Fahamu kuhusu ugonjwa wa kupoteza ufahamu au kusahau (Dementia)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia) ni nini?
Neno ‘Dementia’ (ugonjwa wa kupoteza ufahamu) linaelezea dalili mbalimbali kama vile upotezaji wa kumbukumbu, matatizo ya kufikiria au kuongea, na mabadiliko katika hisia na tabia.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia) husababishwa na magonjwa ya kimwili ya ubongo sio kwa kuzeeka na huwezi kuepukika. Kwa usaidizi mtu anaweza kuishi vyema akiwa na huu ugonjwa.

Dalili za Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia)
Kila mtu aliyeathiriwa na ugonjwa wa kupoteza fahamu (dementia) ni wa kipekee na ataushuhudia kwa njia yake kivyake. Mtu aliye na ugonjwa wa kupoteza fahamu atakuwa na matatizo kwa baadhi yafuatayo:

• Kumbukumbu ya kila siku – kusahau alichokuwa akifanya hata mapema kidogo siku hiyo, kurudia swali lile lile tena na tena

• Kumakinika, kupanga au kuandaa – matatizo ya kufanya uamuzi, kutatua matatizo au kufanya majukumu (kwa mfano, kupika chakula)

• Lugha – Matatizo ya kupata neno sahihi la kitu au kufuatilia mazungumzo

• Kuamua umbali na kina cha vifaa – kwa mfano unapotumia ngazi

• Kusahau wakati au eneo – kuchanganyikiwa kuhusu siku na tarehe, au kupotea katika eneo linalofahamika.

Pia matatizo haya ya kumbukumbu na kufikiria, mtu aliye na ugonjwa wa kupoteza fahamu (dementia) anaweza pia kuwa mwenye mhemko, wasiwasi, hasira, kutotaka kuzungumza au mwenye huzuni.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia) ni kitu kinachoendelea, kumaanisha kuwa dalili huwa mbaya zaidi kadri muda unavyosonga.

Kwa baadhi ya aina za ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia), mtu anaweza kuona vitu ambavyo havipo kabisa (maluweluwe) au anaweza kuendelea kuamini vitu ambavyo si vya kweli. Mtu anaweza kuchanganya ya sasa na yaliyopita.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia) huendelea kuwa mbaya. Hivi ni kusema kuwa, dalili huanza zikiwa ndogo lakini huendelea kuwa mbaya kadri muda unavyosonga. Jinsi dalili zinavyozidi kuwa mbaya polepole au haraka hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Hata baada ya dalili kudhihirika na daktari kufanya utambuzi ya ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia). Watu wengine hudumisha uhuru wao kwa miaka kadhaa juu ya kuelewa pamoja na usaidizi unaofaa.

Aina za Ugonjwa wa kupoteza fahamu (Dementia)
Kuna aina nyingi za ugonjwa wa kupoteza fahamu(Dementia). Zile maarufu zaidi vimeorodheshwa hapa chini. Dalili ya hivi zinaonekana kutofautiana.

Ugonjwa wa Alzheimer’s ndiyo aina maarufu ya ugonjwa wa kupoteza fahamu na upotezaji wa kumbukumbu mara nyingi hutambuliwa kwanza.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu wa mishipa ya damu, ambacho kinaweza kufuata kiharusi, husababisha matatizo ya mapema ya kumakinika au kupanga.

Pia mtu anaweza kuwa na ugonjwa wa kupoteza fahamu wa mchanganyiko, akiwa na ugonjwa wa Alzheimer`s na ugonjwa wa kupoteza fahamu wa mishipa ya damu. Dalili zinaweza kuwa mchanganyiko pia.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu wa Lewy bodies ni aina isiyo maarufu sana. Dalili za mapema zinaweza kujumuisha arifa zinazotofautiana kwa muda, ugumu wa kukadiria umbali, maluweluwe na matatizo ya mwendo.

Ugonjwa wa kupoteza fahamu wa Fronto temporal pia si maarufu sana. Unasababishwa na madhara kwenye sehemu ya mbele na/au pande za ubongo. Dalili za mapema hapa zinaweza kuwa mabadiliko katika tabia, kuwa na wasiwasi mwingi na hisia hata kupoteza stadi za lugha.


===========

Dalili za Ugonjwa wa Kupoteza Kumbukumbu kwa Muda Mfupi
Kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi hutokea wakati mtu anasahau kitu alichofikiri na amejifunza hivi karibuni. Dalili zinazojulikana zaidi ni:
  • Kusahau mahali ulipoweka funguo za gari lako au miwani ya jua
  • Kusahau ulichokuwa ukifanya kabla ya kuingiliwa
  • Ugumu wa kukumbuka majina ya watu wapya unaokutana nao
  • Kulazimika kuuliza maelekezo mara kwa mara
  • Kuhisi kulemewa na kazi rahisi
  • Kuhitaji kuandika vitu mara nyingi zaidi kuliko hapo awali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom