Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Alikuwa Tayari amekwisha fariki wakati gari likiseleleka katikati ya barabara. Raia mmoja aliyekuwa akiendesha gari dogo aligundua na Kuamua Kutoa Msaada wa dharula. Hata hivyo selikali ya Mascow imempa zawadi ya dola za kimarekani Elf 80000 (Sawa na Shilingi Million 200 za Tanzania na 10,300,000 za Kenya) Kwa raia huyo shuajaa aliyejitoa muhanga Kutoa msaada wakati wengine wakikwepa.

Hata hivyo ripoti zinaeleza kuwa dereva huyo alifariki ghafla akiwa katika usukuani dakika chache tu kabla ya gari Hilo kuanza kuseleleka. Sababu za kifo chake hazijawekwa wazi na madaktari



View: https://www.facebook.com/share/v/1FcBDrpW8m/
 
Dereva wa magari ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), anayefahamika kwa jina la John Joseph Mchamba, alizua taharuki na mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana akiendesha gari katika kina kirefu cha maji yaliyokuwa yamejaa barabarani katika eneo la Kilosa kuelekea Mikumi, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, dereva huyo anaonekana akilazimika kuendesha gari kupita kwenye maji mengi yaliyofunika sehemu ya barabara, jambo lililowashangaza na kuwatia hofu baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutokana na hatari iliyokuwepo.

Akizungumza na Ayo TV, Mchamba alisema alichukua uamuzi huo mgumu kwa lengo la kuokoa maisha ya mama aliyekuwa ametoka kujifungua pamoja na mtoto wake, ambao walikuwa katika hatari ya kusombwa na maji hayo yaliyokuwa yakiongezeka kwa kasi.

Alifafanua kuwa hakukuwa na njia nyingine ya haraka ya kuwavusha salama isipokuwa kuvuka eneo hilo lenye maji mengi.
“Nililazimika kufanya uamuzi huo kwa sababu hali ilikuwa mbaya sana. Kama nisingefanya hivyo, mama pamoja na mtoto wake wangeweza kusombwa na maji na kupoteza maisha,” alisema Mchamba.

Tukio hilo limeibua hisia mbalimbali mtandaoni, huku baadhi ya watu wakimsifu kwa ujasiri na moyo wa kujitoa kuokoa maisha ya wengine licha ya hatari iliyokuwepo. Wengine wameeleza kuwa kitendo chake kinaonesha umuhimu wa ubinadamu na kujitolea katika nyakati za dharura.

Maoni yako ni yapi katika hili

✍️ Zhuhura Abdullah
FB_IMG_1773317439778.jpg
 
Back
Top Bottom