Elections 2010 Mabinti watumiwa kumrushia Mbowe kombora!

Status
Not open for further replies.
Mwenye Mobile No. ya Makamba naiomba Tafadhali. Hujab yafaa kuheshimiwa!!! Tuta deal na yeye!
 
Hivi GDP inaingia wapi hapa? Hii message ni ABSOLUTELY STUPID. Ujue na huyo mdada kasema haki ya Mungu kwamba CHADEMA ni mafisadi...
Kuna watu wamezidiwa sasa.
mkuu kama GDP ya tanzania ni 24BN na tunatumia Billion 40 kufyatua picha tunazobandika kwenye miti maeneo ya simanjiro na kongwa ... na bado tunaomba ridhaa ya wananchi then we have a serious problem

hapo bado tunaachia exemption ya 700BN

bado pesa ya radar tunasubiri cycle yake iishe tuseme hatukuichukua mda umepita

iaaaiiiiichh
 
Wazee hao watu waliotengeneza hiyo ADVERT HAWANA DATA ni wahuni tu flani GDP ya Tanzania sio 24billion ni kama ifuatavyo according to CIA FACT BOOK GDP (purchasing power parity):
$57.69 billion (2009 est.)
country comparison to the world: 85 $54.43 billion (2008 est.)
$50.66 billion (2007 est.)
note: data are in 2009 US dollars
 
Nimeiangalia hii video..it's just a crap! Na walioitengeza ni vilaza waliopitiliza..

Wazee hao watu waliotengeneza hiyo ADVERT HAWANA DATA ni wahuni tu flani GDP ya Tanzania sio 24billion ni kama ifuatavyo according to CIA FACT BOOK GDP (purchasing power parity):
$57.69 billion (2009 est.)
country comparison to the world: 85 $54.43 billion (2008 est.)
$50.66 billion (2007 est.)
note: data are in 2009 US dollars
 
Kama hawa mabinti ni hivi kuhusu maswala ya GDP basi elimu bure hadi sekondari ni NECESSARY... :becky:
 
Mabinti watumiwa kumrushia Mbowe kombora!

View attachment 14326

Ama kweli hawa watu wanatuona Watanzania ma-golo, kwamba hatuna akili kabisa. Hata kama ingekuwa kweli kwamba CHADEMA kinapata ruzuku ya shs milioni 60 na ikawa kweli kwamba Mwenyekiti anachukuwa 16.7% ya ruzuku hiyo bila kutaja kama angezichukua hizo kwa matumizi ya ofisi yake au kwa mahitaji yake mwenyewe, hayo yote yangekuwa na uhusiano gani na kusema 16.7% ya pato la taifa ni dola milioni 400? Si wanataka watu warukie fikra kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA anapata asilimia 16.7 ya pato la taifa au dola milioni 400 kwa mahesabu yao?

Kuingia gharama ya kutengeneza na kuisambaza video isiyo na logic hata kidogo ni dharau kubwa kwa akili za watanzania.

Licha ya logic hiyo iliyopotoshwa makusudi, siyo kweli kuwa CHADEMA inapata ruzuku ya milioni 60 tu! Kalkulesheni ya ruzuku ni kompliketedi lakini ninamfahamu mtu aliyeshazifanyia kazi na nimemwomba data akanipatia hizi zifuatazo. Kiasi cha ruzuku kinachopewa chama chochote kinategemea matokeo ya uchaguzi uliopita kwa hiyo viwango HALALI vya ruzuku kwa sasa hivi vinategemea matokeo ya uchaguzi wa Desemba 2005. Kwa mahesabu hayo, kwa mwaka 2008/09 ruzuku halali ya CHADEMA ilikuwa shilingi billion nne, mia nne na 94 millioni wakati ruzuku halali ya CCM ilikuwa shs billion sitini na saba na 67 milioni.

Ruzuku kwa Vyama vya Siasa.JPG
 
Hawa waliotengeneza hiyo Advert ni wahuni ambao hawajui lolote hata fedha za ruzuku hazitolewi na Tume ya Uchaguzi zinapitia kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na sio NEC.
 
Sasa Ni Mtu Gani Ameweka hiyo Video? Iko YouTube so ukiigonga kuangalia inapata idadi ya watu kuiona kwahiyo More hits... sasa hivi ina watu mia tatu (300) ni wachache kuwa na hits sasa Jamii Forum ina watu kama mfano elfu tano (5,000) tukigonga hiyo kila dakika na naona hawa wanadada hawajui kuwa CCM also walipata pesa hizo saidi ya Chadema...

Kweli Tunadanganyika
 
Hamna uhusiano wowote na mambo ya msingi tunayoyatarajia kwa tanzania yetu baada ya 31 oct, Refer Askofu Kakobe!
 
Kama ni hivyo its good kwamba Jamiiforums inakuwa imejaa wapiga debe wa CCM kama ilivyo wa CHADEMA na CUF...

CHADEMA haina wapiga debe; haihitaji wapiga debe. CHADEMA ina wanachama, wazalendo, wanaoujua ukweli. CCM inahitaji wapiga debe kwa kuwa inasimiamia mfumo mbovu wa serikali, unaofanana kabisa na daladala. Daladala inasimama popote, haina vituo maalum; sera nyingi za CCM hazitekelezeki, zinapelekwa huku na huko, kama majaribio, kama vile dala dala inaposimama kati kati ya barabara, ikishusha na kupandisha abiria. Ni CCM pekee yenye wapiga debe... vyama vingine havina haja ya kupigiwa debe, kwa kuwa wanajua wanachokifanya. Kama CCM wangekuwa wanajua wanachokifanya wasingetengeneza tangazo la kipuuzi kama hilo!
 
Mabinti tu mnaanza kupiga makelele,je wakija dada zao sasa ....duh kumbe Mbowe anakunja fungu kubwa hivyo

Yani Hii Clip mbona haigusi akili kabisa? Nadhani Hakuna Haja ya kulumbana kwa vitu visivyo na ukweli!
Yani inakera sana kuona kuna watanzania humu ndani wanatetea machafu ya CCM! Kumbuka ni Billion ngapi CCM wamezichota EPA na kwenye mashirika mengine ya UMMA. Nyie hamjui kwa nini Mashirika ya UMMA yamekufa..ni kwa sababu CCM imekuwa ikitumia faida zake kujiweka madarakani. Je mnaoshabikia mmeshawahi kuziona hizo hela? Ndani ya CCM hawazidi watu 3000 tu ndio wanaozitafuna hela na watanzania, Leo mnakuja na ushabiki wa uongo....nashauri wale wana JF wasio mrengo wa CCM kuacha kupoteza muda kwa hii video isiyo na tija!
 
CHADEMA haina wapiga debe; haihitaji wapiga debe. CHADEMA ina wanachama, wazalendo, wanaoujua ukweli. CCM inahitaji wapiga debe kwa kuwa inasimiamia mfumo mbovu wa serikali, unaofanana kabisa na daladala. Daladala inasimama popote, haina vituo maalum; sera nyingi za CCM hazitekelezeki, zinapelekwa huku na huko, kama majaribio, kama vile dala dala inaposimama kati kati ya barabara, ikishusha na kupandisha abiria. Ni CCM pekee yenye wapiga debe... vyama vingine havina haja ya kupigiwa debe, kwa kuwa wanajua wanachokifanya. Kama CCM wangekuwa wanajua wanachokifanya wasingetengeneza tangazo la kipuuzi kama hilo!

Sasa hapo wewe unafanya nini kama sio kupiga debe???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom