Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Mnamo mwaka wa 1972, ndege ya American Airlines Flight 119 ilitekwa nyara na Martin McNally mwenye umri wa miaka 28, ambaye aliingiza kinyemela bunduki ndogo na kudai kiasi cha dila $500,000 pamoja na miamvuli ya kurukia.

Baada ya ndege kurejea St.Louis na abiria wengi kuachiliwa, McNally alijiandaa kupaa tena akiwa na wafanyakazi na pesa taslimu.

Lakini ndege ilipokuwa ikitembea kwenye njia za maungio (Taxiway) David J. Hanley, mfanyabiashara wa eneo hilo mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa akitazama mchezo huo ukifanyika kutoka sebule ya uwanja wa ndege aliua kujichukulia mambo mikononi mwake.

Aliendesha gari lake la 1971 Cadillac Eldorado kupitia uzio wa uwanja wa ndege na kugonga tairi ya ndege ikiwa mwendo wa kasi, na kusitisha utekaji nyara kwa muda.

McNally, bila kukata tamaa, alidai ndege nyingine na akahamishiwa kwenye ndege ya pili ya Boeing 727.
Akiwa angani, aliruka kwa parachuti juu ya Indiana, ingawa alipoteza mfuko wa pesa wakati wa kuruka.
FB_IMG_1749518549981.jpg
 
Mmiliki wa mnyama jamii ya sungura ameanzisha ombi la kutaka shirika la ndege la Uingereza, Loganair, kubadilisha sera zake za usafirishaji wa wanyama baada ya sungura wake anayefahamika kama Romeo kukataliwa kupanda ndege akiwa katika hali ya dharura kiafya.

Romeo, ambaye anaishi kwenye kisiwa cha Papa Westray kilichopo katika visiwa vya Orkney kaskazini mwa Scotland, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa hatari unaojulikana kama “gastrointestinal stasis”, hali inayosababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kusimama.

Kwa mujibu wa mmiliki wake, usafiri wa feri hutumiwa mara nyingi kumpeleka Romeo kwa daktari wa wanyama,lakini hali mbaya ya hewa ilisababisha feri nyingi kushindwa kufanya kazi, na ndege za shirika la Loganair kuwa namna pekee ya usafiri iliyosalia. Lakini, sera za Loganair zinaruhusu usafirishaji wa paka na mbwa pekee, bila kuwepo kwa ubaguzi hata kwa hali ya dharura kama hii.

Romeo anaishi kwenye kisiwa cha Papa Westray, sehemu ya visiwa vya Orkney vilivyo kaskazini mwa Scotland, ambako kuna wakazi wasiozidi 90 na hakuna daktari wa wanyama. Kwa kawaida, safari ya kutafuta matibabu huhusisha feri mbili na basi. Njia hii pia hutumiwa na ndege za Loganair, ambazo hutegemewa sana na wakazi wa visiwa hivyo.

Jumatano iliyopita, Romeo alianza kuugua kwa kasi na alihitaji matibabu ya haraka kutoka kwa daktari. Kwa kuwa safari za feri zilifutwa kutokana na dhoruba, ndege ya Loganair ndiyo iliyobaki kuwa tumaini pekee. Lakini, sera kali ya shirika hilo kuhusu usafirishaji wa wanyama ilimzuia Romeo kusafiri.

Kwa sasa, Loganair huruhusu tu paka na mbwa kusafiri kwenye ndege zao, hasa zile ndogo aina ya Britten-Norman BN-2 Islander zenye uwezo wa kubeba abiria nane tu. Shirika hilo limetoa tamko kwamba hawasafirishi wanyama wengine kwa kuhofia “kufungua mlango kwa kila aina ya mnyama kuomba kusafirishwa”.

Mmiliki wa Romeo sasa ameanzisha ombi la kutaka Loganair ibadilishe sera zake ili kusaidia wanyama wengine wanaoishi katika maeneo ya mbali kama Papa Westray, hasa wakati wa dharura.

#airline #rabbit #animalrights #loganair #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates
FB_IMG_1749518912052.jpg
 
Ndege ndogo aina ya Piper Cherokee yenye usajili wa ZS-KFB ambayo ilitoweka tarehe 8 Juni 2025 imepatikana imeanguka karibu na Mto Mooi huko KwaZulu-Natal na kugharimu maisha ya watu watatu waliokuwemo.

Mmoja wa waliofariki ni Nqobile Biyela, rubani kijana wa kike mwenye miaka 23.

Ajali hiyo imeanzisha uchunguzi rasmi wa Idara ya Upelelezi wa Ajali na Matukio ya Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (AIID) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Afrika Kusini (SACAA).

Ndege hiyo ya Piper Cherokee iliripotiwa kuondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Virginia mjini Durban takriban saa 3:00 Usiku na ilionekana mara ya mwisho ikiruka juu ya Ladysmith, ikielekea kusini kuelekea Pietermaritzburg au Greytown, kabla ya mawasiliano kupotea.

Operesheni ya utafutaji na uokoaji, iliyoratibiwa na Kituo cha Kuratibu Uokoaji wa Anga (ARCC), ilihusisha juhudi za mashirika mengi, na timu kutoka Utafutaji na Uokoaji wa SAPS, Zimamoto na Uokoaji Okhahlamba, Huduma za Matibabu ya Dharura ya KZN (EMS), ER24, Netcare911, Hamnet, Berg Flying, 1 MTNlunte Community Services na mashirika mengine ya Greytis91 ya Greytown na G91.
FB_IMG_1749651937712.jpg
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imejibu taarifa kuhusu uamuzi wa Tume ya Ulaya ya kupiga marufuku Mashirika ya ndege zilizoidhinishwa na Tanzania kutoka au kuingia katika anga la Umoja wa Ulaya (EU).

TCAA imesema kuwa hatua hiyo haina athari za kiutendaji kwenye
huduma zilizopo na kuthibitisha kuwa usalama wa anga nchini Tanzania bado upo imara.

EU ilitoa taarifa ya katazo kwa ndege zilizosajiliwa Tanzania na Surinam kwenye Orodha yake iliyosasishwa ya Usalama wa Anga ya Umoja wa Ulaya mnamo Juni 4, 2025, ikitaja maswala makubwa ya kiusalama yaliyotambuliwa wakati wa tathmini ya kiufundi.

Tume iligundua mamlaka za usafiri wa anga za nchi zote mbili hazina uwezo wa kutosha wa kutekeleza viwango vya usalama vya kimataifa kutokana na uhaba wa wafanyakazi waliohitimu na maeneo ya uendeshaji na udhibiti ambao haufanyi kazi.

Salim Msangi, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, aliwahakikishia wadau kuwa hakuna ndege yoyote kutoka Tanzania inayofanya safari za ndege kwenda au kutoka EU maana yake marufuku hiyo haina athari za haraka katika uendeshaji wa sasa.

Hata hivyo Mamlaka imesema kuwa inashirikiana kikamilifu na wadhibiti wa Umoja wa Ulaya kushughulikia masuala yaliyoibuliwa wakati wa tathmini yao, lengo ni kusuluhisha maswala yote yanayosalia ya usalama na hatimaye kupata uondoaji kutoka kwa orodha iliyoidhinishwa.

TCAA ilisisitiza kuwa kanuni za usafiri wa anga nchini zinaendana na viwango vya ICAO na kwamba mashirika yote ya anga ya Tanzania yanatakiwa kuzingatia hayo kikamilifu.

Marufuku hiyo inaathiri ufikiaji wa soko la EU siku zijazo lakini haitumiki kwa safari za ndege ndani ya Tanzania au nchi zingine nje ya EU.

EU inachukulia marufuku hiyo kama hatua ya tahadhari na si hukumu kutoka kwenye tukio au ajali.

Wakati wa ukaguzi wa hivi karibuni wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO USOAP-CMA) Tanzania ilipata asilimia 67.3 ambayo ni juu ya wastani wa kimataifa katika Utekelezaji wa Ufanisi na usimamizi wa vipengele muhimu vya usalama wa anga.
FB_IMG_1749670687966.jpg
 
 
Mnamo Tarehe 10 Juni 2025, ndege ya shirika la Wizz Air, Boeing 737-800 inayoendeshwa na GetJet Airlines ilibinuka kukalia nyuma wakati wa ushushaji kwenye Uwanja wa Ndege wa Haugesund Karmøy, Norway.

Taarifa inasema, upakuaji wa mizigo ulioanzia mbele ulisababisha uzito kusalia nyuma na kusababisha mkia wa ndege kugusa chini.

Kwa bahati nzuri, hakuna majeraha yaliyoripotiwa, lakini ni ukumbusho wa umuhimu wa usahihi wa upangaji wa mzigo kwenye ndege.
FB_IMG_1749730181565.jpg
 
Je, uligundua ushiriki wa Paka huyu kwenye kipande hiki cha Helikopta (Helicopter Scene) katika filamu ya World War Z?
FB_IMG_1749762663594.jpg
 
Mradi wa Treni-Ndege ya umoja wa Kisovieti (Soviet Jet Train) ulianza katika miaka ya 1970 kwa wazo rahisi, weka injini za ndege ambazo haziwezi kutumika tena angani, lakini bado zinaweza kutumika ardhini.

Kwa mradi huu, Treni ya ER22 ilirekebishwa umbo kuweza kusimikwa injini za ndegevita ya YAK-40 kuunda treni ya majaribio.

Mnamo mwaka 1971 hadi 1975 Treni yenye injini ya ndege iliundwa na kufanyiwa majaribio kwenye njia ya reli kama sehemu ya Mradi wa Treni mwendokasi ya ER200.

Mnamo 1972, Treni ilifikia kasi ya 250 km/saa katika Reli ya Dnieper, na kuweka rekodi kwa reli za Soviet.

Mnamo 1975, baada ya kutolewa kwa Tteni ya ER200, hitaji
kwa treni ya mwendo kasi yenye injini za ndege ilitoweka na mradi ukaghairiwa.
FB_IMG_1749781376332.jpg
 
𝗠𝗮𝗺𝗯𝗼 𝘆𝗮 𝗚𝗼𝗱.Ramesh miraculously survived the Air India crash. According to reports, he jumped through the emergency exit just seconds before the Boeing 777 hit the ground. He was the sole survivor out of 242 people on board.
Quick recovery to him.
1749797370857.jpg
 
#HABARI Ndege ya Air India iliyokuwa inatoka Phuket nchini Thailand kuelekea mji mkuu wa India New Delhi imelazimika kutua kwa dharura katika kisiwa hicho kutokana na kupokea taarifa za tishio la bomu katika ndege hiyo

Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Phuket kuelekea mji mkuu wa India saa tatu na nusu asubuhi leo Ijumaa, lakini ilizunguka Bahari ya Andaman na kutua tena kwenye kisiwa cha kusini mwa Thailand

Afisa mmoja wa viwanja vya ndege vya Thailand amesema kuwa abiria wote 156 waliokuwa kwenye ndege hiyo ya AI 379 walisindikizwa kutoka kwenye ndege hiyo wakiwa salama

Hata hivyo walinda usalama wa Thailand walifika haraka, wakaikagua ndege nzima, hakuna bomu wala vilipuzi vilivyopatikana na tayari uchunguzi rasmi wa tukio hilo umeanza #EastAfricaTV
 
Back
Top Bottom