Africa football league iwe somo kwa tamasha la simba day na siku ya mwanachi

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,358
9,230
Hi everyone...

Jana ilikua uzinduzi wa michuano mipya na mikubwa zaidi kwa sasa barani Afrika yaani Africa football league...

Sherehe zilifana sana, watu walijitokeza Kwa wingi Sana tena mapema ili waweze kushuhudia burudani mbalimbali. Mageti yalifunguliwa mapema kabisa na watu kuzama ndani.

Utaratibu ulikua mzuri sana watu walipanga mistari na kuhudumiwa Kwa haraka, hakuna aliyesukumwa wala kupigwa kirungu na mgambo.

Nirudi kwenye mada, Hapa bongo kuna matamasha makubwa mawili ya soka kila mwaka. Hapa nazungumzia Simba day na siku ya mwanachi. Ni matamasha ambayo yamekua yakipata umaarufu kila mwaka lakini yamekosa ubunifu zaidi.

Kila mwaka tambo zimebaki kwenye kujaza uwanja. Hii Kwa sasa sioni kama ina umuhimu sana maana tayari watu wameshajua na Wana mwamko mkubwa lakini bado kuna kitu naona hua kina-miss.

Mwaka huu Yanga waliweka kiingilio cha elfu kumi kwenye jukwaa la mzunguko na ikaonekana kuathiri watu kushindwa kuja Kwa wingi siku ya tukio. Lakini kimsingi siamini kama hiyo ndo ilikua sababu.

Naamini Jana watu wamejifunza jinsi ya kuandaa tamasha. Kumbuka msingi wa Yale matamasha ni kutoa burudani Kwa mashabiki na kuifurahia timu Yao ni kama sikukuu. Hivo inabidi maaandalizi yawe ya viwango vya juu. Kwa mfano Jana Ile show kabla ya game kuanza ilikua Babu kubwa.

Kwanza show ilifanyikia uwanjani (kwenye pitch) sio pembezoni lakini pitch ilikua imefunikwa ili isiharibiwe.. Show ilikua imepangwa ikapangika. Sio Ile msanii anapanda jukwaani na kuanza kulazimisha watu waimbe. Jana Alikiba aliimba Ngoma moja Tu, show yake haukuaizi dakika nne lakini ilibamba sana.

Kwakweli tamasha likiandaliwa Kwa viwango Kama vile usishangae hata watu maarufu kama wacheza mpira na wasanii toka sehemu mbalimbali duniani wakawa wanakuja kushuhudia haya matamasha lakini tukifanya Kwa mazoea mashabiki watachoka hata kuja uwanjani wataishia kusubiri muda wa mechi Azam TV...

Ni hayo Tu.
images%20(2).jpg
 
Kwenye system ya watu kuingia ndani hata mimi nimeipenda. Kulikuwa na foleni kubwa lakini ilikuwa inatembea.

Wale vishoka wakuuza tiketi jana walinyimwa nafasi maeneo ya pale uwanjani.

Ikawabidi wajitenge nje kidogo na kuwahamasisha bodaboda wa pale uwanjani wawe wanatangaza sehemu zinapopatikana tiketi.

Ile sold out iliwakatisha tamaa kusogea uwanjani wale watu ambao hawakuwa wamekata tiketi.

So hapo vishoka walionunua tiketi za mzunguko walipata hasara sana.

Hata wale wachache ambao walifika uwanjani wakiwa hawana tiketi walikutana na mfumo mpya ambao uliwapa wasiwasi kununua tiketi za vishoka.

Kwasababu jana tiketi likiwa ina panchiwa mara tatu ukiwa katika mtiririko wa foleni. Tofauti na zamani ambapo ilikuwa unaweza kuongozana na mwenye tiketi mpaka kwa mkaguzi aipanchi ndio ulipie.

Jana ilikuwa ni eidha ununue tiketi kabisa bila kujua kama kweli ina kifurushi halafu ukapanga foleni mwisho wa siku kwenye kui scan ibainike ni card tu ambayo haina tiketi.
 
Hii ndo inatakiwa kwenye zote zinazokuja nikikumbuka siku ya game ya yanga na usma Alger watu waliishia kupigwa na kuvunjwa mbavu kisa utaratibu mbovu wa kuingia ilikua n aibu Sana. Tubadirike sema inshu ya vishoka bongo n ngumu kuisha coz nahisi mtandao wake n mpana
 
Back
Top Bottom