MADA YA WEEKEND: Wazee wa Dar na Benz la Mwinyi

basi kuna walakini kwa waliokua wanatunga hizo sheria .walikuwa walafi kupindukia zote hizo ni kodi za wanainch
Hapo umenena haya mambo yaliongelewa bungeni yakapita na sio hilo tu wamepitisha sheria kuongezea kuwa viongozi hawatashtakiwa wakitoka madarakani zamani ilikuwa Rais tu siku hizi mpaka waziri mkuu na speaker wa bunge na naibu wake ndio maana unaona Ndungai haogopi kuvunja sheria. suala la mafao lilijadiliwa sana lakini wananchi walikaa kimyaa likapita sasa tukae kimya pia.
 
Mnasemaje kwa yule jamaa aliekuwa akigawa fedha kwa wananchi wanyonge..?
Yule walisema anagawa tu pesa kama zake bila kufuata sheria sasa huyu kwa sababu ni rais wa matajiri na wawekezaji sheria zenu hizo za wanyonge hazimuhusu ! Kazi iendelee
 
Tofauti ni moja wale ni wananchi wa kawaida walioenda kumsikiliza rais... Na yule ni rais mstaafu mwenye mtoto rais, aliyeenda kuzindua kitabu cha maisha yake
Kila mmoja hapo anakula kwa urefu wa kamba yake..
Mtoto wake ambaye ni rais na mwingine ambaye ni mbunge kweli kabisa wameshindwa kumnunulia mzee wao gari lunaloendana na umri wake??
 
Hivi Mwinyi anahitaji gari la kwenda wapi na ule umri wake, nafikiri zawadi ya mkongojo au kiti cha kupumzikia ingemfaa zaidi kuliko gari la kifahari. Yaani ukitafakari upeo wa viongozi wa nchi hii unaishia kusikitika, imagine pesa ya kujenga visima vinne vya maji kwenye vijiji inateketezwa kwa staili hiyo..
 
Hivi nchi hii nani katuroga? wazee wanataka wawe wanalipwa kila mwezi alfu 30 kwa maisha yao yote na wazee hawaishi vijana wa leo kesho wazee na utatumia kigezo kipi kusema huyu sasa mzee jana alikuwa bado apewe alfu 30 wanasema kuna wazee 2.5 million hiyo kila mwezi billion 75 kwa mwaka katibia trillion acheni utani kila aliyefanya kazi kuna fao la uzeeni hayo ndio malipo ya kisheria. Kelele zote hizi gari na gari zenyewe unasikia watu kodi zetu utasema hata hiyo kodi wanalipa. haya magari walipewa zawadi wa mfalme wa Morocco acheni roho za chuki yuke mzee alikuwa Rais nchi hii na anamiaka 96 anastahili. Mimi nilikuwa nawaunga kiasi mkono wapinzani lakini hii tabia ya kudandia kila jambo na kuwa negative nimewashusha utasema Mzee kapewa bombadier kelele za watu.
Acha mambo ya kipindi wewe. Bado ukweli uko pale pale, haya ni matumizi mabaya sana ya kodi na fedha za umma. Huyo mstaafu sheria imempa retirement packages kubwa mnoo na ya upendeleo, including V8 na 80 % ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Hii peke yake ni unyonyaji mkubwa sana, kama pia ilivyo kwa viongozi wengine na wabunge, ambao pamoja na kwamba hawacgangii mifuko ya pensheni hata senti tano, wakistaafu wanazoa mamia ya mamilioni kutoka kwenye michango ya wafanyakazi masikini wenye mishahara kuduchu. Kama hilo V8 linamsumbua kwa nini lisiuzwe na akanuniwa gari ingine?? Hata kama hizo benzi ni msaada kwa nini wasipewe watendaji serikalini wenye upungufu wa magari?? Mmekalia kujipendekeza tuu kwa mambo ya ajabu ajabu...
 
Nyumba wanapewa kisheria imetungwa maraisi wastaafu wote wanajengewa na sheria waliopitisha ni hao hao tunaowachagua bungeni na Rais anahudumiwa mpaka usafiri na ulinzi wake na serikali.
Ni sheria ya kipuuzi sana, ingekuwa ya maana hata kipindi cha Nyerere ingekuwepo. Nitajie ni rais gani mstaafu ambaye mpaka abastaafu hana nyumba yake, nani???
 
Mwenye nacho anaongezewa..mwenye kidogo utapokonywa na hicho ulichonacho the world is not fair..
 
Umri wenyewe ushaenda, Benz la nini , huyu mama anajifanya mother Theresa , kitamkuta kitu

Enz za magu Tz ilikua inaheshimika sana duniani, sasa hiv tumerud kuwa mazuzu, hapa raisi hatuna, miaka yake iishe tupige kura
Tatizo kupiga kura siku hizi wala siyo tiketi ya kumpata kiongozi umtakaye...
 
Nadhani Mama aliongea sababu ya kumpa gari ndogo, Huyu mzee ana miaka 96 na amekuwa anaitwa katika shughuli mbalimbali za kiserikali kama Rais mstaafu, kasema tunamuona shida anayopata wakati wa kupanda gari na kushuka tunampa gari ndogo asipate tabu huyu ni mtu mzima 96 years old na mtu aliyewahi kushika nafasi kubwa katika nchi hii. Jamani hata mzee wetu tunamsakama utasema kapewa Boeng gari zenyewe zilikuwa zawadi tu toka Morocco.
Nani kakwambia huyo mzee hana uwezo wa kununua saloon ndogo? Acheni kushabikia misuses of public funds...
 
Hivi nchi hii nani katuroga? wazee wanataka wawe wanalipwa kila mwezi alfu 30 kwa maisha yao yote na wazee hawaishi vijana wa leo kesho wazee na utatumia kigezo kipi kusema huyu sasa mzee jana alikuwa bado apewe alfu 30 wanasema kuna wazee 2.5 million hiyo kila mwezi billion 75 kwa mwaka katibia trillion acheni utani kila aliyefanya kazi kuna fao la uzeeni hayo ndio malipo ya kisheria. Kelele zote hizi gari na gari zenyewe unasikia watu kodi zetu utasema hata hiyo kodi wanalipa. haya magari walipewa zawadi wa mfalme wa Morocco acheni roho za chuki yuke mzee alikuwa Rais nchi hii na anamiaka 96 anastahili. Mimi nilikuwa nawaunga kiasi mkono wapinzani lakini hii tabia ya kudandia kila jambo na kuwa negative nimewashusha utasema Mzee kapewa bombadier kelele za watu.
Alikuwa halipwi mshahara? Hata kodi hakuwa anakatwa Kwenye mshahara wake wakati hao wazee walikuwa wanakatwa. Kama huyo kapewa favor na wengine wapewe pia.
 
Inasemekana alichoka kutumia v8 ziko juu sana kwa umri wake,ikabidi azawadiwe chuma ya chini chini ambayo anaweza ingia amelala,sema maisha inabidi kuwa na subra la sivyo nikukufuru.
 
Acha mambo ya kipindi wewe. Bado ukweli uko pale pale, haya ni matumizi mabaya sana ya kodi na fedha za umma. Huyo mstaafu sheria imempa retirement packages kubwa mnoo na ya upendeleo, including V8 na 80 % ya mshahara wa rais aliyeko madarakani. Hii peke yake ni unyonyaji mkubwa sana, kama pia ilivyo kwa viongozi wengine na wabunge, ambao pamoja na kwamba hawacgangii mifuko ya pensheni hata senti tano, wakistaafu wanazoa mamia ya mamilioni kutoka kwenye michango ya wafanyakazi masikini wenye mishahara kuduchu. Kama hilo V8 linamsumbua kwa nini lisiuzwe na akanuniwa gari ingine?? Hata kama hizo benzi ni msaada kwa nini wasipewe watendaji serikalini wenye upungufu wa magari?? Mmekalia kujipendekeza tuu kwa mambo ya ajabu ajabu...
Acha ujinga wewe hizo sheria natunga mimi? akili za watu wengine unaamka leo wakati sheria zinapitishwa mlikuwa busy na habari zakimbea nenda kaongee na wabunge wako mambo yalijadiliwa bungeni watu wakapiga kelele mimi mmoja wapi ila mlikuwa wapi kupaza sauti. nchi ya watu wa ajabu. sheria mbaya nzuri hili analihusu ila ndio sheria muache roho za korosho pambana mwenyewe.
 
Back
Top Bottom