Mabomu ya machozi yarindima tena Zanzibar leo

Mabomu ya machozi yarindima tena Zanzibar leo

[h=1][/h]Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/06/2012 // Habari // 1 Comment


Monday, 18 June 2012
Salma Said, Zanzibar
MJI wa Zanzibar jana uligubikwa na vurugu mpya za kupinga Muungano na kuwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Uamsho waliokuwa wakiandamana.
Tukio hili lilitokea katika eneo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Ugunja, ambapo wafuasi hao walikuwa wakiandamana kuelekea katika mhadhara uliopangwa kufanyika katika eneo la Donge, nje kidogo ya Mji wa Unguja.
Awali, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake, Mussa Ali Mussa lilizuia mhadhara huo, lakini viongozi wa kundi hilo walikaidi na kuwaamuru wafuasi wao kuandamana kuelekea katika eneo walikopanga kufanya mhadhara huo.
Masemaji wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohammed Mahina aliithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.
Hata hivyo, alikataa kutoa maelezo zaidi kwa madia kuwa hajapata taarifa kamili kutoka katika eneo la tukio.
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu kadhaa tunawashikilia, lakini sina taarifa za ndani zaidi, sijawasiliana na Kamanda wa Polisi wa eneo hilo,” alisema Mhina.
Vurugu hizo zilibuka mara baada ya kundi hilo kufika eneo la Mahonda karibu na Kituo cha Polisi, ambako askari polisi waliokuwepo eneo hilo waliwaamuru wafuasi hao kutawanyika, amri ambayo ilipingwa na kuwalazimisha polisi kutumia nguvu.
Polisi walilipua mabomu ya machozi ambayo yaliwafanya wafuasi hao wakiwemo wanawake na watoto kukimbia ovyo, baadhi yao wakikimbilia katika miskiti ya jirani, ambako walifuatwa na kutiwa mbaroni na wengine kujeruhiwa, kabla ya kukimbizwa hospitalini.
“Mabomu yamepigwa hadi ndani ya msikiti wa Mahonda walipokuwa wamekimbilia wafuasi hao,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo na kuongeza kuwa kuna watu walifuatwa hadi ndani ya msikiti na kupigwa kabla ya kukamatwa.
Vurugu hizo ambazo zilichukua zaidi ya saa moja, zilisababisha gari la Kiongozi wa kundi Maimam Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed kuharibika baada ya kupata ajali wakati dereva wake alipokuwa anajaribu kuwakimbia polisi, lakini hata hivyo sheikh huyo hakuwamo ndani ya gari hilo.
Baada ya kutawanywa eneo la Mahonda wafuasi hao walirudi na kukusanyika eneo la Mjini katika Viwanja vya Msikiti wa Mbuyuni, kabla ya kujaribu kwenda tena katika mhadhara huo na kutawanywa tena na polisi.
Hata hivyo, baadaye Sheikh Farid alipozungumza na gazeti hili alisema maandamano hayo na mhadhara vilifuata utaratibu.
“Tulifuata taratibu zote za polisi, lakini cha ajabu kufika Mahonda tunatawanywa na kupigwa mabomu,” alisema na kuongeza kuwa kusudio lao la kutaka kuvunjwa kwa Muungano linabaki kama lilivyo na viongozi wote wa kundi hilo wapo salama.
Alisema polisi walichofanya sio sawa, kwani wamejeruhi watu na wengine kuwafuata msikitini na kuwapiga mabomu.
Imam Mselem alikiri kukutana na viongozi wa Jeshi la Polisi ambao waliwataka wasifanye maandamano na mhadhara huo.
Mwezi uliopita vurugu kubwa zilitokea mjini Zanzibar baada ya watu wasiofahamika kuchoma moto makanisa kadhaa, magari pamoja kupora mali mbalimbali kwa madai ya kupinga muugano.
Hoja ya Uamsho imewafanya pia wanasiasa mbalimbali kutoa kauli zao, Rais wa Zaanzibar, Dk Ali Mohammed Shein hivi karibuni aliwata Wazanzibar wanaotaka kundolewa kwa kasoro katika Muugano wasubiri Tume ya Katiba na aliahidi kuwa maoni yao katu hayato puzwa.
Sisi ni viongozi tulio chaguliwa na wananchi na pindipo wananchi wa Zanzibar wa maoni yenu hayato puuzwa jitokezeni kwa wingi kutowa maoni yenu.
Chanzo: Mwananchi
 
kwakweli napata shida sn kila nikifikiria haya mambo!cna tatizo na zbar kudai muungano uvunjike!hata mi nawaunga mkono mchukue nchi yenu!....tatizo linakuja hapa,wabara kuisho kwa hofu huko zbzr.....na kuchomwa kwa makanisa na serikali ipo kimya 2!kuna nn hapa katikati?
 
KWA KWELI SASA TANZANIA INAKUWA KAMA SOMALIA AU AFGHANISTANI KWA HALI HII,HUKO ZNZ NIMEONGEA WABARA KAMA WANNE WANASEMA MAISHA NI YA HOFU KAMA VILE LABDA WAO NI WAUAJI WANATAFUTWA.kuna jamaa mmoja wa hapa ni msambaa kajenga huko znz in anasema hao hao uamsho mameamua kukata kabisa fensi yake makusudi kisa ni ili tu aondoke arudi kwao tanga,sasa maisha ya hivi kweli tutafika

"huyo jamaa yako atakuwa ni muongo, uamsho wa kweli kama mimi hawezi kufanya kitu kama hicho, kam akafanyiwa aseme ni na nani na kwa sababu gani lakini sio kila taka mtutupie wana uamsho, sisi dai letu nini tunataka ni ZANZIBAR HURU YENYE MAMLAKA KAMILI, tena kupitia kura ya maoni tuulizwe kam atwautaka muungano ama laa"

 
vurugu jana sunday (17th June) na leo haya na maamir wetu, mashaAllah

dsc-0306.jpg
 
hivi hizi vurugu za Uamsho zinaendelea na kule Pemba?
 
Hivi nyie wangazija, watumbatu mnamdai nani uhuru wenu? Mbona mnafanyiana fujo wenyewe kwa wenyewe. Kama wanaume kweli si mvuke maji mje mdai uhuru wenu huku Tanganyika?
 
BWANA YESU ANAOKOA, KWA NINI MNAUMIZA AKILI HIVI?KWA NINI MNASONONEKA?KWA NINI MNAHANGAIKA NA HII DUNIA? MPE BWANA YESU MAISHA YAKO NA KUHAKIKISHIA HUTA JUTA,roho ya hasira,chuki na mambo mabaya yataondoka nawe utakuwa mwenye furaha muda wote.KARIBU KANISA LOLOTE LILILOKARIBU NAWE LINALOAMINI WOKOVU.
AU TUWASILIANE KWA EMAIL :johnhella2007@yahoo.com hiyo email naitumia hata facebook ukisearch kwa email hiyo utanipata
 
Hivi hawa waislamu nani kawaroga?!!!! Wanahangaika na matawi wakati mizizi ya shida zao wanaifahamu. Ni serikali yao iliyowaweka katika muungano wasioutaka, lakini hasira yao inaishia katika kuchoma makanisa!!

Wanapodai mahakama ya kadhi wanaibembeleza serikali hiyo hiyo iwaanzishie!!! Na bado wanaoisujudia serikali hiyohiyo iwafanyie sensa na iwasaidie kupass mitihani!!!! Iwapo kweli hawautaki Muungano wakaichome moto hiyo ikulu yao kwani ndiyo inayoshinikiza kuwepo kwao katika muungano. Tofauti na hapo hayo maandamano yao na mihadhara ni uendawazimu mtupu!!
 
Back
Top Bottom