SoC03 Maboresho shirika la ndege Tanzania ATCL

Stories of Change - 2023 Competition

Mr godwin

New Member
Jul 29, 2021
2
1
MABORESHO SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATCL)
Shirika la ndege tanzania (ATCL)
Ni shirika la kiserikali linalojihusisha na usafirishaji kwa wa mizigo na watu kwa njia ya anga lililopo chini ya mmiliki wa Ndege za serikali TGFA

Toka shirika hili lifufuliwe chini ya uongozi wa hayati John pombe magufuli shirika hili limekuwa likipata hasara mwaka baada ya mwaka,kwa uchunguzi wangu zifuatazo ni changamoto na namna bora yakuendesha shirika hili

CHANGAMOTO ZA SHIRIKA
1 SHIRIKA KUKOSA UBUNIFU KWENYE KUJITANGAZA NA KUTANGA HUDUMA ZAKE

Apa watanzania wengi mtakubaliana na mimi shirika letu la ndege Halina ubunifu kwenye kujitanga na kuvutia wateja kama ambavyo mashirika shindani yanavyofanya mfano mzuri precision air wao wanatumia mpaka wasanii wakubwa kutangaza huduma zake kitu ambacho kinafanya watu walipende shirika hilo ukilinganisha na air Tanzania

2 SHIRIKA KUTOMILIKI NDEGE ZAKE LENYEWE

changamoto nyingine ninayo iona kwenye shirika letu la ndege ni ndege kumilikiwa na TGFA kitu ambacho kinafanya kuwe na muingiliano katika kuendesha shirika na kusababisha kutojua ni nani hasa anakwamisha shirika hili lisiende mbele

3 SHIRIKA KUKOSA WATU WENYE UJUZI NA BIASHARA YA NDEGE

Kulingana na ukosefu wa elimu ya biashara hasa hii ya ndege,na mlundikano wa hasara kila mwaka Niwazi kuwa ndani ya shirika hakuna watu sahihi au wapo lakini bado hawajui namna gani wanaweza kufanya ili kukuza biashara ndani ya shirika


UTATUZI
1 SHIRIKA KUFUNGUA MATAWI NA WIGO MPANA WA KAZI ZAKE
kama ambavyo mashirika makubwa ya ndege duniani hufanya ukitaka kufanikiwa katika usafirishaji wa anga ni pamoja na kufungua matawi nchi mbali mbali mfano shirika letu linandege kubwa kubwa zakusafiri umbali mrefu tunaweza kufungua matawi sehem mbali mbali duniani ambapo tutavifanya kama vituo mtu anaweza kusafiri kutoka dar hadi dubai lakini tukawa na kituo nigeria hapo maana yake tutabeba watu wa nigeria na dubai kwa wakati mmoja
2 SHIRIKA KUTUMIA SECTA MBALI MBALI KUJITANGAZA

Mfano tunaweza kutumia timu zetu za mpira zenye mashabiki wengi nchini kutangaza huduma zetu kwa kuwa wadhamini wa timu au wa ligi yetu wa ndani ili kuongeza thaman,pili tunaweza kutumia wasanii wetu kutangaza shirika letu,

FAIDA
Kupitia shirika letu kukua tunaweza Kuwa na uwezo wa kusafirisha watalii kutoka nje moja kwa moja hadi Tanzania tukajikuta tumekuza utaliii wetu kupitia shirika la ndege

ASANTE JAMII FORUMS KWA HII FURSA
 
Back
Top Bottom