Hiyo sio dawa. Wanasema unaweza kumuua mjumbe lakini huwezi kuua ujumbe, au fikra ya mjumbe, you can never kill an idea.
Leo ni UAMSHO. Kesho ataibuka mwingine kubeba ujumbe, kubeba ile idea iliyoko vichwani mwa baadhi ya Watanzania, kwamba hawataki Muungano. Kwa hiyo, hata ungefuta usajili wao na kuwafunga, hata ungewapiga risasi UAMSHO wote, kesho hiyo idea itachipuka tena. Huo ndio ukweli. Martin Luther King, wa Marekani, alisema, "a truth buried to the ground will rise again"! Huwezi kuangamiza ukweli. Hata ungewapoteza, nini kufuta usajili, hata ungeficha milele viongozi wa UAMSHO wote, hiyo si dawa.
Dawa ni nini?
Nimesema "baadhi" ya Wananchi hawataki Muungano. Baadhi. Kinachotusumbua mpaka sasa ni, "baadhi" hao ni wangapi wetu? Jibu la hilo swali, ukipata jibu la hilo swali ndio umeanza kutafuta dawa!