Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,532
2,000
Habarini wana jumuiya kubwa ya JamiiForums,

Ni wakati sasa wa kuwa na mada yetu maalum kwa kaliba hii kubwa na pana yenye dhamana adhimu ya kuhakikisha tunasafiri na kufika tuendako salama iwe:
 • Makazini
 • Kwenye starehe
 • Kwenye dharura
 • Kutembeleana nknk
Ni kaliba hii adhimu pia yenye dhamana kubwa ya kufikisha salama mizigo na vifurushi vyetu vyote vya kibiashara, kikazi nknk

Mada hii maalum ni jumuishi ya:
 • Madereva wa magari makubwa na madogo ya mizigo
 • Madereva wa boda to boda
 • Madereva wa magari yote ya abiria
 • Madereva wa viongozi, matajiri na watu maarufu
 • Madereva wa mitambo
 • Madereva bajaj bodaboda wote kwa ujumla wao
 • Na mwisho kabisa madereva wa magari binafsi
Mada hii ni maalum pia ya kusimuliana changamoto mbalimbali za barabarani kuanzia vibali, uendeshaji mbovu, ushirikina, maafisa usalama, mamlaka zenye dhima na usafiri nk.

Kuna ishu ya uzoefu pia ambayo tunaweza kushirikishana hapa ili kupata uzoefu incase likitokea la kutokea ujue jinsi ya kukabiliana nalo

Hakuna mahali hapakosi vituko na vibweka. Kwenye hii kaliba pana ya usafiri vipo vya kutosha. Je, una kituko chochote? Huu ni uwanja wako sasa.

La mwisho lakini ambalo si la mwisho kabisa ni swala zima la kupeana connection. Madereva wazoefu na wazuri ni wengi mno lakini shida inakuja kwenye ajira. Kupitia mada hii nina HAKIKA TUNAWEZA KUPEANA SHAVU LA AJIRA

Ni mada pana na yenye ulingo mpana sana. Kuna mengi ambayo sijaandika hapa. Naomba ushiriki wenu kwa yale niliyosahau.

Dondoo baadhi za uzoefu wangu kwenye udereva
 • Nidhamu barabarani huepusha ajali nyingi
 • Barabarani derava hapaswi kuwa na maamuzi mawili kwa wakati mmoja
 • Muda wote ni dereva anapokuwa kwenye usukani ni lazima macho yake yaone sekunde 15 mbele toka alipo
 • Inapotokea dharura ya pancha si vema kufunga breki ghafla
 • Muhimu muda wote kusoma taa za tahadhari kwenye dashboard
Tutazidi kushirikina mengi kadiri mada itakavyokuwa inaendeleea, na hata kama kuna links za kazi za udereva tutapeana hapa
Nitangulie kuwatakia maandalizi mema ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kwa madereva wenzangu tuna DHIMA kubwa ya kuzivusha salama mwaka huu roho za mamilioni ambazo ni ndugu jamaa marafiki na wanadamu wenzetu.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,532
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom