOGORO ISIYOKUWA YA LAZIMA.

CHAMA KINAPENDA KUWEKA WAZI KWAMBA IWAPO WIZARA ITASHINDWA KUSHUGHULIKIA MALIPO HAYA NDANI YA SAA 48 BASI ITATULAZIMU KUITISHA MKUTANO WA DHARURA KWA MADAKTARI NCHINI ILI KUTAFAKARI MSTAKABALI WA JAMBO HILI NYETI NA YOTE YANAYOHUSU FANI YA UDAKTARI KATIKA TAIFA LETU.

IMETOLEWA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA

DR. NAMALA MKOPI
RAIS - MAT

Dah! Hawa jamaa mi nawakubali sana hawa kwani alwys wanaidhihirishia dunia kuwa wao 'facts' mbele siasa kuzimu. Migomo yao ni ya 'decade' lakini ikiwadia tu jua mshikemshike-ivi na sie wauza samaki hapa ferry hatuna chama chetu ili tutoe tamka la ultimatum-48hrs?
 
Dr Mkopi na Wenzako - Hongereni Sana. Tena nadhani Masaa 48 ni mengi sana. Mngewapa one hour tu, wangekubali. Kutokana na umuhimu wa chama chenu na hasa utaalaamu wenu, ninyi mngeweza kuwa mstari wa mbele kuilekebisha serikali hii. Watu wanafuja resources kwa maposho na makongamano, masafari yasiyoisha, madeal kama kazi serikalini, halafu leo, madaktari wanaowahudumia walalahoi, wanakashifiwa na kutukanwa na kunyanyaswa. Hembu chukueni hatua na Waalimu wafuatie tuone kama watatoa tena vitisho vyao hivyo. Hongereni tena.
 
Teh teh serikari yetu tangu lini ni sikivu. masaa 48 yataisha na hela hawatoi na bit watawapiga kesho.
 
Pesa ambazo mngelipwa zinagharamia safari za viongozi kwenda India kutibiwa
 
huu mgomo naunga mkono na waseme neno tu madktari wote tools down,mishahara midogo risk kibao
 
kwani hao madaktari wanoitwa chini ya uangalizi wanalipwa shilingi ngapi kwa mwezi?
 
shilingi elfu mbili tu, wewe mike tyson NgumiJiwe ukipigana mechi moja tu unaweza kuwalipa wote hao hadi kustaafu kwao pamoja na malipo ya uzeeni!! Magamba noooommmaaaaaa!!!
 
Asante sana Chama cha Madaktari Tanzania (MAT). Tumethubutu tunaweza tunasonga mbele. Naunga mkono tamko tena ikibidi nchi nzima tools down
 
ukiona mtu mzima, msomi anagoma usimuone mjinga, there is a sense in what he want! lesson nzuri sana kwa walimu!
 
Back
Top Bottom