Hata jeshi zima likihamishiwa Zanzibar,vurugu hazitoisha. Nani asiyejua madhara ya kuishi na kero kwa muda mrefu.Magamba lazima wawajibike kwa Moreno Ocampo wasipokuwa makini.Mzizi wa madai ya uamsho ni zaidi ya tunavyodhani lakini J.K,Pius Msekwa,Rais mstaafu Amani Karume na Dr.Shein wanajua nguvu ya historia iliyopakwa matope pale Zanzibar.
Kwa wanaojua vizuri kupika proganda za kivita na uasi ni rahisi kuchochea vurugu za makundi kwa njia ya kutoa elimu hasi kwa wahusika. Haitakiwi kutumia nguvu nyingi then akili kidogo ktk kusuluhisha mgogoro unaofukuta pale Zenj,la sivyo damu itamwagika.
Tuache ushabiki usiojenga...ooh let them go, Mara polisi walikuwa wapi kudhibiti mapema-then what? Wale ni binadamu wenye akili timamu hivyo wanapashwa kusikilizwa.Kama J.K ana uwezo wa kuongea na wazee wa DSM anashindwa nini kuongea na wazee wa Zanzibar kijua namna ya kumaliza tatizo kwa njia ya amani?