Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

Monday

Duncan run,nikiwe na gabr wakiwa mubashara na yao,nikiwe anapigiwa simu na engineer wa SG akimweleza kuwa upande wao hauna tatizo la uchafuzi wa maji.nikiwe anafurahia

The rec,kamo anatoka kuhudumia mteja kufika kanteni analalamika wateja hao hawajampa tip kwa huduma,akiwa anaonhea na aphiwe kanteni obakeng anatokea,obakeng analimia huku akimuangalia kamo,aphiwe anamuuliza maendeleo yake,kamo anaaga na kuondoka,obakeng anamwangalia ,kisha anamwomba msamaha aphiwe kwa yote aliyomtendea na kwamba keshagundua kosa lake,aphiwe anamwambia ameshamsamehe

Zukisa yupo kwa lerato,matlala anapiga simu ila zukisa hapokei,lerato anamshaur apokee simu maana jamaa ataendelea kupiga bila kuchoka,kisha wanaongelea ishu ya obakeng na kamo na kwamba lerato anataman kamo akajifungulie kwao maana zamdela wana drama nying. Matlala anagonga hodi,lerato anamfungulia na kuanza bishana nae ila zukisa anamuomba lerato awape nafasi waongee

Barker akiwa ofisin na brad na rajesh wakiongelea tatizo la kuvuja kwa acid kwenye mitambo yao,huku akilalamika wanawalipa wataalam wao ila wanafanya uzembe na kusema maji ya matumizi ya nyumban inabidi huduma isimame haraka. Rajesh aansema itawalia pesa ila barker anasema wawasiliane na manispaa.rajesh anasema mamlaka hawatapenda ila barker anamwambia ahakikishe anasolve tatizo hilo kisha anamtuma brad akatafute jibu kwann bomba limepasuka wakat wanalipa wataalam

Lerato yupo salun anamalizia mpaka dawa ya nywele mteja,mfanyakazi wake anaingia na kumwambia hamna maji hata kidogo,lerato anamtaka mteja avumilie atafute ufumbuzi,lerato anampigia sechaba kumuuliza kama alilipa bili ya maji maana wamekatiwa maji,sechaba anasema alilipa na kwamba alipokea sms kuwa maji yatakatwa na HI inafanya uchunguzi zaidi,lerato analalamika ana wateja na wanahitaji maji. Lerato anamwambia mfanyakaz wake aende jikon atafute maji yoyote amwoshe mteja

Nikiwe anaenda ofisin kwa sechaba,sechaba analalamika kuhusu maji kukatika na kwamba wafanyakaz wengi wameahindwa wasili kazin SG sababu ya ukosefu wa maji,nikiwe anasema sio kosa lao ni la barker na kwamba anamfata ili asiwasababishie hasara

Lerato analalamika ukosefu wa maji,kamo anamwambia ana shida ya kuongea nae,na kwamba obakeng kabadilika kawa mtu laini kiasi cha kumshangaza na kwamba alimpenda sababu ya ukauzu na sio kama alivyo kipind hiki. Lerato anamwambia amwachie aphiwe ni mzigo wake


Ofisin kwa barker,rajesh anajaribu kumwambia barker kuhusu sheria zinavyowabana kwa kosa walilonalo ila barker anataka kusikia suluhisho,kisha anamwambia rajesh aondoke ofisin kwake nikiwe anaingia na kumtaka barker atafute suluhisho haraka maana linawaathiri hata wao na wafanyakazi wao,barker anasema wanafanyia kazi

Morogwa anaenda ofisin kwa sechaba akiwa na furaha maana kapata majibu mazuri ya test,sechaba anampa mkataba na kumtaak akausome vizuri na kuusaini

Linc yupo gerezan katembelewa na nina,linc anamwambia nina kamuita amsaidie ishu nzito,nina anagundua linc anataka msaada wa kutoroka gerezani,linc anamuahidi kiwango kinene cha pesa

Zukisa anamlaum matlala kwa usalit na kumwambia uhusiano wao umeishia hapo

Nikiwe akiwa duncan anamkuta kgotha kakosa raha,anamuuliza nini tatizo,kgotha anamwonyesha karatasi la talaka,nikiwe anashangaa,kgotha anajiapiza atapigania haki yake hadi mwisho atahakikisha anamfilisi tyson na kumrudisha kwwnye hali yake ya awali(umaskini)nikiwe anauliza kuhusu watoto wao,kgotha anasema sio wa tyson bali wa dada yake kgotha ambao waliwaasili na kuwalea kama watoto wao,nikiwe anamuaga akisema ana appointment na mtu hapo duncan

Obakeng akiwa home,anatoka sebulen,mara anarud anakimbia akimuona jamaa mwenye silaha,obakeng anaweweseka akiomba asiumizwe na kuwa hajui chochote,nina anatokea na kumbembeleza akimwambia hamna mtu hapo mlangoni
 
Tuesday

Papa g anamuuliza nina alienda kufanya nini gerezan,nina anajibu alienda kumuona mteja. Nina anamshauri obakeng akubali matibabu ili arudi kwenye hali yake ya kawaida,obakeng anakataa na kusema hawez ishi na vichaa hospitalin bora afe,nina anapata wasi wasi

Lerato anamfata brad na kumlalamikia kuhusu ukosefu wa maji na kumtaka wamlipe fidia kwa hasara anayoipata,brad anamuahidi atafikisha kwa wakubwa

Morogwa anarudisha mkataba kwa sechaba bila kuusain akitaka kumuona nikiwe,huku akilalamika mkataba hauna haki zake kama muathirika wa TB na kutaka mabadiliko apewe kipaumbele kwa sababu ya ugonjwa alioupata,sechaba anamwambia SG haihusiki na TB aliyoipata na kama anataka kazi akausain mkataba

Nina anakubali dili la linc ila anahitaji milion 5 za souz na asilimia 3 za SG huku akisema barker atamsaidia kwenye masuala ya madini. Linc anakubali mashart ya nina

Morogwa anawashawish wenzie mgodin kupigania haki zao bila kuogopa kutishiwa ukosefu wa ajira,morogwa anawaambia atawasaidia huku akijiita winnie mandela wao.

Aphiwe yupo na obakeng shebeen ila obakeng full mawazo,aphiwe anampigia simu kamo kumuuliza maendeleo ya kazi the rec na ukosefu wa maji,kamo anasema skhu kawaletea maji so kazi wanafanya vizuri,obakeng anamwambia aphiwe amwambie kamo asifanye kazi sana maana ni mjamzito,aphiwe anafikisha ujumbe,calvin anatokea na kwenda kaunta,obakeng anamwita na kumwambia wawe marafiki maana wamepitia magumu.aphiwe anamuuliza calvin kilichotokea,calvin anasema anachojua alisalimika. Obakeng anasema anataka kuwa baba kamili hataki ona mwanae anakosa malez ya wazazi kama yeye

Nina yupo na wafanyakazi wake ofisin wakipanga mipango ya kumtorosha linc,gabr kwa umbea anaingia ghafla,kuulizwa shida anasingizia kaja kulalamika hamna maji chooni hapo shebeen. Nina anasema watasuluhisha so aondoke

Sechaba anapeleka madumu ya maji home kwake,lerato anamtaka akalete mengine ila sechaba anasema hawez hana nguvu nyingi,sechaba anaaga kuondoka ila lerato anamtaka apeleke hayo maji bafun na kila kona inayohitaji maji,sechaba anabaki kulalamika mwenyewe

Gabriel kwa umbea anaenda ofisin kwa nina na kutomkuta nina ila baunsa akaingia na kumuuliza anafanya nini,gabr akasema anashida na nina so anamsubiria hapo,jamaa akaondoka,gabr akaanza pekua ofisin kwa nina ka kukuta raman ambayo nina kaiandaa kwa kumtoroshea linc. Gabr anaipiga picha kwa simu mara anamsikia nina akitoa maelekezo nje gabr anarud kukaa,nina anaingia na kushangaa kumkuta gabr hapo,gabr anaongelea bishara anayotaka kufanya na nina ila nina anasema nafasi imejaa

Obakeng anatoka kaunta na vinywaj anawapa aphiwe na calvin,wakiwa wamekaa calvin na aphiwe wanamwambia kuhusu majukumu ya ulezi,obakeng anashangaa mlangon na kuanza kuhisi kuna mtu mwenye bunduki anainuka akimwambia huyo mtu aondoke huku akitoa bastola kuwa atamshoot,calvin na nina wanamwambia hamna mtu hapo anayemlenga ila obakeng bado anamwona mtu,wateja wanaogopa na kuanza kuondoka,calvin anambembeleza ampe bastola atamshot yeye,obakeng anampa bastola calvin akimwambia amshot huyo mtu ila calvin anamwambia hamna mtu,obakeng kuangalia haon mtu anaishia kupiga kelele za kutaka calvin amshot huyo jamaa

Matlala na morogwa wameitwa ofisin kwa sechaba,sechaba analalamika watu wamemfata wanalalamikia tabia ya morogwa mgodin ya kutaka uhuru,anamwonya morogwa aache la sivyo atakosa ajira

Barker,rajesh na brad wapo duncan bar,brad anafikisha ujumbe kuwa watu wanataka walipwe fidia kwa hasara waliyoipata kutokana na ukosefu wa maji. Barker hajali ila rajesh anasema bora wawalipe fidia kuliko kupelekwa mahakaman

Home kwa papa g Obakeng analia huku kashika kisu,nina anambembeleza ampe kisu ila jamaa hakubali

Duncan hotel ina maji ya kutosha,gabr anasema barker mjanja kaweka maji tele hotelin kwake,gabr anamwambia nikiwe kuhusu biashara anayoitaka kuifanya ya samaki na chips,kisha anasema watachelewa movie,gabr anamwambia atangulie chin atamkuta kisha anaangalia raman aliyoipiga picha kwa nina na kumtumia sms ya vitisho nina

Nina anaenda home kwa sechaba anamwambia kamo aende nae home akasaidie maana obakeng kashika kisu anaweza kujidhuru,lerato na sechaba wanapinga ila kamo anakubali kwenda na kusema akabadili nguo
 
Kuna watu wana passion na vitu flan mpaka wanakera. Toka miaka hyo watu mnazeeka na isidingo.
 
Papa g alimtuma kwenye mishen ya hatari Tanzania,kufika Tz akatekwa na kuteswa sana,huku kwa papa g nina akadhan obakeng alishafariki ila jamaa akarudi na tatizo hilo la kuweweseka sababu ya mateso aliyopata huko mafichoni
Yaani duh!

Mi niliachaga kuangalia isidingo,nimeanza tena,ila ss si unajua kuamzia njiani,baadhi ya sehem nishaelewa ila ambapo sijaelewa ni yule obakeng anavyowehuka/weweseka vile....ilikuwaje mpk akafikia hali ile?
Hebu ukipata muda Numbisa nisaidie
 
Papa g alimtuma kwenye mishen ya hatari Tanzania,kufika Tz akatekwa na kuteswa sana,huku kwa papa g nina akadhan obakeng alishafariki ila jamaa akarudi na tatizo hilo la kuweweseka sababu ya mateso aliyopata huko mafichoni
Asante sn,nimekusoma!
 
Back
Top Bottom