Mabosi zangu wananiandama bila sababu

Mabosi zangu wananiandama bila sababu

Mkuu kua makini sana siku zote ukiwa chini ya hizi Halmshauri na ukaonekana ni mchapa kazi mzuri basi jiandae kwa majungu na mizengwe ya kila namna ili mradi wakukatishe tamaa,Trust me kuna mtu anakuona kwa juhudi zako na report yako iko safi kabisa.
 
Kazi gani ya Halmashauri inayokupq pesa directly?ugomvi wenu unajua ni mgawo wa rushwa na bakhashishi
 
Kumbe upo idara ya ardhi... Hiyo idara nimeshuhudia watu mpaka kulogana... Itakua wewe una ile ya kijifanya mtakatifu wakati idara hiyo watu wanpokea rushwa pitiliza jiandae kutengenezewa zengwe kuhamishwa
Ameshasema anapata kazi za hela akiwa ofisini alafu haujiongezi!!
 
Vaa shati la takukuru/ama shati limepigwa chata hapa kazi tu ...beba na kadi ya chama mkononi.....alafu ongea kisukuma....kwenye simu hakikisha wanasikia...kama hujui jifunze maneno mawili matatu....utapata matokeo chanya mkuu...duniani mbinu.....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji39][emoji23][emoji23]
 
Mtoa mada me nakushauri ufanyie kazi huu ushauri ulotolewa na wengi wa kujaribu kusocialize na wenzio.

Halafu uje utupe mrejesho baada ya muda hali imekwendaje.
 
Sina ligi na mtu
Ila nikiwa karibu na yeyote yataanza maneno na ligi
So nilivogundua hilo nikaamua kukaa pemben,ila nayo imegeuka vita
Inshort mtu anaweza onekana si lolote si chochote ila nikianza mtrain na kufanya naye kazi anageuka lulu,then wanamtumia kuniumiza
Baada ya kutambua hilo nikaamua kuwa selfish,ili nilijulikane tacticts zangu,tatizo nayo imegeuka gumzo kuwa siko social wakat mwanzo sikuwa hivyo
Tatizo na wewe kiherehere kimekuzidi inaonyesha dhahiri unapenda ligi
 
Kazi gani ya Halmashauri inayokupq pesa directly?ugomvi wenu unajua ni mgawo wa rushwa na bakhashishi
Sifatilii rushwa mie
Rushwa anakula maza na rafiki zake,hata wakija takukuru wataona
Natimiza majukumu yangu baaasi
Amekaa serikalin miaka zaidi ya 59 ,hajawah pata ukurugenzi
Anakuja shindana nami kabinti kadogo kakukazaa
Apambane na hali yake
 
Mtoa mada me nakushauri ufanyie kazi huu ushauri ulotolewa na wengi wa kujaribu kusocialize na wenzio.

Halafu uje utupe mrejesho baada ya muda hali imekwendaje.
Siwezi socialize na nyoka
Mtu anajidai mlokole
Akikupiga mgongo anaenda kwa mkurugenzi kukunenea mabaya ambayo hujafanya? Never
 
Kumbe upo idara ya ardhi... Hiyo idara nimeshuhudia watu mpaka kulogana... Itakua wewe? Kama una ile ya kijifanya mtakatifu wakati idara hiyo watu wanpokea rushwa pitiliza jiandae kutengenezewa zengwe kuhamishwa au kupigwa juju
Hawawezi niloga mie mfipa
Hakuna hata panya nyumban kwao atakaye salia
Kama hawaamini wajaribu
Sina vyeti feki, sikuforce kuja ...
Mungu aliyenileta hapa ndiye anayejua hatma yangu na si mwanadamu atakaye kufa na kuoza kama mie.
 
No inachosha aiseeh
Kama nimeomba ruhusa ya kula sikukuu,nimenyimwa wakati wengine kibao wamepewa
Na muda mwingi hata ofisini hawaonekan
Sitak hata hizo zawadi zao kwani wananinyanyasa kisaikolojia
Kwa nini usijaze likizo ya mwaka? Ambayo ni haki yako dogo?
 
Habari za jioni wana jf.
Niende kwenye mada. Ni hivi nafanya kazi ofisi ya serikali.Ni kijana kwenye late 20's. Ni Afisa flani niliyeajiriwa like 5 years ago.Nina kadegree.

Ishu iliyofanya nilete uzi huu,boss wangu kwa maana ya Mkuu wa idara,mkuu wa kitengo na wazee flani wananiandama sana ofisini.

Niko vizuri kwenye kutimiza majukumu yangu.Nikifika job sina muda wa kupoteza kwenye machai wala soga za siasa,mpira,udaku ama lolote.Nikifika after salamu za hapa na pale na kusaini naket kwenye meza yangu napiga kazi kwa malengo niliyojiwekea.Nikiri uwezo wa kazi ninao na ni mwepesi kuelewa mambo.

Kwenye chai ama lunch zao siendi. Nashukuru Mungu nimepata wigo wa kufahamiana na watu wengi sana ambao kifupi wananiletea kazi za hela si haba.Yani nikikubaliana na mtu,njoo kesho uchukue kazi yako ujue itakuwa hivo.Napenda sana kukeep promise na kuitimiza.Hiyo imefanya nipendwe na wateja wengi na hata maboss wa idara nyingine ni rafiki zangu sana ingawa ni watu wazima.wakiwa na ishu kwenye field yangu lazima wanitafute.

Wafanyakazi wenzangu kwenye idara wanawahi job 12 kamili wapo ila ikifika saa 4 asubuh hawapo,ama wakiwepo ni kuzunguka kwenye korido na maofisini wakipiga soga.
Wanachukua ruhusa kila mwezi na wanapewa,ila nikiomba mie nitawekewa mizengwe hadi nijute. Wengine wanakuja j3 na j4 then hawaonekani hadi j3 inayofata na inakuwa siyo kesi.

Ila itokee nisionekane hata siku moja inageuka kesi,najadiliwa hadi kwenye vikao vya idara.Nimechoka kusakamwa na hawa maboss.Najiuliza why me.Sina dharau wala shobo na mtu.Nawaheshimu kama maboss zangu Sema tu nimejiweka mbali na hao maboss kwani sina tabia ya kujikombakomba bila sababu kwa mtu.

Wananichafua kila sehemu.hata kama jambo sijafanya wala kusema nitatajwa tu.imagine boss wako anamwita mtu anayehisi ni mpenzi wako anamwambia kaa mbali na flani hafai.

Naombeni ushauri nifanyeje? Ama nihame halmashauri manake imekuwa too much.
Atakaye vumilia mpka mwisho ndo mshnd
 
Sifatilii rushwa mie
Rushwa anakula maza na rafiki zake,hata wakija takukuru wataona
Natimiza majukumu yangu baaasi
Amekaa serikalin miaka zaidi ya 59 ,hajawah pata ukurugenzi
Anakuja shindana nami kabinti kadogo kakukazaa
Apambane na hali yake
Mwanzo umesema wafanyakazi wenzio na sasa hivi unamtaja specifically,Aihitaji degree kujua nani mkorofi na mpika majungu
 
Back
Top Bottom