Machache kuhusu kupoteza kumbukumbu

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,251
14,232
Habarini wanajamii,

Naomba nizungumzie kwa uchache sana niyajuayo kuhusiana na ugonjwa wa kusahau ama kupoteza kumbukumbu unaojulikana kitaalamu kama amnesia.
images.jpeg


Kusahau ni kushindwa kukumbuka au kuweza kutengeneza kumbukumbu mpya kabla/ baada ya hitilafu kutokea kwenye mfumo wako wa kuhifadhi kumbukumbu.

Sasa tuanze mdogo mdogo.

Kikawaida kumbukumbu hujengwa na mambo 3:

- Kwanza ni usajili wa kumbukumbu (Registration) ambapo hapa akili yako itaweza kuanzisha kumbukumbu mpya.

- Jambo la pili ni kuhifadhiwa (Encoding)

- Na mwisho kabisa ni kuikumbuka hiyo kumbukumbu yenyewe unapoihitaji (Retrieval).

Hivyo mapungufu ya eneo lolote kati ya hayo yanaweza kukupa aina fulani ya usahaulifu, ambapo inaweza ikawa:

- Retrograde amnesia: Hapa mtu anasahau matukio ya nyuma kabla ya hitilafu kutokea, au

- Antegrade amnesia: Ambapo hapa mtu anashindwa kuunda kumbukumbu mpya baada ya hitilafu kutokea.

Vile vile, usahaulifu unaweza ukawa ni:

- Wa muda mfupi na baadae kupona wenyewe (Transient): Mara nyingi hutokea kwa wale waliopata ajali iliyohusisha kichwa au baadhi ya watu wanaotumia dawa fulani.

- Wa kudumu (Permanent): Hasa kwa wagonjwa wenye maambukizi yanayoathiri ubongo (Encephalopathy) au mashambulio ya moyo ( e.g. Stroke),

- Au wa kuendelea (Progressive): Hasa kwa magonjwa ya utu uzima ambapo mtu anapoteza kumbukumbu taratibu kadri anavyozeeka, akianza kusahau majina kisha matukio.


Jambo la kushangaza ni kwamba mtu aliepoteza kumbukumbu mara nyingi huwa hapotezi kipawa/ujuzi alikua nao bila kujali aina ya usahaulifu wake, yaani kama alikua ni dereva au mchezaji mpira basi ataweza kuendelea kuendesha au kucheza mpira.

Watafiti wanasema muziki unaweza kumsaidia mtu kurudisha kumbukumbu zilizopotea. Hata kutembelea sehemu ulizowahi kuishi zamani kunaweza kurudisha baadhi ya kumbukumbu.

Nawaacha na hii, kwa yeyote mwenye wasaa akaitafute movie iitwayo Memento, inaweza kukupa machache niliyodadavua lakini pia itakuburudisha kwa drama zake.
images (1).jpeg


Muwe na siku njema!
 
Back
Top Bottom