Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Mada Moto Channel Ten: Julius Mtatiro vs Humphrey Polepole

Polepole kajiabisha sana, ana chuki binafsi na Lowasa maana madhambi ya wengine hayaoni bali anaona ya Lowasa tu.
 
Pole pole hovyo kweli..hana hoja...

Kila akinena anamtetea Magufuli, na kukashifu Lowassa...

Julius Mtatiro, kamwaibisha sana Polepole, kuwa, Magufuli ni mtu mdogo sana CCM, na Magufuli ana tuhuma nyingi sana tu za kuuza nyumba za serikali, kuwa na mahoteli eg Kebby's hotel Mwenge, pia CAG mara kadhaa katoa data za kimahesabu Wizara anayoongoza Magufuli billions zimepotea..na hazijulikani ziko wapi...

Mpolepole akataka kudanganya eti leo wakati anakaribia kwenda Channel 10 mtu mkubwa wa Cuf kampigia simu eti anapinga ujio wa Lowassa Ukawa....Mtatiro akamwambia aache kuhadaa watu, kwa kumtetea Magufuli, na pia Polepole anajua wazi CCM ndio imechakachua katiba mpya, bado Polepole anaitetea mfumo huo huo...
Pole pole ni mhuni, hana hoja..ana chuki binafsi na Lowassa....!!!

Polepole....kichwa cha ufisadi...dwarfed body and mind...!!!

Bahati mbaya hujaongea point
 
Polepole hana msimamo ni ushabiki tu wa kununuliwa na kitengo cha ccm! Eti leo anawaona mafisadi waliobaki kwenye ubunge wao washughulikiwe na wananchi na siyo kitengo tena! Mbona kwenye Urais hawakuwaachia NEC wapige kura?

Eti wanataka mageuzi siyo mabadiliko, kwa hiyo tuendelee kusubiria mageuzi kwa kuirudishia ccm madarakani wakati yenyewe ndo imetupilia mabali katiba mpya?

Jamaa huyu hata mtangazaji naona ameshamuona kalambishwa maana anajaribu kutetea kitu ambacho hata yeye mwenyewe anakipinga!

Mtatiro amekomesha leo amekula naye sahani moja kila akijaribu kupiga chenga anaye tu na mwisho ndo kamulaza chali kabisa "We need strong institution and not Strong people"

Hongera mtatitiro nadhani ametuelewa wapenda mabadiliko!
 
Kimsingi wote wamejinganya ila kinachotusukuma ni upepeo tu kiukweli wote wameonyesha wazi katika vyama vyao hakuna mtu anaefaa kuwa raisi
 
Kwani huyo pole pole naye kawa mtangazaji wa Chanel10, au hana shughuli za kufanya maana naona kila nikisikia mada moto namkuta ni yeye tu, hadi wakati mwingine yuko peke yake.
Na nyie chanel 10 si mtafute watu wengine au ndo nanyie mnajifia?

ndo hapo na huyo mnafiki alijifanya anaitetea katiba hakuna kitu hapo ameshakuwa ibilisi huyo yale mbowe alisema ukimchukua malaika ukamwacha ccm mwaka tuu utakuta kageuka ibilisi ndo polepole huyo.
 
mbona mtatiro kamtuliza tu huyo polepole....tatizo siku ile alimpata msigwa akapata mteremko...leo kapata size yake
 
Matatizo ni mtu kupenda. MAPENZI MTU YAKIMZIDI HUWA HAONI. MTU CHAKE APENDACHO HAKINA HILA MACHONI!!! HP HANA HILA TENA, AMESAHAU UKWELI WALA HAUHITAJI TENA!!! AMEJISAHAU NA AMEANZA KUNG'ANG'ANIA NENO MOJA MTU MMOJA... HANA HOJA TENA. JM AMEMALIZA KAZI
 
Mara kadhaa nimemsikiliza Bwana Polepole lakini nimeishiwa kuchanganyikiwa. Kuanzia polepole wa Tume ya warioba hadi Pole pole huyu wa Magufuli na mgombea mwenza wake.
Polepole tupe bandiko lako juu ya katiba ipi unayoipigania ,ni ile pendekezwa ama ile ya Jaji Warioba. Tupate fungu la kukuweka maana haijulikani unatembea,ama mchakamchaka,wewe upo pole pole tu.
 
Watanzania tufike mahala tumpuuze polepole
Tushamgundua anatupotosha kwa masilahi yake binafsi
Njaa inamsumbua tu!!
 
Leo channel 10 Ni zamu ya Mtatiro na Polepole. Don't miss saa 4 kamili usiku.

Leo polepole amejidhihirisha kua na chuki binafsi na Lowasa ameshindwa hata kujua mahitaji ya watanzania. NA leo amekutana na kisiki cha mpingo
 
Usitudanganye na sisi tunaangalia.
Hata sisi tuliangalia kwanini unataka sema umedanganywa wapi? Karibu ktk siasa..maji waliyoyashindwa makatibu kibao na viongozi wengine wa CCM...polisi na wakuu wa mikoa, wilaya wote wamechemsha.
 
mtatiro kamalizia vema..
Tatizo sio mtu mmja ni mfumo..
 
Polepole anasema kuwa wananchi wanataka mageuzi 'transformation' na sio mabadiliko kwa maana ya change.Akasema ukawa wanahubiri kuhusu mabadiliko wakati wananchi wanataka mageuzi.

Mifano aliyoitoa huyu polepole kuelezea hayo mageuzi amejikuta akijichanganya na kwakweli sasa naweza kusema kwa uhakika kabisa huyu jamaa ana agenga yake ya kukipigania chama cha mapinduzi hata kwa kujifanya haelewi ili tu malengo yake yatimie.

Ametaja Muungano.Kwamba watanzania wanataka mageuzi ya muungano.Huu uliopo haufai na umeshindwa.Hili lipo kwenye rasimu ya mzee Warioba ambayo ni moja ya misingi mikubwa ya muungano wa UKAWA.

Ametaja watanzania wanataka raisi ambaye madarajka yake yanadhibitiea na katiba.Yani hana mamlaka ya kupindukia kama ilivyo kwa katiba ya sasa hivi.Hili lipo kwenye rasimu ya katiba ya Warioba ambayo inasimamiwa na UKAWA na kubezwa na CCM na Polepole analijua hilo sana kuliko mimi..

Ametaja kitu kingine cha mageuzi ambacho wananchi wanataka ni kuwa na uwezo wakuwawajibisha wabunge easiowajibika kwenye majimbo yao.Hili pia ni moja ya msingi uliopo kwenye katiba ya mzee Warioba ambayo ni mwimbo ulioifanya UKAWA ukawepo......
.
Sasa najiuliza haya makusudi ya kutoa hoja za kijinga kabisa huku akijicontradict mwenyewe huyu Polepole ni kwa manufaa ya nani?Mifano yake ya hiyo anayoita transfomation yote ni mihimili ya katiba ya wananchi na haikubaliki kabisa CCM.Sasa bado anataka watu wachague CCM kupata transformation zipi wakati zote zipo kwenye agenda ya UKAWA?Na yeye ni shahidi kuwa ccm hawataki hayo mambo na ndo moja ya kitu kilichompa yeye umaarufu kwa kuwasema sana ccm kuwa wanapuuza maoni ya wananchi

Leo hii sarakasi anayopiga huyu polepole ni kwa manufaa ya nani?Polepole atueleze sasa kuwa hata kwenye mchakato wa katiba yeye alikuwa anaigiza tu kuwa anaiunga mkono katiba ya wananchi huku akijua chama chake hakiwezi kuipitisha ili tu kutafuta wafuasi ambao watamwamini ili aje kuwadrive upandevwa ccm kwenye uchaguzimkuu.Hapo nitamuelewa sana lakini kinyume na hapi anajichanganya sana huyu jamaa
 
Polepole leo kaishiwa hoja maana Mtatiro kammaliza mazima, halafu tunaomba Channel ten watupumzishe na huyu Polepole kwani hakuna watu wengine!
 
Polepole anasema suala la kuuzwa nyumba za serikali alaumiwe waziri mkuu si magufuli kweli anamtetea magufuli kwa hoja dhaifu hivi......hata ingekuwa wa kulaumiwa ni waziri mkuu magufuli kama hakukubaliana na hili suala si angejiuzulu basi?......na ili kuonyesha chuki ya wazi kwa lowasa anasema anashukuru moja ya aliyekuwa waziri mkuu wa magufuli yaani lowasa alikatwa nadhani alidhani nyumba za serikali ziliuzwa wakati lowasa akiwa pm..
 
Back
Top Bottom