MADA YA WEEKEND: Wazee wa Dar na Benz la Mwinyi

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,976
2,000
Nani kakwambia huyo mzee hana uwezo wa kununua saloon ndogo? Acheni kushabikia misuses of public funds... Kwa faida yako soam tena acha kelele.
Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi, hupata mafao ya mkupuo.

Ingawa kiwango cha mshahara wa Rais wa Tanzania ni siri, sheria hiyo inaeleza kuwa mafao yao hukokotolewa kwa kuzingatia mshahara wa juu aliowahi kupata miezi aliyofanya kazi.

Kiwango cha mafao hayo hukokotolewa kwa kutumia kanuni za kiwango cha asilimia itakayopangwa na mamlaka husika.

Mbali ya mafao yake ya kazi, Rais Mstaafu hulipwa posho ya kila mwezi kiasi cha asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Kiasi hicho ni sawa na Sh80 kwa kila Sh100 anayopata Rais aliye madarakani.

ADVERTISEMENT

Licha ya posho hiyo, Rais hupewa ulinzi, msaidizi, katibu muhtasi, mhudumu wa ofisi, mpishi, dobi, mtumishi wa ndani, mtunza bustani, madereva wawili na gharama za mazishi atakapofariki.

Mafao mengine

Pamoja na malipo ya mkupuo anayopata Rais Mstaafu, pia anapewa pasi ya kusafiria ya hadhi ya kidiplomasia, yeye pamoja na mke au mume wake.

Rais pamoja na mke wake, pia hulipwa gharama za matibabu ndani au nje ya nchi.

Baada ya kustaafu rais pia hulipiwa matengenezo ya magari mawili yenye uzito usiopungua tani tatu, ambayo hutolewa na Serikali, ambayo pia hubadilishwa kila baada ya miaka mitano.

Kama hiyo haitoshi, Rais pia hujengewa nyumba mpya, ambayo ni lazima iwe na vyumba angalau vinne, viwili kati ya hivyo ni lazima viwe na huduma zote ndani (self-contained).

Aidha, nyumba hiyo ni lazima iwe na ofisi iliyokamilika na nyumba kwa ajili ya mfanyakazi wake.

Rais huyo mstaafu vilevile atagharimiwa gharama za mazishi pindi atakapofarikiMakamu wa rais na mawaziri

Mafao hayo ya viongozi wa umma yanampa nafasi Waziri Mkuu mstaafu na makamu wa rais fursa kama anazopata Rais, isipokuwa wao hawajengewi nyumba, pia wanapata gari moja tu.

Makamu wa rais na waziri mkuu wastaafu wanapewa fedha za kulipa mishahara ya watumishi, mpishi, dobi, mfanyakazi wa ndani, mtunza bustani na dereva.

Sheria hiyo inawakinga pia wategemezi wa viongozi wastaafu, hasa viongozi hao wanapofariki.

Kinga ya wategemezi wa viongozi hao iliundwa katika marekebisho ya Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Siasa ya Mwaka 1999, ambayo ilitiwa saini na Rais mstaafu Benjamin Mkapa Juni 2005. Marekebisho yaliyotiwa saini na Rais Mkapa ni pamoja na kuwalipa mafao wajane na wagane wa viongozi wa juu wa kitaifa akiwamo rais, makamu wa rais na waziri mkuu.

Rais mstaafu akifariki dunia, mke au mume wake hupewa nyumba, posho kiasi cha asilimia 40 ya mshahara wa rais aliye madarakani.

Aidha, mjane au mgane huyo hutengewa fedha za matibabu ndani ya nchi na matengenezo ya gari analopewa na Serikali.

Pia hulipiwa mshahara wa kima cha chini kwa dereva na mtumishi wa ndani pamoja na hupewa usafiri wa kwenda mahali atakapoishi maisha yake yaliyosalia.

Mabadiliko hayo yalilenga pia kuhakikisha kuwa iwapo kiongozi husika alikuwa analipwa pensheni kwa ajira ya awali, malipo yake yataendelea kutumiwa na mjane.

Aidha katika kikao cha Bunge la Bajeti mwaka uliopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kuwa Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya matibabu ya wastaafu wanaopaswa kutunzwa na Serikali.
 

Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,144
2,000
Hakugawia wenye nazo tena ukijumlisha alizogawa zote tangu awe rais hata robo ya hii bado maana alikuwa anagawa 5,7 au 10 million tena kwa kuchangisha na wengine wakenya wakiita harambee
Hivi ni nani aliwajengea Wazee(marais wastaafu) nyumba, juzi kati apo!
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,976
2,000
Alikuwa halipwi mshahara? Hata kodi hakuwa anakatwa Kwenye mshahara wake wakati hao wazee walikuwa wanakatwa. Kama huyo kapewa favor na wengine wapewe pia.
Hivi nyinyi mmezaliwa jana? hizi sheria zinapitishwa mlikuwa wapi? busy na simba na yanga. Huyu alikuwa Rais mkuu wa nchi na ziko sheria za JPM kazipisha wakati wake kuwalinda na mashataka mpaka speaker wa bunge. mna shida chagueni watu sahihi barabarani mko na kofia za kijani wanawatungua sheria hata habari hamna. Natakiwa kupewa gari 2 tena sio mara moja kila baada ya miaka 5 anabadilshiwa.
 

mapololo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
322
500
Tatozo la Waafrika ni Elimu zetu za Kikoloni.
Elimu inayowafanya wasomi kujiona ni wazungu kwa sababu ya kahitaji ya kizungu.
Uafrika wetu tumeuondoa na kukimbia uzungu kwa nguvu zote.Wakati wazungu wakitendeana utu mkubwa sana wao kwa wao.

Kila msomi wa Kiafrika anaamini na kuwaza kuwa ipo siku ataingia kwenye nafasi ya ulaji tuu, na sio kutumikia wananchi na kutumia elimu yake kuwasaidia wengine.

Ndani ya mwaka mmoja Bilionea Mzee Ruksa amekabidhiwa mali za mabiloni kwa kodi za watu maskini sana.

Kikwete yeye aliamini kuwa maisha bora yanamfaa kila mtu awe nayo . Akasema maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana.

Mama ameanza kumgawia Bilionea Gari la mamilioni.
Bila shaka maskini wanasubiri mgao wao kutokana na Rasilimali walizopewa wote na Mungu.

Mungu ana Hekima kubwa sana.
Ingekua Hewa ya Oxygen inagawanywa na watawala leo hii mgawanyo ungekuwa kwa Upendeleo na kujuana na sio kwa haki .
Ingekua kifo kingepangiwa Ratiba na watawala wetu wa kiafrika na dunia basi ratiba ya kifo isingeonekana kutemblea maeneo ya wakubwa wala magonjwa.

Kuua Demokrasia ilikua ni jambo baya sana katika nchi hii.
Waoua demokrasia wamepoteza utu na uwajibikaji wa viongozi wetu kwa karne ijayo.
Walaaniwe wakurugenzi na wote walioshiriki kuua Demokrasia katika nchi hii.

Nchi yenye Demokrasia wapiga kura wanaheshimiwa kwa kupewa keki ya taifa mana wanahoji na wanawakataa viongozi wanaotumia vibaya rasilimali za umma kwa manufaa yao.

Nchi siyo na Demokrasia Wapiga kura hawana thamani mana hawawezi kubadili utawala na uongozi.

Tanzania tulipotezwa sana kwa kupumbazwa na watu wa chache kwa manufaa yao huku Demokrasia ikiuawa sasa matokeo yake ni haya.
Watumishi wanaolipwa mshahara laki nne kwa mwezi huku wakiwa wanajitafutia wenyewe mahitaji yao yote mpaka nauli za kufika ofisini na nyumba ya kuishi na chakula wanaambiwa mishahara yao inatosha na serikali haitaongeza mishahara mana sio kipao mbele chake.
Huku watawala wakiwa wanajipa kila kitu kwa kodi za wananchi. Wafanyakazi hawana tena thamani mana waliambiwa kura zao hazifiki hata laki 5 hivyo hazina maana. Na atakayethubutu kumpigia kura mpinzani atakiona cha mtema kuni.

Kazi inaendelea.
Tuliaminishwa Corona imesababisha ugumu wa maisha ikiwemo kushindwa kupandishwa mishahara watumishi, sasa kumbe hali ngumu ya Corona ni kwakina sisi karubanzira wakati wengine wanapewa magari ya kifahari ilihali wanayo ma V8 mpaka wanashindwa kuyapanda, kwakweli hii nikifuru kabisa,wengine hata birthday hatujawahi kusherehekea wengine zawadi n Benz, Tanzania hii hii. Aiseee
 

KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
3,229
2,000
Tofauti ni moja wale ni wananchi wa kawaida walioenda kumsikiliza rais... Na yule ni rais mstaafu mwenye mtoto rais, aliyeenda kuzindua kitabu cha maisha yake
Kila mmoja hapo anakula kwa urefu wa kamba yake..
Aliyenacho huongezewa. Asiyekuwa nacho hunyang'anywa hata kile kidogo alichonacho.
 

mapololo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
322
500
Umri wenyewe ushaenda, Benz la nini , huyu mama anajifanya mother Theresa , kitamkuta kitu


Enz za magu Tz ilikua inaheshimika sana duniani, sasa hiv tumerud kuwa mazuzu, hapa raisi hatuna, miaka yake iishe tupige kura
Hata ukiisha utampigia Kura Nani wakati yeye ndiyo Rais anahitaji miaka 9,na yeye mwenyekiti wa chama kile na lazima atapitishwa tu,ningefurahi sana upinzani wapate mtu makini atakaye simama ili basi wachukue kijiti,lakini na upinzani Sasa tumegeuka na kuunga mkono juhudi za ugawaji magari ya kifahari
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,763
2,000
Namshauri Mh SSh mambo kama haya anayofanya yanamjengea picha mbaya ,angempa kimya kimya tu maana hata ilo kubwa refu alilokuwa anatembelea wakati anapewa hatukujua,ni vizuri kuwajali wazee ila next time afanye kimya kimya maana ilo la mwinyi kupewa gari halina faida kwa wananchi na hata wasipujua hakuna kitachoharibika.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,922
2,000
Wamempa gari mtu asiyehitaji gari, yaani hata mwanae Rais wa Znz angeweza mmnunulia gari , ila wale wazee walikuwa wanahitaji wamepewe hata elfu 30 tu kwa mwezi wametoswa
Mwacheni mzee wa watu, hasa baada ya matusi yote yale ya nguoni ambayo wazee wenu walimtukana walipokuwa chuoni UDSM. Na yeye wala hakuweka mwanafunzi yo yote ndani.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,959
2,000
Aisee we Heijah pamoja na kuwa ni mjadala ila ulichokileta hapa ni tofauti kabisa.

Mama alitoa gari (benz) kama zawadi ya birthday ya mzee Mwinyi na siyo kama unavyotaka kuniaminisha.

👉🏾Aya tuendelee...
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,976
2,000
Aisee we Heijah pamoja na kuwa ni mjadala ila ulichokileta hapa ni tofauti kabisa.

Mama alitoa gari (benz) kama zawadi ya birthday ya mzee Mwinyi na siyo kama unavyotaka kuniaminisha.

👉🏾Aya tuendelee...
Mama ana kiswahili cha kistaarabu sana anatumia maneno laini usichukue kauli yake maana angesema tunampa stahiki yake mzee wetu isingependesha sherehe, yule alikuwa Rais na ni mtu mzima 96 years na ile ilikuwa siku yake ya kuzaliwa pia alitoa kitabu chake akatumia fursa ile kumpa na kutumia neno zawadi kwa heshima kauli ya kiungwana. Chukua mfano wewe kumtunza Mama yako ni wajibu wako labda unamuhudumia kila siku, siku ya mother day umeamua kumpa zawadi kubwa mbele za atu ukasema Mama hii zawadi yako hakika Mama atafurahi sana japokuwa labda unampa kila kitu kila mara yeye atachukulia mwanangu ananipa kama Mama yake ila siku hata ukimpa kitu kidogo mbele za watu na kusema zawadi yako Mama atafurahi sana sio kwa ukubwa wa kile kitu ila heshima. Mama kampa heshima tu mzee afurahi ajisikie mbele za watu. angepata ile benzi kisheria nyuma ya pazia haki yake kama sheria na uhakika mzee asingetoa hata tabasamu. Sio mbaya kumfurahisha mzee kwa kutumia haki yake. Mama muungwana katumia lugha laini mzee afurahi unajuwa surprise ina raha zake bila kujalisha ukubwa wake.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,959
2,000
Mama ana kiswahili cha kistaarabu sana anatumia maneno laini usichukue kauli yake maana angesema ...... na kutumia neno zawadi kwa heshima kauli ya kiungwana. Chukua mfano wewe kumtunza Mama yako ni wajibu wako labda unamuhudumia kila siku, ...
Mama alishasem la yeye na JPM ni kitu kimoja, tuendelee kuwa wavumilivu hadi tutakapo pata kitu kingine cha tofauti!.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,959
2,000
Mama ana kiswahili cha kistaarabu sana anatumia maneno laini usichukue kauli yake maana angesema ...... na kutumia neno zawadi kwa heshima kauli ya kiungwana. Chukua mfano wewe kumtunza Mama yako ni wajibu wako labda unamuhudumia kila siku, ...
Mama alishasema yeye na JPM ni kitu kimoja, tuendelee kuwa wavumilivu hadi tutakapo pata kitu kingine cha tofauti!.
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,976
2,000
Mama alishasem la yeye na JPM ni kitu kimoja, tuendelee kuwa wavumilivu hadi tutakapo pata kitu kingine cha tofauti!.
Ndugu yangu serikali ni ya chama cha CCM, mgombea yoyote kazi yake kutekeleza yaliyopo katika sera zao walizozinadi hakuna mtu akaja na yake kichwani tofauti ni njia tu za kukufikisha katika katika sera zao. Kama sera ni kwenda Arusha basi mwingine atapitia njia ya Moshi, mwingine Singida na mwingine Dodoma wote watafika Arusha njia tofauti tu. Ndio serikali ya CCM kwa kuwa wamechaguliwa watakeleza waliyoyasema nchi haiendi kwa utashi binafsi ni CCM huo ndio ukweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom