Responded Madai ya Halmashauri Bukoba kuuza mchanga wa makaburi ya Kishenge, magari yapigwa marufuku kuingia eneo hilo

Responded Madai ya Halmashauri Bukoba kuuza mchanga wa makaburi ya Kishenge, magari yapigwa marufuku kuingia eneo hilo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa kuna baadhi ya Maafisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wamekuwa wakiuza mchanga eneo lililokuwa na makaburi ya Kishenge, Bukoba Mjini licha ya kuwa limetengwa kwa ajili ya uwekezaji, hatua zimechukuliwa na Mamlaka husika.

Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ Hii biashara ya Mchanga wa Makaburini eneo la Kishenge (Bukoba) ni Mradi wa Halmashauri?

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Renatus Mutatina amezungumzia suala hilo kwa kusema “Zoezi ambalo limekuwa likiendelea pale ni kuhamisha makaburi, hivyo kama kuna Maafisa wanaofanya hiyo biashara ya kuuza mchanga kwa siri sisi hatufahamu na tayari tumeanza kuchukua hatua.
photo_2026-01-10_12-46-25.jpg

photo_2026-01-10_16-59-32.jpg

Screenshot 2025-12-23 094804.jpg
Baada ya kupata hizo taarifa tulifika eneo husika kufanua ukaguzi na uamuzi uliochukuliwa kwanza kabisa tulizungumza na msimamizi wa zoezi la kuhamisha makaburi kuhusu taarifa hizo na pia tumepiga marufuku magari yote kuingia kwenye eneo hilo hata kama ni gari la Mkurugenzi.

Magari yote yatabaki nje na wahusika ndio watakaoingia ndani ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Zoezi la kuhamisha makaburi nalo litakamilika hivi karibuni kabla ya mradi kuanza.

Kuhusu hali ya eneo husika kwamba lipo katika hali mbaya, hapana, unapofanya zoezi la kuhamisha makabuni ni kawaida kutokea kwa mashimo lakini haijafika katika hali mbaya.
 
Back
Top Bottom