Mada: Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester

Ninayo Forester tangu 2010 manual transmission yenye Turbo (kidirisha kwenye bonnet).Ni imara sana ila kwenye foleni za Dar inakula mafuta kwenye safari ndefu inakula mafuta kawaida.Haziharibiki hovyo hovyo ila ikiharibika spea zake ziko juu na nyingi haziingiliani na Toyota.Shock up tu ni karibu laki 2.Ni 4AWD hazinasi kwenye tope;mchanga nk.Kwenye long route V8 Landcruiser ndiyo huwa naona zinani overtake....
Huyu Mnyama anapendeza sana akiwa STI.
 
Kuna toyota shockup inafika hata 500k.
 
Asante sana kwa ushauri huu nataka niivute pia
ukweli ni kwamba subaru ni gari nzuri sana natumaini ukinunua autajuta kwani
1. aina magonjwa
2.kama ni mtu wa kusafiri itakupa utulivu kwa barabara
3.mafuta inakula kawaida kabisa
4.kwenye barabara za vumbi linapiga bila shida

hasara ya subaru
jamii inamtazamo wanaomiliki na kuendesha subaru ni vijana wahuni

ila nunua tu autojuta
 
Kati ya Subaru forester crosssport na Subaru forester XT ipi ni tamu zaidi??
Najua zote ni engine moja tofauti ya body lkn ipi inafaa zaid
 
Kwa niaba ya watu wengine.. kubali kusikiliza ya wanaokwambia subaru nimekaa nayo miaka bila kwenda garage au sikiliza uhalisia.
Gari zote ni nzuri lakini kuna competitive advantage ya nyingine. Mtu anakwambia nafunga oil filter ya subaru 35,000 nasahau nani kakwambia wamili wa toyota wanafunga oil filter kila siku? Oil filter 10k na unaenda nayo service to service.

Ni kweli subaru tena upate yenye ej20 au ej25 zina performance nzuri lakini achana na maneno ya V8 ilisoma namba performance haipimwi na mtu ambae hajui mnashindana. Kufanya service ya subaru inahitaji mtu mwenye kipato cha kuifanya gari yake iishi vizuri Subaru sio gari imara ndo maana haiwezi handle service za mtaani kama toyota na naona watu wanazidi comment ati subaru ni reliable kuliko rav4 nendeni mtaani mkaone hizo fozzy zilifokufa engine na rav4 zinavodumu misukosuko.

Kingine ni sawa zipo rav4 full time 4wd lakin AWD ya forester ni bora sana na inaweza kukuhakikishia kutatua changamoto nyingi kwenye barabara kuliko rav4. Twende kwenye performance toyota wana engine ngumu na imara za kumudu stress kama hitting redline na kuna emgine zilisukwa zinakubali na kuhandle stress za nguvu kubwa unlike subaru chezea redline ununue engine mpya, mod gari yako uihesabie siku za kuendesha. Maamuzi ni yako.
 
Sio zote kaka kuna legacy ambazo ni Sedan type

Gari naipenda hii, acha tu. 2021 yabidi niagize In Sha Allah!!
 
Nimekuwa na mahaba mazito na brand ya Subaru, specifically forester ijapokuwa sijawahi kuiendesha brand yeyote ya Subaru. Kwa sasa ninatumia Toyota wish model 2003 na sio mbaya.

Inanitimizia mahitaji yangu yote sema inanisurubu kwa uhitaji wa genuine spare parts. Pia imeanza kunisumbua Hadi ninafikiria kuipiga gari total check up kuangalia spare parts zake kama zipo fiti au zinahitaji replacement coz I no longer trust them.

Ninafikiria kununua forester, wanaolijua hili yari naomba mnichambulie haswa kwenye ulaji wa mafuta na ubora wa spare parts. Asanteni.
 
Ni gari nzuri sana.

Lakini ingekuwa poa kama ungejielekeza kwenye Forester XT Yenye Engine ndogo/ Ambayo haina turbo.
 
Heri ya mwaka mpya ndugu zangu naombeni msaada wa taarifa za hiyo gari kuhusu spare na kama inadumu vzuri nataka kuagiza moja kwa moja toka japan ahsante.
 
Heri ya mwaka mpya ndugu zangu naombeni msaada wa taarifa za hiyo gari kuhusu spare na kama inadumu vzuri nataka kuagiza moja kwa moja toka japan ahsante.
Yeah zinadumu vzr tuu..
Confidence in motion,
 
Heri ya mwaka mpya ndugu zangu naombeni msaada wa taarifa za hiyo gari kuhusu spare na kama inadumu vzuri nataka kuagiza moja kwa moja toka japan ahsante.
ni gari nzuri sana ndo nayotumia hapa chukua non turbo ndo utaiinjoi mjini ila kama ni mzee wa fujo chukua turbo ili upate ile ladha ya high speed.
 
Back
Top Bottom